Ukuaji usio wa kawaida wa seli na tishu za mapafu (BDP) ni nini?
Ukuaji usio wa kawaida wa seli na tishu za mapafu (BDP) ni uharibifu wa mapafu wa muda mrefu unaotendeka kwa watoto wengine waliokuwa na matatizo mabaya sana ya kupumua wakati wa kuzaliwa.
Mara nyingi BDP hutokea kwa watoto ambao waliwekwa kwenye mashine ya kusaidia kupumua au ambao walihitaji kuwekewa oksijeni kwa kipindi kirefu katika siku za mwanzo za maisha yao.
Mara nyingi BDP huwapata sana watoto waliozaliwa kabla ya wakati wao
Uharibifu wa mapafu unaotokana na BPD huwafanya watoto wahitaji oksijeni ya ziada
Watoto wengi hupata ahueni baada ya miezi kadhaa, lakini hali ikiwa mbaya inaweza kuhatarisha maisha
BPD inaweza kupunguza kasi ya ukuaji na maendeleo ya mtoto wako na kuongeza hatari ya kupata pumu au nimonia
Je, nini husababisha BPD?
Iwapo mtoto wako ana shida ya kupumua, mashine ya kusaidia kupumua na oksijeni ya ziada inaweza kuokoa maisha yake. Lakini mashine ya kusaidia kupumua na oksijeni inaweza kuharibu mapafu ya mtoto wako ikiwa vitatumika kwa kipindi kirefu.
Kuna uwezekano mkubwa wa kutokea kwa uharibifu wa mapafu iwapo mtoto wako:
Amezaliwa kabla ya muda wake
Ana tatizo kubwa la mapafu, kama ugonjwa wa shida ya kupumua
Alipata maambukizi makali akiwa kwenye tumbo la uzazi au mara baada ya kuzaliwa
Zipi ni dalili za BPD?
Dalili kwa watoto hujumuisha:
Kupumua haraka
Inaonekana anatatizika kupumua
Ngozi ya bluu inayosababishwa na viwango vya chini vya oksijeni
Madaktari wanawezaje kujua ikiwa mtoto wangu ana BPD?
Madaktari hushuku uwepo wa BPD ikiwa mtoto wako:
Alizaliwa akiwa njiti na alihitaji mashine ya kumsaidia kupumua kwa kipindi kirefu
Anaendelea kuhitaji oksijeni ya ziada au kuwekwa kwenye mashine ya kumsaidia kupumua baada ya kupata ahueni ya tatizo la mapafu la hapo mwanzo
Ili kuwa na uhakika madaktari watafanya:
Eksirei ya kifua
Je, madaktari hutibu vipi BPD?
Ili kutibu BPD, madaktari:
Watampatia oksijeni mtoto wako kupitia bomba lililowekwa kwenye pua zake
Watamfanya mtoto wako anywe maziwa ya mama ya ziada au maziwa ya kopo ili kusaidia kukua kwa mapafu ya mtoto wako
Watampatia dawa ya kumfanya mtoto wako akojoe ili kupunguza majimaji ya ziada mwilini, ikijumuisha mapafu
Mtoto wako akiondoka hospitalini, madaktari:
Watakufanya uweke mtoto wako mbali na moshi wa sigara
Watampatia mtoto wako dawa na chanjo ya mafua ili kuzuia maambukizi ya mapafu
Watoto wengi hupata ahueni baada ya miezi kadhaa, lakini mtoto wako anaweza kuwa na uwezekano mkubwa wa kupata pumu au nimonia hapo baadaye maishani.