Kasoro ya Kugeuka kwa Utumbo

Imepitiwa/Imerekebishwa Feb 2024

Kasoro ya kugeuka kwa utumbo ni nini?

Una utumbo mdogo na utumbo mpana. Utumbo mdogo ni tyubu ndefu iliyojikunja ambayo huunganisha tumbo yako na utumbo mpana. Utumbo mpana ni mfupi lakini mpana zaidi na unatoka mwishoni mwa utumbo mdogo hadi kwenye rektamu.

Kasoro ya kugeuka kwa utumbo ni kasoro ya kuzaliwa nayo ambapo utumbo haukui kama kawaida kabla ya kuzaliwa.

  • Kabla ya kuzaliwa, utumbo wa mtoto wako hukua katika upande mmoja na kisha hugeuka (huzunguka) katika eneo lake la kawaida

  • Wakati mwingine utumbo wa mtoto hushindwa kuzunguka kwenye eneo la kawaida, hali hii inaitwa mzunguko haribifu

  • Kasoro ya kugeuka kwa utumbo husababisha kuziba kwa utumbo na uhatarisha maisha

  • Watoto wanahitaji kufanyiwa upasuaji ili kurekebisha tatizo hili

Watoto wenye kasoro ya kugeuka kwa utumbo mara nyingi wana kasoro zingine za kuzaliwa.

Dalili za kasoro ya kugeuka kwa utumbo ni zipi?

Kasoro ya kugeuka kwa utumbo inaweza kusababisha utumbo wa mtoto kuziba. Dalili za kuziba zinaweza kuanza wakati wa mwezi wa kwanza wa maisha yake au sivyo kwa miaka kadhaa. Pia dalili zinaweza kutokea na kupotea na kwa kawaida hujumuisha:

  • Kutapika

  • Tumbo lililovimba, lenye kuuma

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa mtoto wangu ana kasoro ya kugeuka kwa utumbo?

Madaktari wanaweza kushuku juu ya mtoto wako kuwa na kasoro ya kugeuka kwa utumbo ikiwa mtoto wako anatapika nyongo ya kijanikijani. Ili kujua kwa hakika, watafanya eksirei ya bariamu ili kusaidia kuona nafasi ya njia ya mmeng'enyo wa chakula ya mtoto.

Je, madaktari hutibu vipi kasoro ya kugeuka kwa utumbo?

Kasoro ya kugeuka kwa utumbo ni dharura yenye umuhimu, hivyo madaktari watamtibu mtoto mara moja kwa: 

  • Majimaji yanayotolewa wa njia ya IV (kupitia mishipa)

  • Upasuaji ili kukarabati utumbo