Kasoro ya Septamu ya Atiria na Ventrikali

Imepitiwa/Imerekebishwa May 2024

Nyenzo za Mada

Moyo una vyumba 4 (chemba), 2 upande wa kulia na 2 upande wa kushoto. Chemba za moyo wako hulegea ili kujaa damu na kisha kukaza ili kusukuma damu itoke.

  • Chemba 2 za juu (atriamu ya kulia na atriamu ya kushoto) huruhusu damu kuingia kwenye moyo

  • Chemba 2 za chini (ventrikali ya kulia na kushoto) husukuma damu nje

  • Chemba 2 za kulia husukuma kwenye mapafu damu inayorudi kutoka mwilini

  • Chemba 2 za kushoto husukuma kwenye mwili damu inayorudi kutoka kwenye mapafu

Damu huenda kwenye mapafu kupata oksijeni na kuondoa kaboni dioksidi.

Je, kasoro ya septamu ya atiria na ventrikali ni nini?

Septamu ni ukuta ambao upo kati ya chemba 2.

  • Kasoro ya septamu ya atiria na ventrikali ni matundu kwenye kuta ambazo hutenganisha pande za kulia na kushoto za moyo

  • Watoto wachanga ambao wana haya matundu huzaliwa nayo

  • Matundu huruhusu damu kiasi kupita njia isiyo sahihi katika moyo

  • Jinsi tundu linavyo kuwa kubwa, ndivyo kiasi kikubwa cha damu hupita njia isiyo sahihi

Kasoro ya septamu ya atiria (ASD) ni matundu kati ya chemba za juu za moyo (atiria).

Kasoro ya septamu ya ventrikali (VSD) ni matundu kati ya chemba za chini za moyo (ventricles).

  • ASD na VSD ni kati ya kasoro za moyo za kawaida za kuzaliwa nazo.

  • Wakati mwingine kasoro hizi hazisababishi dalili zozote, japokuwa tundu kubwa linaweza kusababisha matatizo makubwa

  • Madaktari hutambua ugonjwa wa ASD na VSD kwa kutumia ekokadiografia (upigaji picha wa moyo kwa kutumia mawimbi ya sauti)

  • ASD na VSD ndogo wakati mwingine huziba zenyewe—iwapo hili litatokea, kwa kawaida ni wakati mtoto akiwa na umri wa miaka 3

  • Ili kurekebisha kasoro hizi, madaktari wanaweza kufanya upasuaji

Wakati mwingine, watoto wenye ASD au VSD pia wanakuwa na kasoro zingine za moyo.

Kasoro ya Septamu: Tundu kwenye Ukuta wa Moyo

A septal defect is a hole in the wall (septum) that separates the heart into the left and right sides. Atrial septal defects are located between the heart's upper chambers (atria). Ventricular septal defects are located between the lower chambers (ventricles). In both types, some oxygenated blood, intended for the body, is shortcircuited. It is returned to the lungs rather than pumped to the rest of the body.

Je, nini husababisha ASD and VSD?

Watoto wachanga ambao wana ASD na VSD huwa wanazaliwa nazo. Madaktari hawana uhakika ni nini huzisababisha.

Je, zipi ni dalili za ASD na VSD?

Dalili hutegemea ukubwa wa tundu na eneo lilipo.

Kwa kawaida ASD haisababishi dalili, japokuwa wakati mwingine mtoto huwa anakua taratibu kuliko ilivyotarajiwa. Iwapo mtoto wako ana ASD kubwa ambayo haikutibiwa, mtoto anaweza kuwa na matatizo ya kiafya wakati wa utu uzima kama vile:

  • Kuchoka na kushindwa kupumua kwa urahisi

  • Kiharusi

  • Shinikizo la juu la damu kwenye mapafu (hipatensheni katika mishipa ya mapafu)

VSD ambayo ni ndogo inaweza isisababishe dalili yoyote. Lakini VSD kubwa huanza kusababisha matatizo pale mtoto anapofikisha umri wa wiki 4 hadi 6. Dalili zinajumuisha:

  • Kupumua kwa haraka

  • Matatizo ya kula

  • Kutoa jasho wakati wa kula

  • Kuongezeka uzani kwa taratibu

Hizi ni dalili za moyo kushindwa kufanya kazi.

Ikiwa VSD haikutibiwa, inaweza kusababisha:

  • Shinikizo la juu la damu kwenye mapafu (hipatensheni katika mishipa ya mapafu)

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa mtoto wangu ana ASD au VSD?

Madaktari hushuku ASD au VSD ikiwa watasikia aina fulani ya mivumo ya moyo/sauti ya moyo (sauti zisizo za kawaida zinazosababishwa na mtiririko wa damu kwenye moyo usiokuwa wa kawaida) Madaktari huthibitisha utambuzi wa ugonjwa kwa:

Pia watafanya vipimo kama vile:

  • ECG/EKG (elektrokadiografia—kipimo kisicho na uchungu ambacho hupima mikondo ya umeme ya moyo na kuirekodi kwenye karatasi)

  • Wakati mwingine, eksirei ya moyo

Je, mafaktari hutibu vipi ASD na VSD?

Mara nyingi ASD na VSD ndogo huziba zenyewe kabla ya mtoto kufikisha umri wa miaka 3. Matibabu hutegemea ukubwa wa tundu na dalili za mtoto wako.

Ikiwa ASD haikujiziba yenyewe wakati mtoto anapofikisha umri wa miaka 2 au 3, madaktari wanaweza:

  • Kuingiza katheta (bomba jembamba, linaloweza kupinda) kuptia vena ili kufikia moyo wa mtoto wako na kuziba tundu kwa kifaa kidogo

  • Wakati mwingine, kufanya upasuaji ili kuziba tundu kwenye moyo

VSD ndogo mara nyingi hahitaji matibabu. Ikiwa unahitaji matibabu, huenda daktari akafanya yafuatayo:

  • Kufanya upasuaji ili kuziba tundu

Kabla ya upasuaji, kwa kawaida madaktari humpatia mtoto wako dawa za moyo ili kumsaidia kupunguza dalili. Dawa zinaweza pia kutoa muda kwa ajli ya tundu kuziba lenyewe.