Je, ugonjwa wa akili ni nini?
Ugonjwa wa akili unajumuisha aina mbalimbali za matatizo ya fikira, hisia, na/au tabia.
Kila mtu wakati mwingine huwa na mawazo yanayosumbua au yasiyo ya kawaida au hisia kali. Na watu wengi huonyesha tabia ambazo wakati mwigine watu wengine huwa wanadhani ni za ajabu. Hata hivyo, kwa watu wenye ugonjwa wa akili, mawazo, hisia na tabia hizi hutokea mara kwa mara au ni kali kiasi kwamba watu hupata matatizo makubwa katika maisha yao ya kila siku au kufadhaishwa sana.
Kuna aina nyingi za magonjwa ya akili
Ugonjwa wa akili unaweza kuwa wa muda mfupi au mrefu
Wakati mwingine inaweza kuwa vigumu kutofautisha ugonjwa wa akili na wasiwasi wa kawaida au huzuni, lakini ugonjwa wa akili ni mbaya zaidi, hudumu kwa muda mrefu, na huathiri kwa kiasi kikubwa uwezo wa mtu wa kukabiliana na maisha
Karibu nusu ya watu wazima hupata dalili za ugonjwa wa akili wakati fulani—mfadhaiko ndio huwapata zaidi
Matibabu ya msingi ni dawa na ushauri nasaha (tiba ya kuzungumza)
Familia, marafiki, na vikundi vya usaidizi vinaweza kusaidia watu kukailiana na ugonjwa wa akili
Je, zipi ni aina za magonjwa ya akili?
Ugonjwa wa akili ni matatizo mengi tofauti. magonjwa haya yamegawanywa katika makundi makubwa ikiwa ni pamoja na:
Magonjwa ya hali kama vile kuwa na huzuni sana (mfadhaiko) au kuwa na shauku sana (wazimu)
Magonjwa mengine ya afya ya akili yanajumuisha matatizo ya kula, magonjwa ya mfadhaiko kama vile ugonjwa wa msongo wa mawazo wa baada ya mshtuko (PTSD), na tabia ya kutaka kujiua.
Je, nini husababisha ugonjwa wa akili?
Ugonjwa wa akili bila shaka unasababishwa na mchanganyiko wa mambo mengi, ikiwa ni pamoja na:
Sababu za kurithi—ugonjwa wa akili ambao uko katika familia
Misongo ya kimaisha
Mazingira na utamaduni unaoishi
Matatizo ya afya yanayoathiri ubongo wako
Mawazo mengi, kama vile kupoteza kazi, talaka, au kutumia dawa nyingi, huongeza hatari ya kupata ugonjwa wa akili.
Matatizo fulani ya kiafya yanayoathiri ubongo wa mtoto, kama vile matatizo wakati wa kuzaliwa au ubongo kupata maambukizi ya virusi (kuvimba kwa ubongo), huongeza hatari ya ugonjwa wa akili hapo baadaye maishani.
Ugonjwa wa akili hautokei kwa sababu mtu ni mvivu au mwenye kutokuwajibika. Sio kitu ambacho watu hufanya kwa kukusudia.
Je, dalili za ugonjwa wa akili ni zipi?
Dalili ni tofauti kulingana na aina ya tatizo ulilo nalo. Dalili zinaweza kujumuisha:
Mabadiliko makubwa ya sifa au tabia, haswa ikiwa yanatokea bila sababu dhahiri
Kuchanganyikiwa na kutowaza vyema
Mawazo ya ajabu, yasiyo na mpangilia (kama vile kuhama hama mada au kujibu maswali rahisi kwa majibu marefu, yenye kuchanganya)
Tabia isiyofaa (kama vile kuvua nguo hadharani)
Kuona au kuskia vitu ambavyo havipo (ndoto)
Kuamini mambo ambayo si ya kweli (kudanganywa) licha ya uwepo wa uthibitisho wenye nguvu unaoonyesha kunyume chake
Usununu mwingi
Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa mtu ana ugonjwa wa akili?
Madaktari hugundua ugonjwa wa akili kwa kuzungumza na mtu. Wakati mwingine pia huzungumza na walezi au wanafamilia.
Wakati mwingine dalili zinadhihirisha kuwa mtu ana ugonjwa wa akili. Kwa mfano, mtu kushikilia kuwa yeye ndiye rais au kwamba mawazo yake yanadhibitiwa na redio iliyopandikizwa kwenye ubongo wao.
Wakati mwingine ni vigumu kutofautisha ugonjwa wa akili na hali za kawaida. Kwa mfano, inaweza kuwa vigumu kutofautisha kati ya huzuni na mfadhaiko baada ya kifo cha mchumba au mtoto, kwa sababu yote yanahusisha hali ya huzuni na kufadhaika. Vivyo hivyo, kuna tofauti ndogo kati ya kuwa nadhifu au mwenye mpangilio mzuri na ugonjwa wa kushindwa kudhibiti mawazo na misukumo. Utofauti wake kwa kawaida hutegemea yafuatayo:
Dalili ni kali kiasi gani
Muda ambao dalili zinadumu
Kiasi cha dalili kinachoathiri uwezo wa kufanya kazi.
Je, madaktari huwashughulikia vipi wenye ugonjwa wa akili?
Madaktari wamepiga hatua kubwa katika kutibu magonjwa ya akili kwa mafanikio.
Matibabu makuu ni pamoja na:
Tiba ya kuzungumza (ushauri nasaha)
Kwa matatizo mengi ya afya ya akili, kutumia dawa pamoja na tiba ya mazungumzo ni bora zaidi kuliko kutumia moja pekee.
Matibabu mengine ni pamoja na tiba ya mshtuko wa umeme na uchangamshaji wa sumaku kupitia fuvu la kichwa.
Zamani, wenye ugonjwa wa akili mara nyingi waliwekwa katika taasisi au hospitali. Leo, watu wana uwezekano mkubwa wa kuishi kwa tija katika jamii. Lakini watu wengi wenye ugonjwa wa akili bado hawapati huduma na usaidizi wanaohitaji.