Perema ya Ateri kwenye Mikono, Miguu, Moyo na Ubonge

Imepitiwa/Imerekebishwa Apr 2023

Je, perema ni nini?

Perema ni uvimbe kwenye ateri Ikifanyika kutoka kwenye sehemu dhaifu kwenye ukuta wa ateri. Ateri ni mshipa wa damu ambao hubeba damu kutoka kwenye moyo wako hadi kwenye sehemu tofauti za mwili wako. Vena ni mishipa ya damu inayorudisha damu kwenye moyo wako. Mishipa huwa haipati perema.

  • Perema inaweza kutokea kwenye ateri yoyote

  • Unaweza kuzaliwa na perema, lakini mara nyingi hutokea wakati wewe ni mzee kwa sababu unakuwa na ateri ngumu (atherosklerosisi)

  • Perema wakati mwingine hupasuka kwa ghafla au kusababisha damu iliyoganda mbayo inazuia ateri

  • Madaktari hufanya upasuaji ili kufunga au kuondoa perema

  • Wakati mwingine madaktari huweka koili ndogo ya chuma kwenye perema ili kuifunga bila kufanya upasuaji

Unaweza pia kuwa na perema kwenye aota yako. Aota yako ni ateri kuu ambayo hubeba damu kutoka kwenye moyo wako.

Ni nini husababisha perema?

Perema inaweza kusababishwa na:

  • Udhaifu kwenye ukuta wa ateri ambao ulizaliwa nao

  • Kujiunda kwa nyenzo yenye mafupa ndani ya ateri zako (atherosklerosisi, pia inaitwa hali ya ateri kuwa ngumu)

  • Jeraha kwenye ateri kutokana na kisu au risasi

  • Maambukizi ya bakteria au kuvu kwenye ateri yako—hii inaweza kufanyika kutokana na kujidunga dawa haramu, kama vile heroini

Dalili za maambukizi ya perema ni zipi?

Baadhi ya perema hazisababishi dalili zozote. Dalili zinategemea ni wapi perema iko kwenye mwili wako na kwa ukubwa wake.

Perema kwenye mguu wako kwa kawaida haisababishi dalili isipokuwa kama damu iliyoganda huunda kwenye perema. Ikiwa una damu iliyoganda, inaweza kuuacha perema na kuzuia mtiririko wa damu kwenye mguu wako na kuifanya iwe ngumu zaidi, kufanya ganzi na kutulia.

Perema kwenye shingo yako inaweza kuunda damu iliyoganda ambayo inasafiri kwenye ubongo wako na kusababisha kiharusi.

Perema kwenye ubongo wako inaweza kusababisha maumivu ya kichwa. Perema ya ubongo ikipasuka itasababisha kuvuja damu kando na ubongo wako (inaitwa uvujaji damu wa subaraknoidi) ambao unasababisha maumivu makali ya kichwa na inaweza kuwa ya kufisha.

Wakati mwingine perema inaambukizwa. Perema iliyoambukizwa inasababisha maumivu na kuvimba.

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina perema?

Wakati mwingine madaktari wanaweza kuhisi mfuko wa uvimbe kwenye ateri yako kwa kukuchunguza. Huenda pia:

Madaktari hutibu perema vipi?

Perema katika sehemu tofauti zinatibiwa kwa njia tofauti.

  • Perema kwenye ubongo zinatibiwa kwa njia ya upasuaji ili kufunga perema kwa klipu ya metali au kwenye sehemu ya metali kwenye perema kupitia kwenye bomba ndogo (katheta) iliyopitishwa kupitia kwenye ateri kwenye shingo yako.

  • Perema kwenye mkono au mguu wako zinatibiwa kwa upasuaji ili kutoa perema na kuibadilishia na sehemu ya mshipa wa damu wa kutengenezwa (kupandikizwa). Wakati mwingine madaktari wanaweza kuweka kipandikizwa kupitia kwenye katheta inayopitishwa kupitia kwenye ateri yako.

Utapata dawa za kuua bakteria au dawa za kuvu kwa ajili ya perema iliyoambukizwa.