Ugonjwa wa Mrundikano wa Mafuta kwenye Ateri ya Ukingoni

Imepitiwa/Imerekebishwa Apr 2023

Ugonjwa wa ateri za pembeni ni nini?

Ateri ni mishipa ya damu ambayo hubeba damu kutoka kwenye moyo wako hadi kwenye viungo na tishu zako. Ateri za pembeni ni ateri kwenye mikono au miguu yako. Ugonjwa wa ateri za pembeni ni wakati ateri, kwa kawaida kwenye mguu, kuzuiwa kwa sehemu au yote. Uzibaji huu unaweza kufanyika polepole kwa miaka mingi au kwa ghafla. Ikiwa damu haiwezi kufikia sehemu za mwili wako, tishu hufa kutokana na ukosefu wa oksijeni.

  • Ugonjwa wa ateri za pembeni kwa kawaida unasababishwa na ateri kuwa ngumu (atherosklerosisi)

  • Ina uwezekano mkubwa zaidi kwa wavutaji sigara na watu walio na shinikizo la juu la damu, kisukari na lehemu ya juu

  • Dalili zinajumuisha maumivu au mikakamao kwenye mguu mmoja ambayo hutokea unapotembea na huisha unapopumzika

  • Kwa ugonjwa wa ateri ya pembeni mkali, mguu wako unaweza kuuma wakati wote na unaweza kupata majeraha ya ngozi

  • Ikiwa ateri ya mguu wako inazibika kabisa kwa ghafla, utapata gangrini (kufariki kwa tishu kunaosababishwa na ukosefu wa damu) na unahitaji kukatwa mguu isipokuwa kama kizuizi kinaondolewa mara moja

  • Madaktari wanakupea dawa au kufanya upasuaji ili kurekebisha kizuizi na kutuliza dalili

Nenda kwenye hospitali mara moja ikiwa mkono au mguu wako unakuwa na maumivu, wenye baridi na kusawajika kwa ghafla. Ateri yako inaweza kuwa imezibika.

Ni nini husababisha ugonjwa wa ateri za pembeni?

Ugonjwa wa ateri za pembeni unaweza kutokea wakati ateri:

  • Inakuwa nyembamba hatua kwa hatua wakati mafuta au lehemu inajiunda kwenye kuta za ateri (atherosklerosisi)

  • Inazuiwa kwa ghafla na damu iliyoganda

Ni nini huongeza hatari ya ugonjwa wa ateri ya pembeni?

Hali ya hatari ili kubwa zaidi ni:

Kwa sababu huwa inachukua muda mrefu ili ateri ziwe nyembemba, watu wengi hawapati ugonjwa wa ateri ya pembeni kabla ya umri wa miaka 55.

Hali zingine za hatari muhimu zinajumuisha:

Wanaume na watu ambao wana unene mkubwa wana hatari iliyoongezeka kidogo.

Dalili za ugonjwa wa ateri za pembeni ni zipi?

Ugonjwa wa ateri za pembeni ni wa nadra kwenye mikono. Mara nyingi utapata dalili kwenye miguu yako pekee.

Ikiwa ateri zako zinakuwa nyembamba baada ya wakati, utapata:

  • Kuhisi maumivu, uchungu, mkakamao au uchovu kwenye mguu wako ambao hufanyika unapotembea na huisha baada ya mapumziko mafupi (klaudikesheni ya mara kwa mara)

Baadaye, kwa wembamba mkubwa sana, unaweza:

  • Kutoweza kutembea umbali ambao ulikuwa unatembea

  • Kupata maumivu unapopumzika

  • Kuwa na vidonda kwenye kidole cha mguu au kisigino

  • Kuwa na vidonda kwenye ngozi ambavyo vinachukua muda mrefu kupona

Ikiwa dalili zako zinakuwa mbaya sana kwa ghafla, nenda kwa daktari mara moja.

Ikiwa ateri yako imezuiwa kabisa na kwa ghafla, mkono au mguu wako:

  • Chungu sana

  • Baridi

  • Utapata ganzi

  • Kusawijika

Nenda hospitali ni mara moja. Kizuizi kikubwa zaidi kinaweza kusababisha gangrini (kufariki kwa tishu kunaosababishwa na ukosefu wa damu). Damu ikizuiwa kwenda kwenye mkono au mguu wako kwa muda mrefu, mkono au mguu wko unaweza kuhitaji kukatwa (kukatwa kwa njia ya upasuaji).

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina ugonjwa wa ateri ya pembeni?

Madaktari watauliza kuhusu dalili zako na kufanya uchunguzi wa kimwili. Madaktari wanaweza pia kufanya vipimo, kama vile:

Je, madaktari wanatibu vipi ugonjwa ateri ya pembeni?

Ili kutibu ugonjwa wa ateri ya pembeni, madaktari hutumia:

  • Dawa ambazo husaidia kuongeza mtiririko wa damu

  • Upasuaji ili kutoa damu iliyoganda au kukwamua ateri iliyozuiwa

  • Upasuaji wa kufungua mshipa (utaratibu ili kufungua kizuizi kwa kutumia viputo na kuuweka ukiwa pana kwa kutumia bomba ya waya ndogo, inayoitwa stent)

Ikiwa mkono au mguu umekufa au hakuna njia nyingine ya kupeleka damu kwake, inaweza kuhitaji kukatwa (kukatwa kwa njia ya upasuaji).

Huenda daktari akakueleza:

  • Acha kuvuta sigara

  • Tembea angalau dakika 30 kwa siku, siku 3 kwa wiki

  • Shirikiana na daktari wa kimwili au wa shughuli za kila siku katika mpango wa kuwezesha kuishi maisha ya kawaida

  • Epuka baridi, ambayo hufanya mishipa yako ya damu iwe nyembamba zaidi

  • Epuka dawa fulani ambazo hufanya mishipa yako ya damu iwe myembamba, kama vile baadhi ya dawa za mafua na sanasi

  • Tunza vizuri miguu yako ili kuzuia vidonda na maambukizi

Ninawezaje kuzuia ugonjwa wa ateri za pembeni?

Ili kuzuia ugonjwa wa ateri za pembeni:

  • Usivute sigara

  • Dhibiti viwabgo vyako vya sukari kwenye damu (ikiwa una kisukari)

  • Viwango vya chini zaidi vya shinikizo la damu na lehemu

  • Punguza uzani

  • Kuwa amilifu na ufanye mazoezi