Maambukizi Sugu ya Sikio (Hali Sugu ya Kuvimba Sehemu Ya Kati Ya Sikio)

Imepitiwa/Imerekebishwa Jun 2024

Sikio la kati ni nafasi tupu nyuma ya kiwambo cha sikio lako. Sikio la kati lina mifupa 3 midogo ambayo hutuma mitetemo ya kiwambo cha sikio lako hadi kwenye neva za sikio la ndani.

Ndani ya Sikio

Je, maambukizi sugu ya sikio ni nini?

Maambukizi sugu ya sikio ni maambukizi ya sikio la kati yanayodumu kwa zaidi ya miezi 3.

  • Kuwa na maambukizi makali ya sikio ambayo hayaishi kabisa yanaweza kugeuka kuwa maambukizi sugu ya sikio

  • Sikio lako haliumi lakini una majimaji mazito au usaha ukitoka kwenye sikio lako

  • Umepoteza uwezo wa kusikia, hali inayoweza kuwa ya kudumu

  • Madaktari watasafisha mfereji wa sikio lako na kukupa dawa za kuua bakteria za matone

Je, nini husababisha maambukizi sugu ya sikio?

Kwa kawaida maambukizi sugu ya sikio yanaanza na maambukizi makali ambayo:

Maambukizi sugu ya sikio yanaweza yakaibuka baada ya:

  • Kupata mafua

  • Maji yanaingia kwenye sikio lako la kati kupitia tundu la kiwambo cha sikio wakati unaoga kwenye maji mengi au kuogelea

Watoto walio na kasoro za kuzaliwa kwenye nyuso zao wana hatari zaidi ya kupata maambukizi ya sikio.

Je, dalili za maambukizi sugu ya sikio ni zipi?

Dalili za kawaida ni:

  • Majimaji mazito au usaha ukitoka kwenye sikio lako

  • Kupoteza uwezo wa kusikia

Je, matatizo ya maambukizi sugu ya sikio ni yapi?

Kitundu kwenye kiwambo cha sikio kinaweza kuingiza bakteria hatari wanaosababisha maambukizi mabaya. Maambukizi hayo yanaweza kuharibu mifupa midogo iliyo kwenye sikio lako la kati ua kuenea kwenye mifupa ya fuvu ya karibu.

Baadhi ya watu wenye maambukizi sugu ya sikio wanakuwa na kolestiatoma kwenye sikio la kati. Kolestiatoma ni uvimbe unaoonekana kama ngozi ambao hauna saratani. Kolestiatoma huongeza hatari ya wewe kupata matatizo makubwa, ikiwa ni pamoja na:

  • Kupoteza uwezo wa kusikia ambao haupati unafuu

  • Maambukizi kwenye sehemu zingine za sikio lako, mifupa ya fuvu lako au ubongo wako

  • Uharibifu kwenye neva inayodhibiti mwendo kwenye sura yako

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina maambukizi sugu ya sikio?

Madaktari watafanya kipimo cha kusikia na kutumia tochi ya kushika mkononi uangalia sikio lako:

  • Kuna usaha (majimaji mazito)

  • Kolestiatoma (ukuaji wa tishu inayofanana na ngozi kwenye sikio la kati)

Ikiwa madaktari watadhani kwamba una kolestiatoma wanaweza kufanya uchanganuzi wa CT (topografia ya kompyuta) au MRI (kupiga picha kwa sumaku).

Ni kwa jinsi gani madaktari wanatibu maambukizi sugu ya sikio?

Maambukizi sugu ya sikio yanapojitokeza, madaktari:

  • Watasafisha mfereji wa sikio lako na sikio la kati

  • Watakupatia dawa ya matone ya sikio ya kuua bakteria

  • Watakupa dawa za kuua bakteria za kutumia kwa kinywa, ikiwa inahitajika

Ikiwa una tundu kwenye kiwambo cha sikio lako, watakuambia uondoe maji kwenye sikio lako.

Madaktari wanaweza pia kupendekeza upasuaji ikiwa una: