Esophageal Atresia na Fistula ya Tracheoesophageal

Imepitiwa/Imerekebishwa Feb 2024

Je, esophageal atresia na fistula ya tracheoesophageal ni nini?

Umio ni bomba ambalo hubeba chakula na majimaji kutoka mdomoni hadi tumboni. Esophageal atresia ni kasoro ya kuzaliwa nayo ambapo mtoto wako huzaliwa akiwa na umio jembamba au umio lililofungwa, hivyo chakula hakiwezi kufika tumboni.

Fistula ya tracheoesophageal ni uwazi ambao uko katikati ya umio na bomba la upepo (bomba la pumzi), hivyo mtoto anapomeza, chakula huingia kwenye bomba la upepo na mapafu ya mtoto.

Mara nyingi watoto huwa na matatizo yote.

  • Madaktari hawajui ni nini husababisha esophageal atresia na fistula ya tracheoesophageal, lakini mara nyingi matatizo haya huambatana na kasoro nyingine za kuzaliwa

  • Mtoto wako hukohoa au kukabwa anapojaribu kula

  • Madaktari hufanya upasuaji ili kurekebisha kasoro

Atresia na Fistula: Kasoro kwenye Umio

In esophageal atresia, the esophagus narrows or comes to a blind end. It does not connect with the stomach as it normally should. A tracheoesophageal fistula is an abnormal connection between the esophagus and the trachea (which leads to the lungs).

Je, dalili za esophageal atresia na fistula ya tracheoesophageal ni zipi?

Kwa atresia ya umio, dalili ni pamoja na:

  • Kukohoa, kukabwa na kutokwa mate wakati mtoto wako anakula

Fistula ya tracheoesophageal ni ya hatari kwa sababu chakula na mate yaliyomezwa husafiri kupitia tundu lililo kwenye bomba la upepo na mapafu ya mtoto wako na kusababisha:

  • Kukohoa, kukabwa, na shida ya kupumua

  • Wakati mwingine, aina fulani ya nimonia (nimonia ya mpumuo)

  • Rangi ya kivulivuli kwa ngozi ya mtoto kutokana na viwango vya chini vya oksijeni kwenye damu

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa mtoto wangu ana fistula ya tracheoesophageal?

Madaktari wanaweza kushuku uwepo wa matatizo kupitia kipimo cha kawaida cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti wakati wa ujauzito. Baada ya kuzaliwa watafanya vipimo kama vile:

  • Kupitisha bomba hadi chini ya umio la mtoto wako ili kujua kama limezibwa kuungana na tumbo

  • Eksirei ya shingo na kifua

Je, madaktari hutibu vipi sophageal atresia na fistula ya tracheoesophageal?

Madaktari hufanya upasuaji ili kurekebisha kasoro hizi: Kwa esophageal atresia, watatengeneza muunganisho baina ya umio na tumbo la mtoto wako. Kwa fistula ya tracheoesophageal, huziba muunganisho baina ya umio na bomba la upepo.