Nyongo ni majimaji ya kumeng'enya chakula ambayo ni mazito, yenye rangi ya njano-kijani yanayotengenezwa kwenye ini lako. Husaidia mwili wako kuvunja na kunyonya mafuta katika mlo wako. Nyongo uhifadhiwa kwenye kibofu nyongo hadi inapohitajika kwenye utumbo. Nyongo husafiri kutoka kwenye ini na kibofu nyongo hadi kwenye utumbo kupitia mabomba yanayoitwa mifereji ya nyongo.
Je, biliary atresia ni nini?
Kwenye biliary atresia, mifereji ya nyongo ya mtoto wako huwa myembamba na huziba ndani ya kipindi kifupi.
Kwa sababu nyongo haiwezi kutiririka kama kawaida, hujikusanya kwenye ini na kusababisha uharibifu wa ini
Dalili ni pamoja na ngozi ya manjano, mkojo mweusi, kinyesi kilichopauka, na ini kubwa
Ili kutibu tatizo hili, madaktari hufanya upasuaji ili kutengeneza mifereji mipya ya nyongo
Madaktari hawajui sababu inayofanya biliary atresia kutokea, lakini mara nyingi huambatana na kasoro zingine za kuzaliwa nazo
Je, dalili za biliary atresia ni zipi?
Dalili huanza kiasi cha wiki 2 baada ya kuzaliwa. Dalili za biliary atresia ni pamoja na:
Mkojo wenye rangi nyeusi
Kinyesi chenye rangi iliyopauka
Ngozi ya mtoto hubadilika na kuwa ya rangi ya njanonjano (homa ya nyongo ya manjano)
Ini la mtoto huongezeka
Mara baada ya mtoto wako kufikisha umri wa miezi 2 au 3, dalili hujumuisha:
Kukua polepole
Mihangaiko
Mishipa mikubwa inayoonekana kwenye tumbo la mtoto
Bandama kubwa lisilo la kawaida (kiungo kidogo kinachosaidia kuchuja maambukizi na virusi kutoka kwa damu yako)
Madaktari wanawezaje kujua ikiwa mtoto wangu ana biliary atresia?
Ili kufahamu kama mtoto wako ana biliary atresia, madaktari watafanya uchunguzi wa ana kwa ana na:
Kipimo cha damu
Kipimo kwa kutumia kifuatiliaji nunurishi (madaktari hutafuta kikwazo kwa kuingiza kifuatiliaji ndani ya mkono wa mtoto wako na kukifuatilia wakati kikitiririka kupitia kwenye mfumo wa kibofu cha nyongo na kuingia kwenye utumbo)
Kipimo cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti kwa tumbo
Wakati mwingine, upasuaji
Madaktari wanatibu vipi biliary atresia?
Madaktari watatibu biliary atresia kwa kutumia:
Upasuaji wa kutengeneza njia ya kuondoa nyongo kutoka kwenye ini
Upandikizaji wa ini—watoto wengi wenye biliary atresia watahitaji upandikizaji haijalishi walifanyiwa upasuaji mwingine au la