Kwa nini kuvuta sigara ni vibaya kwa afya yangu?
Watu waanavuta tumbaku kwenye sigara, biri na kiko. Uvutaji wa sigara una kemikali nyingi hatarishi zinazosababisha matatizo kwenye mwili wako wote, si mapafu yako tu.
Uvutaji sigara unaleta uraibu kwa sababu tumbaku ina dawa ndani yake inayoitwa nikotini
Uvutaji sigara unasababisha saratani
Uvutaji sigara unaongeza uweekano wa kwamba utapata shambulio la moyo au kupata ugonjwa wa mapafu (kama vile ugonjwa sugu wa kuziba mapafu [COPD] au saratani ya mapafu)
Ni vigumu kuacha kuvuta sigara, lakini kutumia dawa na kujifunza jinsi ya kubadilisha mazoea yako kunaweza kusaidia
Kuvuta moshi kutoka kwa mtu mwingine anayevuta sigara, kunaitwa uvutaji sigara mtumba, kunaweza kusababisha matatizo yaleyale sawa na kuvuta sigara mwenyewe.
Kuvuta sigara wakati wa ujauzito kunaweza kumdhuru mtoto ambaye hajazaliwa na kusababisha:
Mtoto kuzaliwa mapema zaidi
Uzani wa chini wakati wa kuzaliwa
Matatizo kwenye mapafu ya mtoto, ikiwa ni pamoja na asthma
Vipi kuhusu sigara za kielektroniki?
Sigara za kielektroniki na sigara za mvuke zina kiowevu cha nikotini na kemikali za ladha, si tumbaku. Sigara ya kielektroniki au mvuke hupasha moto kiowevu na kuwa mvuke ambao unauvuta.
Unaweza kuwa mraidbu wa sigara za kielektrobiki au mvuke ikiwa zina nikotini kwa sababu nikotini inafanya uwe mraibu
Kwa sababu hakuna kinachoungua kwenye sigara ya kielektroniki au mvuke, hupati matatizo yaleyale yanayosababishwa kwa kuvuta sigara
Dutu fulani kwenye mvuke, kama vile THC au vitamini E asetati, inaonekana kusababisha majaraha mabaya ya mapafu na wakati mwinginekifo
Sigara za kielektroniki na mvuke hazijakuwepo kwa muda mrefu madaktari kujua athari za muda mrefu
Niki kitatokea ikiwa mtoto atameza nikotini?
Mtoto ambaye amekula sigara au kitu chochote chenye nikotini (kama vile bigijii ya nikotini) anahitaji matibabu ya dharura. Madaktari watamtibu mtoto kuondoa sumu ya nikotini.
Athari za kuvuta sigara ni zipi?
Athari za haraka
Mara nyingi huwezi kuhisi kitu chochote kwa kuvuta sigara, lakini unaweza kuhisi:
Nguvu zaidi
Kumakinika vizuri zaidi
Kutohisi njaa sana
Ikiwa unajaribu kuvuta sigara na hujaizoea bado, unaweza kujihisi kichefuchefu tumboni mwako, ngozi kuwa nyekundu au yote mawili.
Athari za baada ya muda mrefu
Uvutaji wa sigara huua karibu kila ogani kwenye mwili wako. Matatizo makubwa yanayohusiana na kuvuta sigara ni:
Shambulio la moyo na maumivu ya kifua
COPD, ambao ni ugonjwa wa mapafu unaofanya iwe vigumu kupumua
Kuvuta sigara pia kunafanya uwe na uwezekano zaidi wa:
Saratani, pamoja na saratani ya mapafu
Maambukizi kwenye mapafu na asthma
Ugonjwa wa kudhoofu kwa mifupa (ugonjwa unaofanya mifupa yako iwe dahifu na ivunjike kwa urahisi)
Vidonda kwenye tumbo lako
Mtoto wa jicho (wakati lenzi ya jicho lako inapata ukungu taratibu, na kufanya uoni wako uwe na hali mbaya kadiri muda unavyokwenda)
Uvutaji sigara pia husababisha:
Ngozi kavu na yenye mikunjo
Nywele kuwa nyembamba
Meno ya njano
Kupungua uzani
Dalili za kujiondoa
Ikiwa utaacha kuvuta sigara, huenda ukapitia hali ya kujiondoa. Kujiondoa ni wakati ambapo unahisi kuumwa baada ya kuacha kutumia dawa ya kulevya ambayo ulitumia kwa muda mrefu. Hali ya kujiondoa katika uvutaji wa sigara inaweza kusababisha:
Utake kuvuta sigara
Kujihisi mwenye hasira, wasiwasi, usingizi au huzuni
Kuumwa kichwa na kupata shida kumakinika
Kutetemeka(tikisiko)
Kuwa na maumivu ya tumbo na kuongezeka uzito
Je, ninapaswa kuzungumza na daktari wangu kuhusu uvutaji wangu wa sigara?
Ndiyo, unapaswa kuzungumza na daktari wako kuhusu kuvuta sigara na kiwango unachovuta.
Daktari wako anaweza:
Kuelezea kwa nini kuvuta sigara kunaweza kuudhuru mwili wako
Atakusaidia uache kuvuta sigara