Kandidiasi

(Kandidosisi; Moniliasisi; Maambukizi ya chachu)

Imepitiwa/Imerekebishwa Feb 2024

kandidiasisi ni nini?

Kandidiasi ni maambukizi yanayosababishwa na chachu ya Kandida, ambayo ni aina ya kuvu.

Kandidiasi inaweza kutokea:

  • Kwenye tabaka la juu la mwili wako, mara nyingi huwa ni ya kawaida

  • Kusambaa sehemu kubwa ndani ya mwili wako (huitwa kandidiasi inayosambaa), ambayo ni yenye kutishia maisha

Kandidiasi kwenye tabaka la juu la mwili wako inaweza kumuathiri mtu yeyote. Kwa kawaida hutokea kwenye sehemu zenye hali ya joto na unyevunyevu kama vile:

  • Mdomo

  • Kwapa

  • Eneo la msamba

  • Ngozi iliyo katikati ya vidole vya miguu yako au chini ya matiti yako

Kwa kawaida kandidiasi inayosambaa hutokea kwa watu ambao wana mfumo dhaifu wa kingamwili au waliolazwa hospitalini kwa sababu ya ugonjwa mbaya. Inaweza kupita kwenye mtiririko wako wa damu na kuathiri ogani zako nyingi, ikijumuisha:

  • Vali zako za moyo

  • Ubongo

  • Macho

  • Figo

  • bandama

Kwa aina zote za kandidiasi, madaktari watakupatia dawa ya kuvu.

Je, nini husababisha kandidiasi?

Kwa kawaida kandida hupatakina kwenye ngozi yako, kwenye utumbo wako, na kama wewe ni mwanamke, kwenye sehemu zako za siri. Kwa kawaida, haisababishi matatizo.

Maambukizi ya kandida kwenye tabaka la juu la mwili wako yana uwezekano mkubwa wa kutokea ikiwa:

  • Una kisukari, saratani au UKIMWI

  • Una mimba

  • Unatumia dawa za kuua bakteria

Kandidiasi inayosambaa sehemu kubwa kimsingi hutokea ikiwa:

  • Umelazwa hospitali kwa tatizo kubwa kama vile upasuaji mkubwa au matatizo ya UKIMWI

  • Una mabomba mwilini mwako (kwa mfano, ya kukulisha chakula)

  • Unaingiza dawa fulani za kuua bakteria kupitia mishipa

Je, dalili za kandidiasi ni zipi?

Dalili zinategemea aina ya kandidiasi uliyonayo.

Kandidiasi ya mdomo
Ugonjwa wa kuvimba ndani kwa ndani mwilini (Chini ya meno na kwenye ulimi)
Ugonjwa wa kuvimba ndani kwa ndani mwilini (Chini ya meno na kwenye ulimi)

Katika kandidiasi ya kinywa, viraka vyeupe, vichungu hutokea kinywani-kwa mfano, chini ya meno (picha ya juu) au kwa ulimi (picha ya chini).

... soma zaidi

Picha kwa hisani ya Jonathan Ship, MD.

Ugonjwa wa kuvimba ndani kwa ndani mwilini (Midomo)
Ugonjwa wa kuvimba ndani kwa ndani mwilini (Midomo)

Katika kandidiasi ya kinywa, viraka vyeupe, vichungu vinaweza kuunda ndani ya midomo.

© Springer Science+Business Media

Ugonjwa wa kuvimba ndani kwa ndani mwilini (Ulimi)
Ugonjwa wa kuvimba ndani kwa ndani mwilini (Ulimi)

Katika kandidiasi ya kinywa, viraka vyeupe, vichungu vinaweza kuunda kwa ulimi.

© Springer Science+Business Media

Kandidiasi ya Umio
Kandidiasi ya Umio

Picha hii inaonyesha mabaka meupe yanayosababishwa na Kandida.

Picha imetolewa na Kristle Lynch, MD.

Kwa kandidiasi ya ngozi unaweza kuwa na upele mwekundu wenye kuwasha ambao unaweza kufanana magamba. Wakati mwingine aina ya ukurutu utokanao na nepi husababishwa na kandida.

Kwa kandidiasi ya mdomo wako, dalili ni pamoja na:

  • Madoa yenye rangi yeupe ya malai mdomoni mwako

  • Kupasuka kwenye pembe za mdomo

Kwa kandidiasi ya uke, dalili ni pamoja na:

  • Kutokwa na uchafu mweupe au wa manjano wenye kufanana na jibini kwenye uke

  • Madoa meupe ndani au nje ya uke

  • Mwako na kuwashwa kwenye sehemu za ndani au nje ya uke

Kwa kandidiasi inayoasambaa kwa hatua, dalili zako hutegemea na sehemu ya mwili wako ambayo imeathiriwa. Inaweza kuwa vigumu kwa madaktari kujua ni dalili gani zinasababishwa na kandidiasi na zipi zinasababishwa na matatizo mengine ya kiafya unayoweza kuwa nayo.

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina kandidiasi?

Kwa kawaida madaktari hutambua kandidiasi kwenye eneo la nje la mwili wako kwa kuiangalia. Wanaweza kukwangua sampuli ya ngozi ili kuichunguza kwenye hadubini.

Kwa kandidiasi inayosambaa ndani, kwa kawaida madaktari hupima sampuli ya damu yako au tishu kuangalia kama kuna kuvu.

Je, madaktari hutibu vipi kandidiasi?

Madaktari hutibu kandidiasi kwa kutumia dawa ya kuvu. Kwa kutegemea aina ya maambukizi uliyonayo, unaweza kuzitumia kama malai, kidonge, au kupitia mshipa wa damu.