Kasoro ya Ukuta wa Tumbo

Imepitiwa/Imerekebishwa Feb 2024

Kasoro ya ukuta wa tumbo ni nini?

Kasoro ya ukuta wa tumbo ni uwazi katika ngozi na misuli ya tumbo. Utumbo hutokeza nje kupitia uwazi huu na kugusana na hewa.

  • Kasoro za ukuta wa tumbo ni kasoro za kuzaliwa nazo ambazo huonekana mara tu baada ya kuzaliwa

  • Utumbo wa mtoto wako huchomoza nje kupitia uwazi kwenye tumbo

  • Mara nyingi uwazi uko ndani au karibu na kitovu

  • Wakati mwingine utumbo hufunikwa kwa utando mwembamba

  • Ikiwa utumbo haukufunikwa kwa utando, unaweza kusumbuliwa na maji ya amnioti kabla ya kuzaliwa

  • Mtoto wako atatakiwa kufanyiwa upasuaji ili kurudisha utumbo tomboni na kuziba uwazi

Watoto wenye kasoro za kuta za tumbo mara nyingi wanakuwa na kasoro nyingine za kuzaliwa nazo au matatizo ya kijenetiki (kama vile ugonjwa wa Down).

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa mtoto wangu ana kasoro ya ukuta wa tumbo?

Kwa kawaida madaktari hugundua kasoro ya ukuta wa tumbo wakati wa kipimo cha kawaida cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti kinachofanywa wakati wa ujauzito wako. Ikiwa hawatagundua tatizo wakati wa ujauzito wako, wataliona mara tu baada ya mtoto kuzaliwa.

Je, madaktari hutibu vipi kasoro ya ukuta wa tumbo?

Madaktari watatibu kasoro ya ukuta wa tumbo ya mtoto wako mara tu baada ya mtoto wako kuzaliwa. Atafanya yafuatayo:

  • Hutumia bendeji kufunika na kukinga utumbo

  • Huweka majimaji na dawa za kuua bakteria kupitia mishipa

  • Hupitisha bomba la plastiki chini ya pua ili kutoa maji-tumbo

  • Hufanya upasuaji ili kurudisha utumbo tumboni na kuziba uwazi huo

Wakati mwingine madaktari lazima watumie siku chache wakinyoosha ngozi ya tumbo la mtoto kabla ya upasuaji ili ipatikane ngozi ya kutosha kufunika uwazi. Ikiwa sehemu kubwa ya utumbo imetokeza nje, wanaweza kuurudisha tumboni kidogo kidogo kwa siku kadhaa au wiki.