Ugonjwa wa shida ya kupumua kwa watoto waliozaliwa karibuni ni nini?
Upumuaji unahusiana na kupumua. Ugonjwa wa shida ya kupumua ni aina ya tatizo la kupumua ambalo linaweza kuwapata watoto waliozaliwa hivi karibuni.
Ugonjwa wa shida ya kupumua hutokea pale mapafu ya mtoto wako yanapokuwa magumu na hayawezi kubaki wazi yakashikilia pumzi
Hutokea pale mapafu ya mtoto wako yanaposhindwa kuunda safaktanti ya kutosha, dutu ambayo husaidia mapafu kubaki wazi
Hutokea zaidi kwa watoto waliozaliwa kabla ya wakati wao
Ikiwa mtoto wako atazaliwa mapema sana, madaktari watakupatia dawa ambayo itasaidia mapafu ya mtoto wako kuunda safaktanti
Baada ya kuzaliwa, madaktari huweka dawa chini ya bomba la pumzi la mtoto wako na kumpatia oksijeni
Je, nini husababisha ugonjwa wa shida ya kupumua?
Kabla ya kuzaliwa, mapafu yako huwa yamefungwa. Mara baada ya kuzaliwa, mtoto wako huvuta pumzi kwa nguvu ili kufungua mapafu na kuyajaza hewa. Ndani ya mapafu kumepakwa dutu ambayo huyafanya yafunguke kwa urahisi. Dutu hiyo huitwa safaktanti.
Watoto waliozaliwa mapema sana (watoto waliozaliwa kabla ya muda wao) huwa hawana safaktanti ya kutosha. Mapafu yao ni magumu kufunguka na mtoto anaweza kupata tatizo la kupumua.
Kwa kawaida ugonjwa wa shida ya kupumua hutokea kwa:
Watoto waliowahi kuzaliwa kwa zaidi ya mwezi mmoja
Jinsi mtoto wako anavyozaliwa mapema, ndivyo alivyo na nafasi kubwa ya kupata ugonjwa wa shida ya kupumua. Vigezo vingine vya hatari ni pamoja na:
Kubeba mimba ya zaidi ya mtoto mmoja, kwa mfano, mapacha, mapacha watatu au mapacha wanne
Zipi ni dalili za ugonjwa wa shida ya kupumua?
Dalili huanza mara baada ya kuzaliwa au ndani ya saa chache. Watoto wachanga wana dalili kama vile:
Kupumua haraka
Inaonekana anatatizika kupumua
Tundu za pua zenye kutanuka wakati wa kuvuta hewa ndani
Kukoroma ukitoa pumzi
Ngozi ya bluu inayosababishwa na viwango vya chini vya oksijeni
Iwapo hatatibiwa, hali ya upumuaji ya mtoto wako itakuwa mbaya. Ukosefu wa oksijeni unaweza kusababisha uharibifu wa ubongo au matatizo mengine.
Madaktari wanawezaje kujua ikiwa mtoto wangu ana ugonjwa wa shida ya kupumua?
Madaktari hushuku uwepo wa ugonjwa wa shida ya kupumua kulingana na dalili za mtoto wako. Ili kuwa na uhakika:
Watachunguza kiwango cha oksijeni cha mtoto wako
Watapiga eksirei ya kifua
Je, madaktari wanatibu vipi ugonjwa wa shida ya kupumua?
Madaktari wanatibu ugonjwa wa shida ya kupumua kwa watoto waliozaliwa karibuni kwa:
Kumpatia mtoto wako oksijeni ya ziada kupitia mipira ya pua au mfuniko wa plastiki
Kutumia mashine kumsaidia mtoto wako kupumua, iwapo mtoto wako anapata shida sana
Kumpatia safaktanti ya bandia kupitia bomba liliwekwa chini ya bomba la pumzi
Ikiwa una uwezekano wa kujifungua mtoto njiti, madaktari watakuchoma sindano ya kotikosteroidi. Dawa hii husaidia mapafu ya mtoto wako kuunda safaktanti na husaidia kuzuia ugonjwa wa shida ya kupumua.
Ikiwa mtoto wako atawahi sana kuzaliwa, madaktari wanaweza kumpatia mtoto wako safaktanti hata kabla ya ugonjwa wa shida ya kupumua kuanza.