Ugonjwa wa Mpumuo wa Mekoni

Imepitiwa/Imerekebishwa Oct 2022

Mekoni ni dutu iliyo kwenye utumbo wa mtoto wako wakati bado yuko kwenye tumbo lako la uzazi (mtoto ambaye hajazaliwa anaitwa kijusi). Japokuwa kijusi hakili chakula, huwa kinameza maji ya amnioti ambayo kinaelea ndani yake. Haya hutengeneza dutu inayonata, ya rangi ya kijani kibichi kwenye utumbo wa kijusi.

Mpumuo ni pale unapovuta baadhi ya vitu ndani ya mapafu yako.

Ugonjwa wa mpumuo wa mekoni ni nini?

Ikiwa kijusi kina tatizo kabla ya kuzaliwa, kijusi kinaweza kujisaidia mekoni kwenye maji ya amnioti. Ugonjwa wa mpumuo wa mekoni hutokea pale kijusi kinapovuta maji ya amnioti yaliyojaa maekoni kwenye mapafu.

Hakuna madhara ya kuvuta maji ya amnioti yasiyo na kitu kingine. Lakini ikiwa majimaji hayo yana maekoni, mekoni huziba njia za hewa na kuwasha mapafu ya mtoto.

  • Watoto wachanga hupata shida ya kupumua

  • Hupumua kwa haraka, hukoroma wanapotoa pumzi nje na wanaweza kuwa na ngozi yenye rangi ya bluu.

  • Madaktari wanaweza kulazimika kuweka mpira wa kupumulia kwenye bomba la pumzi la mtoto wako na mtoto wako anaweza kuwekwa kwenye mashine ya kumsaidia kupumua.

  • Watoto wengi huendelea kuishi, lakini wana uwezekano mkubwa wa kupata pumu hapo baadaye maishani

Zipi ni dalili za ugonjwa wa mpumuo wa mekoni?

Dalili zinajumuisha:

  • Kupumua haraka

  • Inaonekana anatatizika kupumua

  • Kukoroma ukitoa pumzi

  • Ngozi ya bluu kutokana na viwango vya chini vya oksijeni

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa mtoto wangu ana ugonjwa wa mpumuo wa mekoni?

Madaktari hushuku uwepo wa ugonjwa wa mpumuo wa maekoni ikiwa kuna mekoni katika maji ya amnioti wakati mtoto anapozaliwa na ikiwa mtoto wako ana matatizo ya kupumua. Huenda daktari pia:

Je, madaktari wanatibu vipi ugonjwa wa mpumuo wa mekoni?

Madaktari hutibu mtoto wako kwa:

  • Ufyonzaji ili kuondoa mekoni inayoziba mdomo, pua, na koo la mtoto wako

  • Mpira wa kupumulia kwenye bomba la pumzi la mtoto wako—pia mtoto anaweza kuhitaji CPAP (shinikizo la njia ya hewa endelevu) au chombo cha kupitisha hewa ili kusaidia kupumua

  • Dawa za kuua bakteria ili kuzuia maambukizi