Ngiri ya Kiwambo

Imepitiwa/Imerekebishwa Feb 2024

Kiwambo ni misuli iliyo kati ya kifua na tumbo ambayo hukusaidia kupumua. Ngiri ni tundu au eneo dhaifu katika msuli.

Je, ngiri ya kiwambo ni nini?

Ngiri ya kiwambo ni tundu au eneo dhaifu kwenye kiwambo ambalo huruhusu viungo vya tumboni kuvimba ndani ya kifua.

  • Watoto wanaweza kuzaliwa wakiwa na ngiri ya kiwambo

  • Tumbo, utumbo, ini au bandama ya mtoto mchanga inaweza kuvimbia kifuani katika upande mmoja na kusukuma pafu

  • Ngiri ya kiwambo karibu mara zote hutokea upande wa kushoto

  • Inaweza kusababisha matatizo makubwa ya kupumua wakati wa kuzaliwa

Ikiwa viungo vya tumbo vinasukuma ndani ya kifua kabla ya kuzaliwa, mapafu ya upande huo hayawezi kukua kama inavyotakiwa. Ikiwa viungo vya tumbo vinasukuma ndani ya kifua baada ya kuzaliwa, mtoto wako atakuwa na wakati mgumu wa kupumua.

Je, nini husababisha ngiri ya kiwambo?

Madaktari hawana uhakika wa kwanini baadhi ya watoto hupata ngiri ya kiwambo, lakini mara nyingi huwapata watoto wenye kasoro nyingine za kuzaliwa nazo.

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa mtoto wangu ngiri ya kiwambo?

Madaktari wanaweza kugundua tatizo la ngiri ya kiwambo kabla ya mtoto wako kuzaliwa wakati wa kipimo cha kawaida cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti. Baada ya kuzaliwa, madaktari hupiga eksirei ya kifua.

Je, madaktari wanatibu vipi ngiri ya kiwambo?

Ili kutibu ngiri ya kiwambo, madaktari wafanya:

  • Kama itahitajika, watampatia mtoto wako oksijeni kwa kutumia mashine ya upumuaji (mashine ya kumsaidia kupumua)

  • Watafanya upasuaji ili kukarabati tundu au eneo dhaifu lililo kwenye kiwambo cha mtoto wako