Daktasi ya Ateriosasi Iliyowazi

Imepitiwa/Imerekebishwa May 2024

Mkole/aota husafirisha damu kutoka kwenye moyo hadi sehemu zingine za mwili. Ateri ya mapafu husafirisha damu kutoka kwenye moyo hadi kwenye mapafu.

Kabla ya kuzaliwa na siku chache baada ya kuzaliwa, ateri ya mapafu na mkole huunganishwa na mshipa wa damu mfupi unaoitwa daktasi ateriosasi.

  • Kwa sababu kijusi hakipumui, damu kiasi kidogo sana cha damu kinatakiwa kwenda kwenye mapafu

  • Kijusi kina daktasi ateriosasi ili damu isipite kwenye mapafu

Baada ya kuzaliwa, daktasi inapaswa kufunga kwa haraka ili damu itiririke kama kawaida, kwanza kupitia kwenye mapafu na kisha sehemu zingine za mwili.

Je, daktasi ateriosasi iliyowazi (PDA) ni nini?

Katika daktasi ateriosasi iliyowazi (PDA), daktasi ateriosasi huwa haifungi

  • Watoto waliozaliwa kabla ya wakati wana uwezekano mkubwa wa kuwa na PDA

  • Mara nyingi hakuna dalili, lakini daktari anayesikiliza kwa stethoskopu wanaweza kusikia kuvuma kwa moyo (sauti zisizo za kawaida kati ya mapigo ya moyo)

  • Madaktari hutibu PDA kwa dawa na wakati mwingine upasuaji

  • Watoto wenye PDA wana uwezekano mkubwa zaidi ya kawaida wa kupata maambukizi ya moyo

Patent Ductus Arteriosus: Failure to Close

The ductus arteriosus is a blood vessel that connects the pulmonary artery and the aorta. In the fetus, it enables blood to bypass the lungs. The fetus does not breathe air, and thus blood does not need to pass through the lungs to be oxygenated. After birth, blood does need to be oxygenated in the lungs, and normally the ductus arteriosus closes quickly, usually within days up to 2 weeks.

In patent ductus arteriosus, this connection does not close, allowing some oxygenated blood, intended for the body, to return to the lungs. As a result, the blood vessels in the lungs may be overloaded and the body may not receive enough oxygenated blood.

Je, nini husababisha PDA?

Madaktari hawana uhakika wa kwanini daktasi ateriosasi haifungi kama inavyotakiwa kwa baadhi ya watoto. PDA huwapata zaidi watoto waliozaliwa kabla ya wakati.

Je, dalili za PDA ni zipi?

Ikiwa PDA ni ndogo, mtoto anaweza asiwe na dalili zozote. Ikiwa PDA ni kubwa, mtoto anaweza kuwa:

  • Kupumua haraka

  • Kupumua kwa shida

  • Shinikizo la chini la damu

  • Tatizo la kula

  • Ukuaji wa polepole au mbaya

Je, watoto wanawezaje kujua ikiwa mtoto ana PDA?

Madaktari wanaweza kushuku uwepo wa PDA ikiwa watasikia aina fulani ya kuvuma kwa moyo. Madaktari huthibitisha utambuzi wa ugonjwa kwa:

Daktari pia atafanya yafuatayo:

  • ECG/EKG (elektrokadiografia—kipimo kisicho na uchungu ambacho hupima mikondo ya umeme ya moyo na kuirekodi kwenye karatasi)

  • Eksirei za kifua

Je, madaktari wanatibu vipi PDA?

Matibabu yanategemea:

  • Ukubwa wa PDA

  • Je, mtoto amezaliwa mapema kwa kiasi gani

  • Dalili mtoto alizonazo

Wakati mwignine PDA ndogo itajiziba yenyewe. Kwa kawaida hili hutokea kabla ya mtoto kufikisha umri wa mwaka 1. Ikiwa madaktari wanahitaji kutibu PDA ya mtoto wako, wanaweza:

  • Kumpatia mtoto wako dawa fulani ambazo zinaweza kusaidia kuziba daktasi

  • Kuweka bomba refu, jembamba (katheta) kwenye moyo wa mtoto na kutumia kifaa ili kuziba daktasi

  • Iwapo PDA ni kubwa kuliko kawaida, hufanya upasuaji ili kufunga daktasi