Kuanguka kwa Watu Wazee

Imepitiwa/Imerekebishwa Jul 2023

Watu wengi wazee wana hofu ya kuanguka na wana sababu nzuri ya kufanya hivyo. Kuanguka ni tukio la kawaida—angalau mtu 1 kati ya watu 3 wazee huanguka mara moja kwa mwaka. Kuanguka kunaweza kusababisha majeraha mabaya.

  • Mtu ambaye amewahi kuanguka mara moja ana uwezekano wa kuanuka tena

  • Kuanguka si sehemu ya kawaida ya kuzeeka

  • Kuanguka ni kisababishi kikuu cha vifo vya kiajali

  • Matukio ya kuanguka hufanyika wakati wa mwendo, kwa mfano wakati unatoka kitandani au unaharakisha kuchukua simu

  • Baadhi ya matukio ya kuanguka yanaweza kuzuiwa kwa kufanya mazoezi na kuchukua hatua za kuimarisha usalama wa nyumba yako

Ni nini husababisha watu wazee kuanguka?

Matukio mengi ya kuanguka husababishwa na matatizo ya mwili au na hatari zilizoko nyumbani.

Matatizo ya mwili yanaweza kuongeza uwezekano wa kuanguka:

  • Matatizo ya kuwa imara

  • Matatizo ya kuondoka sehemu moja hadi nyingine

  • Matatizo ya kuona vizuri

  • Matatizo ya kuhisi miguu yako

  • Dawa zinazokufanya uhisi kizunguzungu au usingizi

  • Matatizo ya shinikizo la damu au moyo

  • Kuchanganyikiwa

  • Udhaifu wa misuli

  • Ugonjwa

Hatari zilizo karibu nawe zinazoongeza uwezekano wa kuanguka:

  • Giza au taa zenye mwangaza hafifu

  • Sakafu zinazoteleza

  • Nyaya za muunganisho wa umeme au vifaa vilivyo kwenye njia ya kutembelea

  • Vitu vilivyoachwa ovyoovyo sakafuni au kwenye ngazi

  • Vinjia vya miguu visivyo sawasawa na vizuio vilivyovunjika

  • Kuwa mahali usipopajua vizuri

Majeraha yapi hutokea zaidi kutoakana na kuanguka?

Kuanguka kunaweza kusababisha:

  • Mifupa iliyovunjika, hususani mfupa wa nyonga kuvunjika, kwa sababu watu wazee mara nyingi huwa na mifupa dhaifu (ugonjwa wa kudhoofu kwa mifupa)

  • Kuvilia, kuteguka, au kutenguka

  • Majeraha makubwa ya kukatwa

  • Uharibifu wa ogani

  • Kano zilizochanika

  • Jeraha la kichwa

Ukianguka ukiwa pekee yako na ulazimike kukaa sakafuni kwa muda mrefu, huenda ukapata matatizo kama vile:

  • Upungufu wa maji mwilini (ambapo kiwango cha maji mwilini hakitoshi)

  • Halijoto ya mwili kupungua (hipothemia)

  • Nimonia—maambukizi kwenye mapafu yako

Je, nitarajie nini ninapokwenda kumwona daktari wangu?

Madaktari watakuuliza kilichotokea na iwapo ulikuwa na dalili zozote kabla ya kuanguka (kama vile kizunguzungu au maumivu ya kifua). Watakuuliza kuhusu dawa zako na iwapo umekuwa ukinywa pombe.

Madaktari watafanya uchunguzi wa mwili ili kubaini iwapo una majeraha na kujua ni kwa nini ulianguka. Wataangalia:

  • Shinikizo la damu—shinikizo la damu yako likishuka unaposimama, huenda kuanguka kwako kulisababishwa na kizunguzungu au wepesi wa kichwa

  • Moyo wako ili waone kama una matatizo ya mapigo ya moyo, mtindo wa mapigo ya moyo usio wa kawaida, au moyo kushindwa kufanya kazi

  • Uthabiti wa misuli

  • Macho na uwezo wa kuona

  • Uwezo wa kuwa imara na kutembea kwa urahisi

Madaktari hutibu vipi matatizo ya kuanguka?

Madaktari watafanya:

  • Kutibu majeraha yaliyotokana na kuanguka kwako

  • Kutibu matatizo yoyote ambayo huenda yalisababisha uanguke

  • Kukusaidia kutengeneza mpango wa kuzuia kuanguka katika siku za usoni

  • Kukupa rufaa ya tiba ya mazoezi ya mwili au shughuli za kila siku, panapohitajika

Athari za kuanguka zinaweza kudumu kwa muda mrefu. Kwa mfano, mfupa wako wa nyonga ukivunjika, huenda usiweze kutembea vizuri hata baada ya matibabu na mazoezi ya kurejesha hali.

Hofu ya kuanguka inaweza pia kusababisha matatizo kama vile kupunguza shughuli na kukakamaa kwa viungo.

Ninawezaje kuzuia kuanguka?

  • Fanya mazoezi mara kwa mara—mazoezi ya kuinua vitu vizito, kuwa imara, na kujinyoosha ni muhimu

  • Vaa viatu vyenye soli zisizoteleza

  • Amka polepole baada ya kuketi au kulala ili uepuke kuhisi kizunguzungu

  • Mwombe daktari akuonyeshe mbinu ya Epley ikiwa una matatizo ya kizunguzungu (kisulisuli)

  • Zungumza na daktari wako kuhusu dawa unazotumia ili kuona kama kunazo zinazoweza kuongeza uwezekano wa kuanguka

  • Hakikisha kuwa uwezo wako wa kuona umeangaliwa na upate miwani mipya ikiwa unaihitaji, na uhakikishe kuwa umepata matibabu ya glaukoma au mtoto wa jicho

  • Shirikiana na tabibu wa mazoezi ya mwili, hususan iwapo unatumia kifaa au fimbo ya kutembelea, ili ufahamu jinsi ya kuitumia kwa usalama

Imarisha usalama wa nyumba yako:

  • Hakikisha una mwangaza wa kutosha

  • Weka swichi za taa ambazo ni rahisi kufikia au kitambuzi cha mwendo

  • Weka taa kwenye ngazi za ndani na nje ya nyumba

  • Weka vishoroba visivyoteleza na vishikio thabiti vya mikono kwenye ngazi

  • Ongeza soketi zaidi za umeme au ufunge nyaya za umeme zinazopita milangoni (au chini ya zulia) kwa njia salama ili uepuke kujikwaa

  • Ondoa vitu visivyotakikana kwenye sakafu na ngazi

  • Weka pau za kushikilia ndani ya bafu karibu na choo na hodhi

  • Weka kitii cha chooni kilichoinuliwa

  • Fungilia mazulia madogo chini kwa utepe (au uyaondoe kabisa)

  • Weka mikeka ya kuzuia kuteleza ndani ya bafu na jikoni

  • Weka vitu unavyovitumia sana nyumbani kwenye sehemu ambapo hutalazimika kujinyoosha au kuinama ili uvifikie

Ukianguka na ushindwe kuinuka, geuka ulalae kwa tumbo yako kisha utambae hadi palipo na fanicha, kisha uitumie kujivuta juu. Weka simu mahali unapoweza kuifikia ukiwa sakafuni au uvae kifaa cha ilani za matibabu

Just the Right Height

For people who are recovering from a leg injury or surgery, using a cane that is the correct height is important. A cane that is too long or too short can cause low back pain, poor posture, and instability. The cane should be held on the side opposite of an injured leg.