Kubana kwa Aorta

Imepitiwa/Imerekebishwa May 2024

Je, kubana kwa mkole ni nini?

Mkole ni mshipa mkuu wa damu ambao hubeba damu kutoka kwenye moyo hadi sehemu nyingine za mwili. Kuwepo kwa kufunga kwa aota ni kasoro ya kuzaliwa ambapo sehemu ya aota ya mtoto ni nyembamba kuliko inavyopaswa kuwa.

  • Mkole ambao umepungua upana huzuia mtirirko wa damu kwenye nusu ya sehemu ya chini ya mwili, ikijumuisha figo, utumbo, ini, na miguu

  • Moyo hufanya kazi kwa bidii ili kusukuma damu ipite kwenye sehemu ya mkole iliyobana

  • Hii shughuli ya ziada inayofanywa na moyo husababisha shinikizo la damu kwenye mkole na matawi yake

  • Shinikizo la juu la damu huongeza hatari ya kupata kiharusi na linaweza kuchosha moyo, na kusababisha shinikizo la moyo

Mara nyingi, watoto wenye mkole uliobana pia huwa na kasoro nyingine za moyo.

Je, nini husababisha kubana kwa mkole?

Watoto wachanga wenye mkole uliobana huwa wamezaliwa nao. Madaktari hawana uhakika kwanini hili hutokea.

Je, dalili za kubana kwa mkole ni zipi?

Mtoto mwenye hali ya kubana mkole kiasi anaweza asiwe na dalili.

Iwapo mkole umebana kwa kiasi kikubwa, mtoto wako anaweza akawa:

  • Kupumua kwa haraka au kuishiwa pumzi

  • Mapigo ya moyo ya haraka

  • Matatizo ya kula

  • Ngozi ya kijivu

  • Nepi chache zilizokojolewa kuliko kawaida

  • Uchovu (usingizi usio wa kawaida na ukosefu wa tahadhari)

  • Shinikizo la moyo, kama mkole umebanwa sana

Iwapo mtoto atakua na bado akawa ana hali ya kubana kwa mkole, mtoto anaweza kuwa na dalili kama vile:

  • Maumivu ya kichwa

  • Maumivu ya kifua

  • Maumivu ya mguu wakati wa mazoezi

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa mtoto wangu ana tatizo la kubana kwa mkole?

Madaktari hushuku uwepo wa hali ya kubana pale wanaposikia aina fulani ya kuvuma kwa moyo (sauti zisizo za kawaida zinazosababishwa na mtiririko wa damu usio wa kawaida). Madaktari huthibitisha utambuzi wa ugonjwa kwa:

Daktari pia atafanya yafuatayo:

  • ECG/EKG (elektrokadiografia—kipimo kisicho na uchungu ambacho hupima mikondo ya umeme ya moyo na kuirekodi kwenye karatasi)

  • Eksirei za kifua

Je, madaktari hutibu vipi kubana kwa mkole?

Matibabu hutegemea kiwango cha kubana huko, na hasa kubana huko kupo sehemu gani ya mkole, na kunasababisha dalili gani. Huenda daktari:

  • Humpatia mtoto wako dawa za kutuliza mkazo kwenye moyo

  • Kufanya upasuaji ili kurekebisha sehemu ya mkole ambayo ni nyembamba

  • Wakati mwingine hufanya upasuaji wa kufungua mshipa

Upasuaji wa kufungua mshipa ni hatua ambapo madaktari huingiza bomba jembamba (katheta) kwenye mkole wa mtoto wako. Hupanua mkole kwa kujaza puto lililowekwa kwenye katheta. Wakati mwingine huingiza mpira wa waya wa wavu (stent) ili kushikilia sehemu iliyobana ibaki wazi.