Tatizo la kukosa utulivu ni nini?
Tatizo la kukosa utulivu (ADHD) ni tatizo la ubongo ambalo linafanya iwe vigumu kuzingatia na kuweka umakini na kukaa kwa utulivu. Mara nyingi husababisha matatizo hsuleni na nyumbani.
Dalili za ADHD zinaweza kuwa ndogo au kubwa Maeneo fulani (kama vile shule) yanaweza kufanya ziwe mbaya zaidi.
ADHD inaanza wakati wa utotoni, mara nyingi kufikia umri wa miaka 4
ADHD wakati mwingine inaondoka kadiri mtoto anapokuwa mkubwa, lakini watu wengi wanaendelea kuwa na tatizo hili wakiwa watu wazima
Watoto wenye ADHD wana tatizo la kutoweza kumakinika na wana shughuli nyingi (amilifu kupita kiasi)
Watoto wengi wenye ADHD pia wana matatizo ya kujifunza
Dawa mara nyingi zinawasaidia watoto wenye ADHD
Je, ADHD husababishwa na nini?
Madaktari hawana uhakika kwa nini mtoto anapata ADHD. Pengine husababishwa na matatizo ya jinsi ubongo ulivyoundwa wakati mtoto anakua tumboni kabla ya kuzaliwa. Mara chache sana, matatizo baada ya kuzaliwa yanasababisha ADHD.
ADHD ni tatizo la ubongo na wala si tatizo la tabia.
Watoto wana uwezekano mkobwa wa kupata ADHD ikiwa:
Wana ndugu mwenye ADHD (unarithishwa kwenye familia)
Alikuwa ana uzito chini ya 3 wakati wa kuzaliwa
Alipata jeraha kichwani au maambukizi ya ubongo
Alikuwa katika mazingira ya madini ya risasi, pombe, umbaku au kokeni kabla ya kuzaliwa
Dalili za ADHD ni zipi?
ADHD kwa watoto
Dalili za ADHD kwa watoto:
Kutoweza kumakinika
Shughuli za kimwili nyingi kupita kiasi
Mwenye mihemko sana (anafanya vitu bila kufikiri)
Ukilinganisha na watu wazima, watoto wote wana shida kidogo ya kuwa na umakinifu na kukaa wakiwa wametulia. Hata hivyo, watoto wenye ADHD wana matatizo zaidi kuliko watoto wengine
Ishara za matatizo ya kwua na umakini:
Kutosikiliza anaposemeshwa
Kutofuata maelekezo au kumaliza kazi
Kuepuka kazi ambazo zinahitaji kufikiri sana
Kupata shida kupangilia kazi
Kuchanganywa kwa urahisi
Kupoteza au kusahau vitu
Ishara za kukosa utulivu:
Kuriaria kwa mikono au miguu au kutembeza miguu
Kutoka kwenye viti vyao wakiwa shuleni au nyumbani
Kukimbia au kupanda juu ya vitu kuliko kawaida
Kupata shida kucheza kwa utulivu
Kuzungumza zaidi kuliko kawaida
Ishara za kufanya mambo kwa mihemko:
Kutoa majibu kabla swali halijakamilika kuulizwa
Kupata shida kusubiri zamu yake
Kuzungumza wakati si zamu yake kuwakatiza wengine
Watoto wengi wenye ADHD wanapunguza kidogo hali ya kutokuwa na utulivu wanapokuwa wakubwa na wanaweza kukabiliana vizuri na mazingira. Wengi watakuwa na kuwa watu wazima wenye tija na wabunifu. Hata hivyo, ADHD isiyotibika inaweza kusababisha uwezekano wa matumizi mabaya ya pombe, dawa za kulevya au kujinyonga.
ADHD kwa watu wazima
Dalili za ADHD kwa watu wazima:
Kupata shida kumakinika
Kupata shida kukamilisha kazi
Kutokuwa na utulivu
Mihemko ya hisia
Kutokuwa mvumilivu
Kupata shida kwenye mahusiano
Madaktari wanawezaje kujua ikiwa mtoto wangu ana ADHD?
Madaktari hushuku uwepo wa ADHD kutokana na dalili za mtoto wako. Hakuna vipimo vyovyote ambavyo vinaweza kusema kwa uhakika kuwa mtoto wako ana ADHD au la. Hata hivyo, madaktari wanaweza kuangalia endapo dalili za mtoto wako zinasababishwa na tatizo jingine, kama vile:
Je, madaktari wanatibu vipi ADHD?
Kumfokea au kumwadhibu mtoto wako hakusaidii. Madaktari watamtibu mtoto wako kwa kutumia:
Ushauri nasaha kuhusu namna ya kuboresha tabia (tiba ya tabia)
Dawa
Madaktari na washauri nasaha wanaweza kupendekeza kukusaidia wewe na mtoto wako kushughulika na ADHD. Mambo ambayo mara nyingi husaidia hujumuisha:
Kuweka utaratibu nyumbani na shuleni
Kutoa zawadi ndogo kwa tabia nzuri
Kudumu kuwa thabiti kuhusu tabia unayoitarajia
Kufanya kazi na walimu ili kutoa kazi na masomo mafupi shuleni
Mtoto mwenye ADHD huenda akahitaji usaidizi maalumu shuleni. Nchini Marekani, Sheria ya Elimu ya Watu Wenye Ulemavu (IDEA) inazitaka shule za umma kutoa elimu ya nzuri na ya bila malipo kwa watoto wenye ADHD.
Dawa za kutibu ADHD ni dawa kama vile Ritalin® na nyinginezo ambazo kimsingi zinaamsha ubongo. Unaweza kudhani mtoto wako tayari amechochewa sana. Hata hivyo, dawa hizi zinaamsha sehemu za ubongo wako ambazo zinasaidia mtoto wako kuwa na umakini.
Dawa za kuamsha ubongo zinaweza kuwa na athari:
Kushindwa kulala
Kupoteza hamu ya kula (watoto wanaweza kula kidogo sana na wakashindwa kukua vizuri)
Mapigo ya mayo ya haraka na shinikizo la juu la damu
Ili kupunguza athari, daktari wako anaweza kupendekeza uache kutumia dawa siku za wikendi na wakati wa likizo.