Hitilafu katika uumbaji wa tundu la haja kubwa na rektamu ni nini?
Tundu la haja kubwa ni tundu lililo katikati ya matako ambapo haja kubwa (kinyesi) hutoka nje. Rektamu ni mwisho wa utumbo mpana ambayo imeungana na tundu la haja kubwa.
Hitilafu katika uumbaji wa tundu la haja kubwa na rektamu ni kasoro ya kuzaliwa ya tundu la haja kubwa na rektamu.
Hitilafu katika uumbaji wa tundu la haja kubwa na rektamu hutokea pale uwazi wa tundu la haja kubwa unapokuwa mwembamba, umefunikwa kwa ngozi au haupo kabisa.
Hitilafu katika uumbaji wa tundu la haja kubwa na rektamu huziba utumbo hivyo mtoto wako hawezi kujisaidia
Kwa kawaida, madaktari hufanya upasuaji ili kurekebisha tatizo la hitilafu katika uumbaji wa tundu la haja kubwa na rektamu
Watoto wachanga wenye tatizo la hitilafu katika uumbaji wa tundu la haja kubwa na rektamu mara nyingi wanakuwa na kasoro nyingine za kuzaliwa.
Je, dalili za hitilafu katika uumbaji wa tundu la haja kubwa na rektamu ni zipi?
Watoto wachanga wenye hitilafu katika uumbaji wa tundu la haja kubwa na rektamu huwa hawatoi kinyesi mara baada ya kuzaliwa. Tundu la haja kubwa la mtoto halionekani kuwa kawaida.
Ikiwa hitilafu katika uumbaji wa tundu la haja kubwa na rektamu haitatibiwa, utumbo wa mtoto wako unaweza kuziba na kusababisha:
Maumivu
Kuwashwa
Kutapika
Tumbo lililovimba
Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa mtoto wangu ana hitilafu katika uumbaji wa tundu la haja kubwa na rektamu?
Madaktari wanaweza kufahamu ikiwa mtoto wako ana hitilafu katika uumbaji wa tundu la haja kubwa na rektamu kwa kumchunguza mtoto wako mara tu baada ya kuzaliwa. Pia wanaweza kumpiga eksirei.
Je, madaktari wanatibu vipi hitilafu katika uumbaji wa tundu la haja kubwa na rektamu?
Ili kutibu hitilafu katika uumbaji wa tundu la haja kubwa na rektamu mara nyingi madaktari hufanya:
Upasuaji ili kuondoa au kufungua ngozi ambayo imeziba tundu la haja kubwa
Wakati mwingine, kwa matatizo makubwa, madaktari kwanza hutuboa tundu la muda mfupi kwenye tumbo (kolostomia). Madaktari hutoboa tundu kwenye utumbo mpana na kuliunganisha na tundu la tumbo. Kinyesi cha mtoto wako hupitia kwenye tundu na kuingia kwenye mfuko hadi pale mtoto wako atakapokua vya kutosha kuweza kufanyiwa upasuaji mwingine ili kurekebisha tatlizo la hitilafu katika uumbaji wa tundu la haja kubwa na rektamu na kuziba kolostomia.