Vasculitics ni nini?
Vasculitics ni kuvimba kwa mishipa ya damu.
Vasculitics inaweza kuathiri ukubwa wowote au aina ya mshipa wa damu
Inaweza kuathiri mishipa mingi ya damu katika viungo vingi au mishipa machache tu katika viungo 1 au 2
Mishipa ya damu iliyovimba huwa nyembamba au kuziba na haitoi damu ya kutosha
Vasculitis inaweza kusababishwa na maambukizi fulani, dawa, au dawa haramu
Unaweza kuwa na homa na kujisikia uchovu, kisha kupata dalili nyingine kulingana na viungo gani vimeathirika
Madaktari huondoa kipande cha tishu kwa uchunguzi (kuchukua sampuli ya tishu kutoka kwa ogani iliyoathirika) kuangalia mishipa yake ya damu
Madaktari hukushauri ukunywe kotikosteroidi au dawa zingine kupunguza uvimbe
Nini husababisha uvimbe wa mishipa ya damu?
Kwa kawaida, madaktari hawawezi kupata sababu ya uvimbe wa mishipa ya damu.
Wakati mwingine, maambukizi, sumu, dawa, au dawa haramu huchochea tatizo hilo.
Mishipa ya damu iliyovimba mara nyingi hupungua au kuziba. Mishipa hii haiwezi kupeleka damu ya kutosha kwa kiungo iliyomo. Bila damu ya kutosha, viungo hivyo havifanyi kazi vizuri.
Je, dalili za uvimbe wa mishipa ya damu ni zipi?
Kuvimba kwa mishipa ya damu kunaweza kusababisha dalili za jumla kama vile homa, kutokwa na jasho usiku, maumivu ya misuli na viungo, kupungua uzani na kuhisi uchovu.
Dalili zingine mahususi hutegemea mishipa ya damu iliyoathirika, kama vile:
Kwenye ngozi yako: Upele au vidonda (vidonda) kwenye miguu yako
Katika ubongo wako: Maumivu ya kichwa na kuchanganyikiwa
Kwenye mafigo yako: Figo kushindwa kufanya kazi
Katika mapafu yako: Kupumua kwa shida
Kwenye neva zako Kufa ganzi, kuwashwa na udhaifu katika mikono au miguu
Kwenye macho yako Uoni hafifu au upofu
Huenda ukahitaji matibabu ya haraka kwa dalili hizi.
Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina uvimbe wa mishipa ya damu?
Uvimbe wa mishipa ya damu haitokei mara kwa mara. Madaktari mara nyingi hawashuku wakati dalili zinaanza. Wakati mchanganyiko fulani wa dalili hudumu kwa muda wa kutosha, madaktari wanaweza kushuku uvimbe wa mishipa ya damu. Ili kudhibitisha kuwa una uvimbe wa mishipa ya damu, madaktari hufanya:
Vipimo vya damu
Wakati mwingine uondoaji wa kipande cha tishu kwa uchunguzi (kupima sampuli ya tishu kutoka kwa kiungo kilichoathirika)
Huenda ukahitaji vipimo vingine ili kuangalia ni viungo gani vimeathiriwa. Kwa mfano, huenda ukapimwa mkojo ili kuona ikiwa mafigo zako zimeathirika. Unaweza fanyiwa EKG/ECG (elektrokadiografia) ili kuona kama moyo wako umeathirika. Ikiwa mapafu yako yanaonekana kuathirika, madaktari wanaweza kufanya eksirei ya kifua na uchanganuzi wa CT (tomografia ya kompyuta).
Je, madaktari hutibu uvimbe wa mishipa ya damu?
Madaktari hutibu kisababishaji cha uvimbe wa mishipa ya damu. Wakati mwingine hiyo inamaanisha unahitaji kusitisha kukunywa dawa ambazo wanashuku kuwa zinasababisha uvimbe wa mishipa ya damu.
Bila kujali kilicho sababisha, madaktari wanajaribu kusitisha uchochezi wa mishipa ya damu kwa kutumia:
Kotikosteroidi
Dawa ya kutuliza mfumo wa kingamwili wako (dawa za kukandamiza kingamwili)