Je, uvimbe wa matiti ni nini?
Uvimbe wa matiti ni kitu kilichofura, kiotea, au sehemu ngumu zinazohisi tofauti na sehemu zingine za titi lako. Unaweza kugundua uvimbe wa matiti kibahati au wakati wa tathmini ya matiti.
Uvimbe wa matiti ni hali inayotokea sana
Aina nyingi za uvimbe huwa si kansa
Uvimbe wa matiti unaweza kusababisha maumivu au kutosababisha maumivu
Uvimbe unaweza kuwa laini, mviringo na unaweza kusogezeka au uwe mgumu na mzito
Je, nini husababisha uvimbe wa matiti?
Saratani si kisababishi kikuu cha uvimbe wa matiti.
Visababishi vikuu vya uvimbe wa matiti ni:
Fibroadenomas, ambao ni uvimbe wa mviringo mdogo, laini, unaosogezeka, usio na maumivu ambao kawaida hutokea kwa wanawake ambao wako katika umri wa kuzaa watoto
Mabadiliko ya fibrosisti, ambayo ni ugumu na maumivu katika matiti yako yanayosababishwa na mabadiliko ya kila mwezi katika homoni za kike kama vile estrojeni na projesteroni
Visababishi visivyo vya kawaida sana vya uvimbe wa matiti ni:
Maambukizi ya matiti
Tezi ya maziwa iliyofungamana baada ya kuacha kunyonyesha
Ninapaswa kumwona daktari wakati gani kuhusiana na uvimbe wa matiti?
Nenda kwa daktari ndani ya siku 1 au 2 ikiwa una uvimbe wa matiti na:
Kuvimba, wekundu na maumivu
Usaha unaotoka
Nenda kwa daktari ndani ya siku 7 ikiwa una uvimbe wa matiti na:
Uvimbe huo hausogei (unahisi kana kwamba umekwama kwenye ngozi au kifua chako)
Uvimbe unasikika ukiwa mgumu sana na una sehemu zisizotoshana
Vinundu vya limfu vilivyovimba kwenye kwapa lako ambavyo haviwezi kusogea
Kubonyea kwa ngozi yako karibu na uvimbe kunakofanana na ngozi ya chungwa
Je, nitarajie nini ninapokwenda kumwona daktari wangu?
Daktari atakuuliza maswali kuhusu dalili na afya yako. Watafanya uchunguzi, ikijumuisha tathmini ya titi ili kuhisi jinsi uvimbe ulivyo.
Ili kujua iwapo uvimbe wako wa matiti ni kansa, madaktari mara nyingi hufanya vipimo zaidi, kama vile:
Kipimo cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti (uchunguzi kwa kutumia mawimbi ya sauti kutayarisha picha ya mwendo ya sehemu ya ndani ya titi lako)
Mamogramu (eksirei ya matiti yako)
Kulingana na dalili na matokeo ya vipimo hivi, daktari wako anaweza:
Kudunga sindano kwenye uvimbe na kutoa majimaji au sampuli ya tishu
Kukukata ngozi ili kuchukua sehemu ya uvimbe na kuichunguza kenye hadubini (uondoaji wa kipande cha tishu kwa uchunguzi)
Madaktari hutibu vipi uvimbe wa matiti?
Ikiwa uvimbe wako wa matiti ni mabadiliko ya fibrosisti, madaktari wanaweza:
Kutoa majimaji ya uvimbe kwa kutumia sindano
Akushauri uvalie sidiria laini, inayokutosha vyema, kama vile sidiria ya wanamichezo
Kukuelekeza umeze acetaminophen au ibuprofen ili kupunguza maumivu
Ikiwa uvimbe wako wa matiti ni fibroadenomas, madaktari wanaweza:
Kufanya upasuaji ili kuuondoa
Kuuacha lakini waratibu miadi ya ukaguzi wa kuangalia mabadiliko yoyote
Ikiwa uvimbe wako wa matiti ni saratani ya matiti, madaktari wanaweza kufanya upasuaji ili kuondoa uvimbe wako na wakupe aina zingine za matibabu ya saratani, kama vile tiba ya mionzi, tibakemikali na dawa.