Kichocho

(Ugonjwa wa kichocho)

Imepitiwa/Imerekebishwa Jul 2023

Je, ugonjwa wa kichocho ni nini?

Ugonjwa wa kichocho ni maambukizi yanayosababishwa na kimelea kidogo kinachoitwa mnyoo bapa.

  • Minyoo bapa hupatikana zaidi katika mito na maziwa katika maeneo ya tropiki huko Amerika ya Kusini, Afrika na Asia

  • Unaweza kupata ugonjwa wa kichocho kwa kuogelea au kuoga kwenye maji yenye minyoo bapa

  • Minyoo bapa hupenya kwenye ngozi yako na kusafiri kupitia damu yako

  • Mwishowe huishia katika mishipa midogo ya damu ndani ya utumbo au kibofu chako cha mkojo

  • Kwanza dalili hujumuisha ukurutu wenye kuwasha, ukifuatiwa na homa, mzizimo, misuli kuuma, udhaifu na maumivu ya tumbo

  • Madaktari hupima sampuli za kinyesi (choo kikubwa) na mkojo ili kuona kama kuna mayai ya minyoo bapa

  • Madaktari watakutibu kwa dawa za kuua vimelea ili kuua minyoo bapa

Je, nini husababisha ugonjwa wa kichocho?

Ugonjwa wa kichocho husababishwa na kimelea kinachoitwa mnyoo bapa, ambacho ni aina ya mnyoo mviringo Minyoo iliyokomaa ina urefu wa takribani inchi ¼ hadi ¾ (sentimita 1 hadi 2)

Unapata ugonjwa wa kichocho kwa kuongelea, kutembea kwenye maji, au kuoga kwenye maji baridi ambayo yana hawa minyoo bapa.

  • Wakati ukiwa kwenye maji, minyoo bapa hupanda ngozi yako

  • Minyoo bapa hupenya kwenye ngozi yako, na kisha kusafiri kupitia damu yako hadi kwenye kibofu cha mkojo au utumbo wako

Minyoo bapa iliyopo kwenye kibofu cha mkojo au utumbo wako hutaga mayai mengi:

  • Mayai husumbua tishu zako na kusababisha vidonda, majeraha na kuvuja damu

  • Baadhi ya mayai hutiririka kutoka kwenye utumbo hadi kwenye ini

  • Mayai hutoka mwilini mwako kupitia kinyesi au mkojo wako

  • Ikiwa mkojo au kinyesi chako kitaingia kwenye maji baridi, mayai huaguliwa na kukua hadi kuweza kumwambukiza mtu mwingine

Pale mayai yanapotiririka kutoka kwenye utumbo hadi kwenye ini, ini lako linaweza kuvimba. Hali hii inaweza kusababisha majeraha na kuongezeka kwa shinikizo kwenye mshipa wa lango. Mshipa wa lango husafirisha damu kati ya mfumo wa utumbo na ini. Shinikizo la juu la damu kwenye mshipa wa lango (huitwa shinikizo la juu la damu kwenye mshipa wa lango) linaweza kusababisha bandama lako kutanuka. Pia, inaweza kusababisha damu kuvuja kwenye mishipa iliyopo kwenye umio lako ("umio ya chakula" inayounganisha koo lako na tumbo lako).

Je, zipi ni dalili za ugonjwa wa kichocho?

Watu wengi huwa hawana dalili. Minyoo bapa inapoingia mwilini mwako kwa mara ya kwanza, unaweza kupata:

  • Ukurutu unaowasha

Baada ya wiki chache, unaweza kuanza kuumwa na kupata dalili kama vile:

  • Homa

  • Baridi

  • Kikohozi

  • Maumivu ya misuli

  • Maumivu ya tumbo

Kwa kutegemea sehemu ya mwili ilipo minyoo bapa iliyokomaa unaweza kupata: 

  • Maumivu wakati wa kukojoa na damu kwenye mkojo wako

  • Kuhara damu (Kinyesi chepesi, chenye majimaji)

  • Kutanuka kwa ini na bandama

Maambukizi makali yanaweza kukufanya upoteze damu ya kutosha ukapata:

  • Anemia (kiwango cha chini cha seli nyekundu za damu)

Pia ugonjwa wa kichocho unaweza kuathiri viungo vingine, kama vile mapafu, uti wa mgongo, figo na ubongo.

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina ugonjwa wa kichocho?

Madaktari hushuku uwepo wa ugonjwa wa kichocho kutokana na dalili zako, hasa ikiwa uliogelea au kuoga kwenye maji yanayoweza kuwa na maambukizi hivi karibuni. Madaktari hupima uwepo wa ugonjwa wa kichocho kwa kutafuta mayai ya minyoo bapa kwenye:

  • Kinyesi

  • Mkojo

  • Tishu za utumbo na kibofu cha mkojo

Wakati mwingine, madaktari pia hufanya vipimo vya damu, kipimo cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti, au uchanganuzi wa CT ili kuona maambukizi ni makali kwa kiasi gani.

Je, madaktari hutibu vipi ugonjwa wa kichocho?

Madaktari hutibu ugonjwa wa kichocho kwa kutumia:

  • Dawa za kuzuia vimelea

Pia madaktari wanaweza kupima kinyesi au mkojo wako baada ya mwezi 1 au miezi 2 baadaye ili kuhakikisha kuwa hakuna tena mayai ya minyoo bapa ndani yake.

Je, ninawezaje kuzuia ugonjwa wa kichocho?

Unaweza kusaidia kuzuia ugonjwa wa kichocho kwa:

  • Kutokuogelea, kuoa au kutembea kwenye maeneo yanayojulikana kuwa yana minyoo bapa

  • Katika maeneo ambapo kuna tatizo la minyoo bapa, kuchemsha maji au kuyahifadhi kwa siku moja au mbili kabla ya kuyaoga

  • Kujikausha vizuri kwa taulo ikiwa utaingia kwa bahati mbaya kwenye maji yaliyochafuliwa—hii husaidia kuondoa vimelea kabla ya kupenda kwenye ngozi yako

Mayai yanapoanguliwa kwenye maji, minyoo bapa huambukiza konokono. Hivyo, baadhi ya watu huweka kemikali ambazo zinaua konono kwenye vyanzo vya maji baridi vinavyojulikana kuwa na minyoo bapa.