Una aina kadhaa za seli za damu:
Seli nyekundu za damu hubeba oksijeni
Seli nyeupe za damu hupambana na maambukizi
Chembe sahani husaidia damu yako kuganda wakati unavuja damu
Seli za plasma ni aina maalum ya seli nyeupe za damu. Seli za plasma hutengeneza kingamwili. Kingamwili ni protini ambazo ni sehemu ya ulinzi wa asili wa mwili wako dhidi ya maambukizi na saratani. Kingamwili hupata na kushambulia seli za kigeni.
Uboho uko katikati ya mifupa yako. Seli nyingi katika damu yako zinatengenezwa kwenye uboho wako. Seli tofauti za damu zote hukua kutoka kwa kile kinachoitwa seli ya shina.
Myeloma ya wingi ni nini?
Myeloma ya wingi ni kansa ya seli za plazma. Moja ya seli zako za plasma huongezeka bila udhibiti katika uboho wako na kutengeneza nakala nyingi yenyewe.
Myeloma nyingi mara nyingi husababisha maumivu ya mfupa, kuvunjika, na figo kushindwa kufanya kazi
Umri wa wastani wa watu walio na myeloma ya wingi ni takribani miaka 65
Madaktari hufanya uchunguzi wa damu na mkojo na kuondoa sehemu ya uboho kwa ajli ya uchunguzi (kutoa sampuli ya uboho ili kuitazama kwa hadubini) kugundua myeloma ya wingi.
Madaktari kwa kawaida hutibu saratani kwa tibakemikali, kotikosteroidi, na wakati mwingine upandikizaji wa seli ya shina
Myeloma ya wingi inasababishaje matatizo?
Seli za plasma zenye saratani:
Zinavamia mfupa wenye afya ulio karibu
Hufurukia seli za kawaida kwenye uboho wako
Zinazalisha kwa wingi aina moja ya kingamwili
Uvamizi wa mifupa hufanya mifupa yako kuumiza na uwezekano wa kuvunjika.
Wakati seli zisizo za kawaida zinateka uboho wako, hautengenezi seli za kawaida za damu. Bila seli nyekundu za damu za kutosha, unapata anemia (kiwango cha chini cha damu). Bila seli nyeupe zenye afya za kutosha, uko katika hatari ya maambukizi. Bila chembe sahani za kutosha, unaweza kuvuja damu kupita kiasi.
Kingamwili za ziada zinazotengenezwa na seli za plasma zenye saratani si za kawaida na hazikusaidii kukukinga dhidi ya maambukizi. Hata hivyo, inaweza kuziba figo zako na kukusababisha figo kushindwa kufanya kazi.
Nini husababisha myeloma ya wingi?
Madaktari hawajui myeloma ya wingi, lakini wanafikiri inaweza:
Kuwa a kurithi katika familia
Wakati mwingine hutokea kutokana na kuwa karibu na mionzi mingi au kemikali fulani
Je, dalili za myeloma ya wingi ni zipi?
Dalili ya kawaida ni:
Maumivu katika mifupa yako, kwa kawaida nyonga, mgongo, mbavu, na fuvu la kichwa
Unaweza kuwa na dalili nyingine kutokana na matatizo:
Kuhisi uchovu na udhaifu kwa sababu ya anemia (kiwango cha chini cha damu)
Maambukizi ambayo husababisha homa na mzizimo
Michubuko na hali ya kutokwa na damu isiyo ya kawaida kwa sababu ya matatizo ya kuganda kwa damu yako
Madaktari wanawezaje kujua kama nina myeloma ya wingi?
Madaktari watafanya:
Vipimo vya damu ili kupima aina tofauti za seli za damu na kingamwili
Vipimo vya mkojo kupima kingamwili na protini nyingine zinazotengenezwa na myeloma
Eksirei ya mifupa yoyote inayouma
Ikiwa vipimo hivi vitaonyesha unaweza kuwa na myeloma ya wingi, madaktari watafanya:
Kuondoa sehemu ya uboho wa mfupa kwa ajli ya uchunguzi (kuondoa sampuli ya uboho ili kuitazama kwenye hadubini)
Eksirei ya mifupa yote katika mwili wako (uchunguzi wa mifupa) ili kuona ni ipi iliyoathiriwa na myeloma.
Madaktari hutibuje myeloma ya wingi?
Madaktari watakusaidia kupunguza kasi ya ukuaji wa saratani na kupunguza dalili zako. Hawawezi kuponya myeloma ya wingi, lakini unaweza kuishi kwa muda mrefu.
Huenda daktari akakupa:
Tibakemikali na dawa nyingine za kuzuia saratani kukua
Dawa za kuimarisha mifupa yako
Wakati mwingine tiba ya mionzi kutibu mifupa yenye maumivu
Wakati mwingine madaktari hufanya upandikizaji wa seli ya shina.
Wanachukua seli shina zenye afya kutoka kwako, au mara chache kwa mtu mwingine
Kisha wanakupa tibakemikali thabiti ili kutoa seli zako zisizo za kawaida za plasma
Kisha wanakurudishia seli shina zenye afya kupitia mshipa (IV)
Seli hizi za shina huenda kwenye uboho wako ambapo zinaweza kutoa seli za kawaida za damu
Madaktari wanafanya upandikizaji wa seli shina chache kwa sababu dawa mpya zaidi za myeloma ya wingi hufanya kazi vizuri.