Kuzuizi cha Ateri za Figo

Imepitiwa/Imerekebishwa Oct 2023

Figo zako ni viungo 2 vyenye umbo la maharagwe ambavyo hutengeneza mkojo (haja ndogo), husawazisha viwango vya maji na madini mwilini, na huchuja uchafu kwenye damu yako.

The Urinary Tract

Je, kuzuizi cha ateri za figo ni nini?

Ateri za figo ni mishipa ya damu ambayo husafirisha damu hadi kwenye figo zako. Kizuizi kinamaanisha ateri za figo hupunguzwa au kuziba hivyo damu kushindwa kupenya.

  • Ateri za figo zinaweza kuzuiwa kwa taratibu kwa kupungua au kwa ghafla kwa damu iliyoganda

  • Kizuizi cha ghafla kwenye ateri za figo husababisha maumivu ya kuuma kwenye sehemu ya chini ya mgongo wako au tumbo, homa, au kichefuchefu

  • Kizuizi kinaweza kusababisha shinikizo la juu la damu au figo kushindwa kufanya kazi

  • Madaktari hutibu kuzuizi kwenye ateri za figo kwa kutumia dawa au kwa upasuaji

Je, nini husababisha kizuizi cha ateriza figo?

Ateri zako za figo zinaweza kuziba ikiwa:

  • Damu iliyoganda kutoka sehemu nyingine ya mwili itasafirishwa na damu yako hadi kwenye figo yako moja au zote

  • Damu itaganda kwenye ateri yako

  • Ateri zako zitageuka kuwa ngumu (atherosklerosisi) au matatizo mengine ya kiafya yanayoweza kufanya kuta za ateri za figo zako kuwa nene, ngumu, na nyembamba

Kwa kawaida damu iliyoganda huathiri figo moja tu. Kwa kawaida kusinyaa kwa ateri huathiri figo zote.

Je, dalili za ateri za figo zilizoziba ni zipi?

Kizuizi cha ghafla, cha moja kwa moja kinaweza kusababisha:

  • Maumivu ya kuuma kwenye sehemu ya chini ya mgongo au sehemu ya chini ya tumbo

  • Homa

  • Kuhisi mgonjwa tumboni na kutapika

Kwa kawaida kizuizi cha ghafla, cha moja kwa moja huathiri figo moja tu. Kwa kawaida figo yako nyingine huchukua jukumu la kuchuja damu yako na kutengeneza mkojo na hupati hali ya figo kushindwa kufanya kazi.

Kwa kawaida kizuizi cha sehemu hakisababishi dalili zozote, lakini kinaweza kukusababishia:

Kwa kawaida kizuizi cha sehemu huathiri figo zote. Hali ikiendelea kwa muda mrefu, unaweza kupata tatizo la figo kushindwa kufanya kazi.

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa ateri zangu za figo zimeziba?

Madaktari hushuku uwepo wa kizuizi kutokana na dalili zako. Wanaweza kufanya vipimo vya upigaji picha wa njia ya mkojo:

  • Angiografia ya upimaji kwa kompyuta (aina ya uchanganuzi wa CT unaozingatia mishipa ya damu), angiografia ya upigaji picha kwa kutumia MRI (aina ya MRI inayozingatia mishipa ya damu), au kipimo cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti

  • Wakati mwingine, angiografia ya kawaida (kuingiza kimiminiko maalum kinachoitwa majimaji yenye kutofautisha kwenye mishipa ya damu yako, hivyo kuwaruhusu madaktari kuona mishipa yako ya damu kwenye eksirei)

Pia watafanya vipimo vya damu na mkojo ili kuona jinsi figo zako zinavyofanya kazi vizuri.

Je, madaktari hutibu vipi kizuizi kwenye ateri za figo?

Madaktari hufanya matibabu mbalimbali kutegemea na chanzo cha kizuizi hicho:

  • Damu iliyoganda: Vilainisha damu (vizuizi vya damu kuganda) ili kuzuia madonge ya damu yasiongezeke ukubwa au kusitokee madonge mengine ya damu

  • Ateri zilizopungua: Upasuaji au kufungua mishipa ili kufua ateri

Wakati wa ufunguaji mishipa, madaktari hupitisha bomba jembamba kwenye kinena chako hadi kwenye ateri iliyoziba ili waweze kuipanua kwa kutumia puto dogo au bomba dogo la waya linaloitwa stent.

Ikiwa kizuizi kilisababisha shinikizo la juu la damu, madaktari watakupatia dawa ya shinikizo la juu la damu.

Ikiwa una tatizo la figo kushindwa kufanya kazi, unaweza kuhitaji huduma ya kusafisha damu (mashine ya kuchuja damu wakati figo zinaposhindwa kufanya hivyo).