Ugonjwa wa Chembe Kuziba Mishipa ya Damu ya Figo

Imepitiwa/Imerekebishwa Oct 2023

Figo zako ni viungo 2 vyenye umbo la maharagwe ambavyo hutengeneza mkojo (haja ndogo), husawazisha viwango vya maji na madini mwilini, na huchuja uchafu kwenye damu yako.

Njia ya Mkojo

Je, ugonjwa wa chembe kuziba mishipa ya damu ya figo ni nini?

Ugonjwa wa chembe kuziba mishipa ya damu ya figo husababishwa na chembechembce ndogo ngumu za mafuta kwenye ateri zako zinapobanduka na kuziba ateri ndogo ambazo husambaza damu kwa figo zako. Chembechembe hizo ngumu za mafuta huitwa emboli.

  • Ugonjwa wa chembe kuziba mishipa ya damu ya figo unaweza kuathiri figo moja au zote mbili

  • Ikiwa figo zote zitaathiriwa vibaya sana, unaweza kupata hali ya figo kushindwa kufanya kazi.

  • Kwa kawaida husababishwa na upasuaji au utaratibu wa matibabu ya ateri

  • Figo kushindwa kufanya kazi hugunduliwa kwa kipimo cha damu

  • Madaktari hawawezi kurekebisha uharibifu wa figo, lakini wanaweza kujaribu kuzuia hali yake isizidi kuwa mbaya

  • Unaweza kuhitaji huduma ya kusafisha damu (mchakato wa kuchuja damu yako wakati figo zako hazina uwezo wa kufanya hivyo)

Je, nini husababisha ugonjwa wa chembe kuziba mishipa ya damu ya figo?

Pale unapopata hali ya ateri zako kuwa ngumu (atherosklerosisi), ateri zako huziba kwa kitu chenye mafuta magumu. Vipande vya mafuta ya mwili vinaweza kubanduka na kuelea kwenye damu yako hadi vikanasa kwenye mshipa mdogo wa damu. Kama kiasi cha kutosha cha mafuta hayo ya mwili yatanasa kwenye mishipa ya damu katika ogani moja, ogani hiyo inaweza kushindwa kufanya kazi.

Ugonjwa wa chembe kuziba mishipa ya damu ya figo mara nyingi hutokea baada ya kufanyiwa upasuaji au tiba inayohusisha mkole wako (ateri kubwa zaidi kwenye mwili wako). Chembechembe za mafuta ya mwili zilizoganda kwenye ukuta wa mkole wako zinaweza kubanduka kwa bahati mbaya wakati wa matibabu na kusafiri hadi kwenye figo zako. Wakati mwingine mafuta ya mwili hubanduka yenyewe.

Mafuta hayo ya mwili yanaweza kuziba mishipa ya damu katika viungo vingine kwenye tumbo lako, kama vile utumbo na kongosho.

Je, dalili za ugonjwa wa chembe kuziba mishipa ya damu ya figo ni Zipi?

Kwa kawaida unakuwa huna dalili isipokuwa kama ukipata hali ya figo kushindwa kufanya kazi. Dalili za figo kushindwa kufanya kazi ni pamoja na:

  • Kuhisi udhaifu na uchovu

  • Kuhisi mgonjwa tumboni

  • Kutohisi njaa kama kawaida

  • Kuwasha

  • Kuhisi usingizi au kuchanganyikiwa

Ni nadra, kwa uharibifu wa figo kusababisha Shinikizo la juu la damu

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina ugonjwa wa chembe kuziba mishipa ya damu ya figo?

Madaktari wanaweza kushuku uwepo wa ugonjwa wa chembe kuziba mishipa ya damu ya figo ikiwa vipimo vya kila mara vya damu au mkojo vitaonyesha kuwa figo zako hazifanya kazi kama kawaida mara baada ya kufanyiwa upasuaji au matibabu ya mkole wako. Ili kuwa na uhakika, wakati mwingine:

  • Watafanya uondoaji wa kipande cha tishu kwa uchunguzi (wataondoa kipande cha tishu ya figo kwa ajili ya kukichunguza kwenye hadubini)

  • Kipimo cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti

Je, madaktari hutibu vipi ugonjwa wa chembe kuziba mishipa ya damu ya figo?

Madaktari hawawezi kurekebisha uharibifu wa figo, lakini wanaweza kukutibu ili kukusaidia kuzuia emboli kwa:

  • Dawa ili kuzuia kukusanyika kwa mafuta ya mwili zaidi kwenye ateri zako

Ikiwa figo zako zimeharibika kwa kiasi kikubwa, unaweza kuhitaji: