Kuvuja damu ndani ya subaraknoidi

Imepitiwa/Imerekebishwa Sept 2023

Ni nini maana ya kuvuja damu ndani ya subaraknoidi?

Kuvuja damu ndani ya subaraknoidi ni uvujaji wa damu ndani ya nafasi inayozingira ubongo. Ni dharura ya kimatibabu inayoweza kusababisha kifo au uharibifu wa kudumu kwenye ubongo.

  • Hali ya kuvuja damu ndani ya subaraknoidi hutokea mshipa wa damu unapopasuka kwenye ubongo wako

  • Utapata maumivu makali ya ghafla ya kichwa na huenda ukazirai

  • Madaktari wanaweza kufanya upasuaji ili kujaribu kusitisha uvujaji wa damu

Watu walio na dalili yoyote ya kuvuja damu ndani ya subaraknoidi wanapaswa kwenda kwenye kitengo cha dharura mara moja.

Bursts and Breaks: Causes of Hemorrhagic Stroke

When blood vessels of the brain are weak, abnormal, or under unusual pressure, a hemorrhagic stroke can occur. In hemorrhagic strokes, bleeding may occur within the brain, as an intracerebral hemorrhage. Or bleeding may occur between the inner and middle layer of tissue covering the brain (in the subarachnoid space), as a subarachnoid hemorrhage.

Je, ni nini husababisha kuvuja damu ndani ya subaraknoidi?

Tatizo la kuvuja damu ndani ya subaraknoidi linaweza kusababishwa na jeraha la kichwa (kwa mfano, kutokana na ajali ya barabarani).

Tatizo la kuvuja damu ndani ya subaraknoidi ambalo halijasababishwa na majeraha kwa kawaida huwa limesababishwa na kupasuka kwa ateri iliyofura ndani ya ubongo wako.

Kufura kwa mshipa wa damu ni uvimbe kwenye sehemu dhaifu ya ukuta wa mshipa wa damu. Kwa kawaida, huwa unazaliwa na uvimbe huu. Wakati mwingine kufura kwenye mishipa ya damu huanza baadaye kutokana na shinikizo la damu kuwa juu kwa miaka mingi. Huenda ukawa na zaidi ya uvimbe mmoja wa mshipa wa damu ndani ya ubongo wako.

Ni zipi dalili za kuvuja damu ndani ya subaraknoidi?

Mshipa wa damu uliofura unapopasuka, unasababisha:

  • Maumivu makali ya kichwa ya ghafla (wakati mwingine huitwa maumivu makali ya kichwa yanayoanza ghafla)

  • Kuzirai

  • Kuchanganyikiwa

Takribani nusu ya watu wanaopatwa na tatizo la kuvuja damu ndani ya subaraknoidi hufa kabla ya kufika hospitalini. Baadhi ya watu husalia katika hali ya usingizi mzito au kupoteza fahamu kwa muda mrefu. Watu wanaofanikiwa kuamka wanaweza kuchanganyikiwa na kuhisi usingizi na wapate dalili zifuatazo:

  • Shingo iliyokaza

  • Kutapika na kuhisi kizunguzungu

  • Vifafa

Unaweza kupona kabisa au kuachwa na uharibifu wa akili.

Baadaye, ikiwa una zaidi ya uvimbe mmoja wa mshipa, uvimbe uliosalia unaweza kupasuka pia, na kukupa tukio lingine la kuvuja damu.

Madaktari wangu watajuaje iwapo nimepata tatizo la kuvuja damu ndani ya subaraknoidi?

Madaktari kwa kawaida watashuku kuwa unavuja damu ndani ya subaraknoidi kulingana na dalili zako. Ili kuhakikisha kuwa hawajakosea, watafanya vipimo mara moja ili kubaini iwapo ubongo wako unavuja damu na mahali damu inavuja:

Je, madaktari hutibu vipi tatizo la kuvuja damu ndani ya subaraknoidi?

Madaktari watatibu matatizo yaliyosababisha kuvuja damu. Watakushauri ulazwe hospitalini au katika kituo cha kiharusi ambapo utapata:

  • Mapumziko ya kitandani bila kufanya chochote

  • Dawa za kupunguza maumivu yako ya kichwa (hutapewa aspirini au ibuprofeni kwa sababu dawa hizi zinaweza kuzidisha uvujaji wa damu)

  • Dawa na vinywaji vya kudumisha shinikizo la damu kiwango kinachostahili

  • Wakati mwingine dawa za kuzuia mkazo wa ghafla wa mishipa ya damu unaoweza kusababisha kiharusi kutokana na ubongo kutofikiwa na damu ipasavyo

  • Wakati mwingine, madaktari huweka koili ndogo ya chuma kwenye uvimbe wa mshipa unaovuja damu au kufanya upasuaji ili kufunga sehemu hiyo

  • Ikiwa una zaidi ya uvimbe mmoja wa mshipa wa damu, madaktari watatibu uvimbe mwingine wote, ili usivuje damu baadaye