Neuroblastoma

Imepitiwa/Imerekebishwa Jul 2024

Je, neuroblastoma ni nini?

Neuroblastoma ni aina ya saratani ambayo huota kwenye seli za neva ambazo hazijakomaa katika sehemu mbalimbali za mwili. Neuroblastoma ni saratani inayopata sana watoto wachanga, na inayopata zaidi watoto wadogo.

  • Kwa kawaida neuroblastoma huanzia kwenye tezi za adrenali (zilizopo juu ya figo) au kwenye neva ambazo ziko pembeni ya uti wa mgongo kwenye kifua na tumbo.

  • Saratani inaweza kuanza hata kabla ya kuzaliwa

  • Kwa kawaida neuroblastoma husambaa kwenye sehemu nyingine za mwili, kama vile mifupa, ngozi, na uti wa mgongo

  • Watoto huwa na matokeo bora ikiwa ni wadogo na saratani bado haijasambaa

  • Madaktari hutibu neuroblastoma kwa upasuaji, tibakemikali, na wakati mwignine tiba ya mionzi

Je, nini husababisha neuroblastoma?

Mara nyingi, madaktari hawajui kwanini watoto hupata neuroblastoma. mara chache, mtoto mchanga hurithi jeni isiyo ya kawaida ambayo husababisha neuroblastoma.

Je, dalili za neuroblastoma ni zipi?

Dalili za neuroblastoma hutegemea sehemu ambapo saratani imeanzia na kama imesambaa.

Ikiwa neuroblastoma imeanzia kwenye tumbo la mtoto, dalili zake ni pamoja na:

  • Tumbo kubwa

  • Hisia za kushiba

  • Maumivu ya tumbo

Ikiwa neuroblastoma imeanzia kwenye kifua, dalili zake ni pamoja na:

  • Kikohozi

  • Kupumua kwa shida

Mtoto wako anaweza kuwa na dalili zingine iwapo neuroblastoma imesambaa kwenye sehemu zingine za mwili:

  • Mifupa: Maumivu kwenye mifupa, udhaifu na uchovu, ngozi iliyopauka, na kuvilia

  • Ngozi: Uvimbe kwenye ngozi

  • Uti wa mgongo: Mikono na/au miguu dhaifu

Mengi kati ya haya ni dalili ambazo ni za kawaida sana kwa matatizo ya afya ya watoto.

Madaktari wanawezaje kujua kama mtoto wangu ana neuroblastoma?

Wakati mwingine madaktari hushuku uwepo wa neuroblastoma baada ya kuona uvimbe kupitia kipimo cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti wakati wa ujauzito. Wakati mwingine madaktari huhisi uvimbe kwenye tumbo la mtoto wako wakati wa ziara ya kuonana na daktari. Ili kujua kwa uhakika kama mtoto wako ana neuroblastoma, madaktari:

Ikiwa mtoto wako ana neuroblastoma, madaktari watafanya vipimo zaidi ili kuona kama saratani imesambaa, ikijumuisha:

  • Eksirei ya mifupa yote ya mtoto wako

  • Uchanganuzi wa CT au MRI ya sehemu zingine za mwili

  • Kuchukua sampuli ya uboho (kukata kipande cha uboho) ili kuchunguza saratani

Je, madaktari hutibu vipi neuroblastoma?

Madaktari kawaida hufanya:

  • Upasuaji wa kuondoa uvimbe

  • Tibakemikali (kutumia dawa kuharibu seli za saratani)

Ikiwa neuroblastoma ina sifa ambazo zinaifanya iwe hatarishi, madaktari wanaweza kufanya:

  • Tiba ya mionzi (kutumia mionzi kuharibu seli za saratani)

  • Tiba ya kingmwili (matibabu ya kuamsha mfumo wa kingamwili wa mtoto wako ili kupambana na saratani)