Malaria ni nini?
Malaria ni maambukizi yanayosababishwa na kimelea kinachoitwa Plasmodium.
Malaria husambazwa na mbu
Kila mwaka mamilioni ya watu duniani kote hupata malaria
Takribani watu nusu milioni hufa kwa malaria kila mwaka, hasa watoto
Malaria husababisha homa na mzizimo
Hutambuliwa kwa kutumia kipimo cha damu
Dawa kadhaa hutibu malaria, lakini vimelea vinakuwa sugu kwa dawa
Malaria ilikuwa ikitokea karibu kila mahali duniani. Sasa iko katika sehemu zenye joto zaidi ulimwenguni kama vile:
Amerika Kusini
Amerika ya Kati na Visiwa vya Karibi
Afrika
India na sehemu zingine za Asia ya Kusini
Mashariki ya kati
Je, nini husababisha malaria?
Kuna spishi 5 za vimelea vya malaria vinavyoathiri watu.
Vimelea vya malaria huishi kwenye seli nyekundu za damu za watu walioathiriwa
Pale mbu wanapomuua mtu mwenye maambukizi, hubeba vimelea
Mtu anayefuata atakayeumwa na mtu anaweza kupata maambukizi
Vimelea vya malaria kwanza huenda kwenye ini ili vikomae na kuzaliana. Kisha vimelea huingia kwenye damu na kuzaliana ndani ya seli nyekundu za damu yako.
Mwishowe seli nyeupe za damu hupasuka na kuachia vimelea, ambavyo huambukiza seli nyekundu za damu zaidi
Iwapo seli nyingi nyekundu za damu zitaharibiwa, unaweza kuwa na kiwango cha chini cha damu (anemia)
Aina hatari zaidi ya malaria inaitwa malaria ya falciparum. Malaria ya falciparum hasa ni hatari kwa sababu seli nyekundu za damu zilizo ambukizwa zinaweza kuziba mishipa midogo ya damu na kusababisha uharibifu wa viungo. Zinaweza kuharibu ubongo, figo, mapafu yako, na viunge vingine Aina zingine za malaria huwa hazifanyi hivi.
Zipi ni dalili za malaria?
Unaweza usipate dalili kwa wiki kadhaa au zaidi mara baada ya kuumwa na mbu mwenye maambukizi. Kisha unapata:
Homa kali
Mzizimo wa kutetemeka (tetemeka sana)
Maumivu ya kichwa, misuli kuuma, na kuumwa sana
Homa na mzizimo huja na kupotea kila baada ya siku kadhaa. Jinsi maambukizi yanavyoendelea, unaweza kupata:
kiwango cha chini cha damu (anemia)
Macho na ngozi ya manjano (homa ya nyongo ya manjano)
Malaria ya falciparum pia husababisha dalili nyingine kutegemea na viungo vilivyoambukizwa:
Ubongo: Maumivu ya kichwa, kuchanganyikiwa, kupoteza fahamu, kifo
Mapafu: Kupumua kwa shida
Figo: Mkojo mweusi, figo kushindwa kufanya kazi
Kiwango cha chini cha sukari kwenye damu (hipoglisemia)
Wajawazito wanaweza kupata tatizo la kuharibika mimba, au watu wao wachanga wanaweza kuambukizwa
Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina malaria?
Madaktari hufanya:
Vipimo vya damu
Kuna aina 2 za vipimo vya damu: (1) vipimo vya haraka kwa kutumia damu inayowekwa kwenye kadi na (2) vipimo vya kuchunguza damu kwenye hadubini. Mara nyingi madaktari hufanya aina zote mbili za vipimo.
Je, madaktari hutibu vipi malaria?
Dawa za malaria hutegemea ni spishi gani uliyonayo na umeipata wapi. Katika baadhi ya maeneo ya dunia, vimelea vya malaria ni sugu kwa dawa nyingi za malaria.
Katika baadhi ya maeneo ya mbali ambako malaria ni ya kawaida, dawa za malaria zinazouzwa katika maduka ya dawa ya mtaani zinaweza kuwa ni bandia. Ikiwa unasafiri kwenda katika maeneo yenye hatari kubwa, daktari wako anaweza kukufanya ubebe dawa za malaria kama tahadhari iwapo utapata maambukizi.
Ninawezaje kuzuia malaria?
Mnamo tarehe 6 Oktoba, 2021, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilipendekeza matumizi makubwa ya chanjo ya malaria miongoni mwa watoto wanaoishi Kusini mwa Jangwa la Sahara na katika maeneo mengine yenye maambukizi ya wastani hadi ya juu ya maambukizi ya malaria ya Plasmodium falciparum.
Iwapo utatembelea au unaishi katika eneo ambalo lina malaria, unapaswa:
Kufanya vitu ili kuepuka kuumwa na mbu
Tumia dawa za kuzuia ili kuua vimelea vya malaria
Ili kuepuka kuumwa na mbu:
Lala ndani ya chandarua cha kuzuia mbu chenye kiuwa wadudu cha permethrin
Jipake kifukuza mbu chenye DEET (daethiltoluamidi)
Vaa suruali ndefu and mashati ya mikono mirefu, hasa jioni na alfajiri
Iwapo utakumbana na hatari ya mbu wengi, vaa nguo ambazo zimepakwa permethrin
Watu wanaoishi katika maeneo ambayo yana malaria mara nyingi hunyunyiza viuwa wadudu kwenye makazi na majengo yao ya nje, huweka wavu kwenye milango na madirisha, na kusafisha maji yoyote yasiyotiririka (kama vile kwenye matairi ya zamani, vyungu vya maua, au madimbwi), ambapo mbu hupenda kuzaliana.
Unaweza kutumia dawa ili kuzuia malaria. Dawa nyingi tofauti zinapatikana. Daktari wako anaweza kukushauri ni ipi inayofaa kwa mahali unaposafiri na kwa hali ya afya yako. Utapaswa kuanza kutumia dawa kabla ya kufika kwenye eneo lenye malaria.