Mvilio wa Damu kwenye Mshipa wa Damu wa Figo

Imepitiwa/Imerekebishwa Oct 2023

Figo zako ni viungo 2 vyenye umbo la maharagwe ambavyo hutengeneza mkojo (haja ndogo), husawazisha viwango vya maji na madini mwilini, na huchuja uchafu kwenye damu yako.

The Urinary Tract

Je, mvilio wa damu kwenye mshipa wa damu wa figo ni nini?

Mvilio wa damu kwenye mshipa wa damu wa figo ni uwepo wa damu iliyoganda kwenye vena ya figo, ambayo ndio vena kuu inayosafirisha damu kutoka kwenye figo zako

  • Mvilio wa damu kwenye mshipa wa damu wa figo unaweza kusababisha uharibifu wa figo

  • Figo lako moja au yote yanaweza kuathiriwa

  • Dalili ni pamoja na maumivu kwenye kifua, mgongo, na nyonga, na kukojoa kwa nadra

  • Madaktari hukufanya utumie dawa ili kuvunjavunja damu iliyoganda

Je, nini husababisha mvilio wa damu kwenye mshipa wa damu wa figo?

Mvilio wa damu kwenye mshipa wa damu wa figo mara nyingi husababishwa na:

Sababu nyingine zinajumuisha:

Je, dalili za mvilio wa damu kwenye mshipa wa damu wa figo ni zipi?

Kwa kawaida unakuwa huna dalili isipokuwa kama ukipata hali ya kushindwa kwa figo kufanya kazi. Dalili za figo kushindwa kufanya kazi ni pamoja na:

  • Kuhisi udhaifu na uchovu

  • Kuhisi mgonjwa tumboni

  • Kutohisi njaa kama kawaida

  • Kuwasha

  • Kuhisi usingizi au kuchanganyikiwa

Kama mvilio kwenye mshipa wa damu umesababishwa na kuongezeka kwa ugandaji wa damu wa jumla, unaweza kupata dalili za damu iliyoganda kwenye ogani zako zingine, kama vile kwenye:

  • Mapafu: Maumivu ya kifua na kuishiwa na pumzi

  • Ubongo: Dalili za kiharusi, kama vile udhaifu na kuchanganyikiwa

  • Miguu: Kuvimba na maumivu kwenye mguu

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina mvilio wa damu kwenye mshipa wa damu wa figo?

Ili kujua kama una mvilio wa damu kwenye mshipa wa damu wa figo, madaktari wanaweza kufanya:

  • Angiografia ya upigaji picha kwa kutumia MRI (aina ya MRI inayozingatia mishipa ya damu)

  • Angiografia ya upimaji kwa kompyuta (aina ya uchanganuzi wa CT unaozingatia mishipa ya damu)

  • Kipimo cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti

Pia madaktari watafanya vipimo vya damu na mkojo ili kutafuta ishara za uharibifu wa figo na sababu zingine za mvilio kwenye mshipa wa damu.

Je, madaktari hutibu vipi mvilio wa damu kwenye mshipa wa damu wa figo?

Madaktari hutibu sababu yoyote inayosababisha mvilio wa damu kwenye mshipa wa damu wa figo? Pia kwa kawaida watakupatia:

  • Dawa za kuzuia damu kuganda (dawa za kulainisha damu)

Wakati mwigine wataondoa donge la damu kutoka kwenye vena ya figo kwa kutumia katheta au watakupatia dawa ambazo zitavunjavunja donge la damu.