Arteraitisi ya Seli Kubwa

(Arteraitisi ya Muda; Arteraitisi ya Cranial; Ugonjwa wa Horton)

Imepitiwa/Imerekebishwa Sept 2023

Ateri ni mishipa ya damu ambayo hubeba damu kutoka kwenye moyo wako hadi sehemu zote za mwili wako. Arteraitisi ni kuvimba kwa ateri zako. Kuvimba kwa mishipa ya damu kwa ujumla huitwa vaskulitisi.

Arteraitisi Ya Seli Kubwa ni nini?

Arteraitisi ya seli kubwa ni aina ya uvimbe wa mishipa ya damu ambayo huathiri baadhi ya mishipa yako mikubwa. Wakati mwingine huitwa arteraitisi ya muda kwa sababu mara nyingi huathiri ateri kwenye upande wa kichwa nyuma ya macho yako (upande wa kichwa chako).

  • Arteraitisi ya seli kubwa kawaida huhusisha mishipa mikubwa inayotoka moyoni hadi shingoni na kichwani

  • Madaktari hawajui kinachosababisha arteraitisi ya seli kubwa

  • Kawaida huathiri watu wenye umri zaidi ya miaka 55

  • Unaweza kuwa na maumivu makali ya kichwa, maumivu ya ngozi ya kichwa wakati unapochana nywele zako, na maumivu kwenye taya yako unapotafuna chakula.

  • Arteraitisi ya seli kubwa inaweza kusababisha upofu au kiharusi ikiwa hautapata matibabu mara moja

  • Madaktari hufanya kipimo cha damu na kuondoa kipande cha tishu kwa uchunguzi (kuchukua sampuli ya tishu) kutoka kwa moja ya mishipa yako

  • Madaktari watakuelekeza kutumia dozi kubwa ya kotikosteroidi kama vile prednisone

Nini husababisha arteraitisi ya seli kubwa?

Madaktari hawajui kinachosababisha arteraitisi ya seli kubwa.

Je, dalili za arteraitisi ya seli kubwa ni zipi?

Dalili za arteraitisi ya seli kubwa zinaweza kuanza ghafla au kutokea polepole kwa wiki kadhaa.

Unaweza kuwa na dalili za jumla kama vile homa, jasho, na kuhisi uchovu na mgonjwa. Takriban nusu ya watu wana misuli ngumu, yenye maumivu kwenye shingo, mabega, na viuno. Maumivu na ugumu huwa mbaya zaidi asubuhi, sawa na kile kinachotokea katika polimyaljia reumatika.

Dalili maalum hutegemea ni mishipa gani iliyoathiriwa na inaweza kujumuisha:

  • Maumivu makali ya kichwa kwenye upande wa kichwa nyuma ya macho yako au nyuma ya kichwa chako

  • Uoni hafifu, maono mara mbili, upofu wa ghafla katika jicho moja

  • Maumivu ya taya wakati wa kutafuna

  • Kiharusi

Mara chache, ateritisi ya seli kubwa huathiri mkole wako, ateri kuu inayotoka kwenye moyo wako. Unaweza kupata maumivu ya kifua yanayosababishwa na uvimbe kwenye mkole au mpasuko wa mkole.

Je, madaktari wanawezaje kubaini kuwa nina arteraitisi ya seli kubwa?

Ikiwa dalili zako zinaonekana kama arteraitisi ya seli kubwa, madaktari watafanya:

  • Vipimo vya damu

  • Uondoaji wa kipande cha tishu kwa uchunguzi ya moja ya mishipa yako ya upande wa kichwa nyuma ya macho yako (chukua kipande cha ateri kwenye upande wa kichwa nyuma ya macho yako ili uangalie chini ya darubini)

Je, madaktari hutibu aje arteraitisi ya seli kubwa?

Ili kutibu arteraitisi ya seli kubwa, madaktari watakuelekezeka ukunywe:

  • Dozi kubwa ya kotikosteroidi kama vile prednisone

Watajaribu kukupa dawa haraka iwezekanavyo ili kuzuia upofu.

Madaktari hujaribu kupunguza dozi ya prednisone baada ya kama mwezi mmoja. Lakini unaweza kuhitaji kuendelea kuchukua kipimo cha chini kwa muda mrefu, wakati mwingine hadi miaka 2. Wanaotumia kotikosteroidi kwa muda mrefu huenda wakapata:

Madaktari wanaweza kuagiza kalsiamu na vitamini D ili kuzuia upotezaji wa mfupa. Pia hukupa kiwango cha chini cha aspirin kila siku ili kusaidia kuzuia kiharusi.