Nefrosklerosis ya Kawaida ya Shinikizo la Juu la Damu

Imepitiwa/Imerekebishwa Oct 2023

Figo zako ni viungo 2 vyenye umbo la maharagwe ambavyo hutengeneza mkojo (haja ndogo), husawazisha viwango vya maji na madini mwilini, na huchuja uchafu kwenye damu yako.

Njia ya Mkojo

Je, nefrosklerosis ya kawaida ya shinikizo la juu la damu ni nini?

Haipatensheni ni shinikizo la juu la damu, viateri ni ateri ndogo, "nefro" humaanisha figo na "sklerosis" ni kupata makovu au uharibifu.

Nefrosklerosis ya kawaida ya shinikizo la juu la damu ni uharibifu wa figo unaosababishwa na kuwa na shinikizo la juu la damu kwa muda mrefu.

  • Kwa kawaida uharibifu wa figo huzidi kuwa mbaya kwa taratibu na unaweza kusababisha ugonjwa wa figo sugu ambao ni mbaya

  • Ni kawaida zaidi ikiwa shinikizo lako la damu limekuwa juu kwa muda mrefu

  • Kwa kawaida uharibifu wa figo hugundulika kwa kipimo cha damu  

  • Kwa kawaida unakuwa huna dalili hadi unapopata hali ya figo kushindwa kufanya kazi

  • Madaktari hujaribu kudhibiti shinikizo la damu kwa kutumia dawa

  • Unaweza kuhitaji huduma ya kusafisha damu (mashine huchuja damu yako pale ambapo figo zake hazina uwezo wa kufanya hivyo)

Je, nini husababisha haipatensheni ya uharibifu wa figo?

Kuwa na shinikizo la juu la damu kwa muda mrefu huweka mkazo kwenye mishipa yako ya damu. Mwishowe, mkazo unaharibu mishipa ya damu hivyo damu haitiririki vizuri ndani yake. Kama mtiririko wa damu kwenda kwenye ogani ni duni, ogani inaweza kuharibiwa.

Hatari yako ya kuharibika kwa figo kutokana na shinikizo la juu la damu ni kubwa ikiwa:

  • Shinikizo lako la damu halidhibitiwi vizuri

  • Umekuwa na shinikizo la juu la damu kwa muda mrefu

Je, zipi ni dalili za uharibifu wa figo utokanao na shinikizo la juu la damu?

Kwa kawaida unakuwa huna dalili isipokuwa kama ukipata hali ya kushindwa kwa figo kufanya kazi. Dalili za figo kushindwa kufanya kazi ni pamoja na:

  • Kuhisi udhaifu na uchovu

  • Kuhisi mgonjwa tumboni

  • Kutohisi njaa kama kawaida

  • Kuwasha

  • Kuhisi usingizi au kuchanganyikiwa

Je, madaktari wanawezaje kujua kama nina uharibifu wa figo utokanao na shinikizo la juu la damu?

Madaktari hushuku uwepo wa ugonjwa wa figo ikiwa umewahi kuwa na shinikizo la damu kwa muda mrefu na vipimo vya damu vya kila mara vinaonyesha kuwa figo zako hazifanyi kazi kama kawaida. Ili kuchunguza sababu zingine za ugonjwa wa figo, wanaweza kufanya:

  • Vipimo vya damu na mkojo

  • Kipimo cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti kwa figo

Je, madaktari hutibu vipi uharibifu wa figo utokanao na shinikizo la juu la damu?

Madaktari hujaribu kudhibiti uharibifu usiweze kuwa mbaya zaidi kwa:

Ikiwa figo zako zimeharibiwa vibaya, unaweza kuhitaji: