Ugonjwa wa Baridi Yabisi Uliosababishwa na Maambukizi Katika Sehemu Nyingine ya Mwili

Imepitiwa/Imerekebishwa Sept 2024

Ugonjwa wa baridi yabisi ni magonjwa ambayo husababisha viungo kupata maumivu, kuvimba na kuwa vyekundu. Kuna aina nyingi za ugonjwa wa baridi yabisi.

Ni nini maana ya ugonjwa wa baridi yabisi uliosababishwa na maambukizi katika sehemu nyingine ya mwili?

Ugonjwa wa baridi yabisi uliosababishwa na maambukizi katika sehemu nyingine ya mwili ni aina ya ugonjwa wa baridi yabisi unaotokana na athari za maambukizi mahali pengine mwilini. Ugonjwa wa baridi yabisi uliosababishwa na maambukizi katika sehemu nyingine ya mwili ni tofauti na maambukizi halisi ya ndani ya kiungo.

  • Dalili zinajumuisha maumivu ya viungo na kuvimba

  • Huenda pia ukawa na kano zilizofura, maumivu ya mgongo, upele, au macho mekundu

  • Dalili huanza siku au wiki kadhaa baada ya kupata maambukizi kwenye matumbo yako (gastroenteraitisi) au maambukizi ya zinaa (STI)

  • Madaktari wanaweza kujua ikiwa una ugonjwa wa baridi yabisi uliosababishwa na maambukizi katika sehemu nyingine ya mwili kulingana na dalili zako na kwa kufanya uchunguzi

  • Dawa zinaweza kusaidia kutibu dalili zako

Kwa watu wengi, ugonjwa wa baridi yabisi uliosababishwa na maambukizi katika sehemu nyingine ya mwili hutoweka baada ya miezi 3 au 4. Nusu ya watu wana dalili zinazokuja na kutoweka kwa kipindi cha miaka kadhaa. Viungo na uti wa mgongo vinaweza kuharibika umbo iwapo dalili hazitatoweka au zikiendelea kurudi mara kwa mara. Watu wachache wanaopata ugonjwa wa baridi yabisi uliosababishwa na maambukizi katika sehemu nyingine ya mwili hupata ulemavu wa kudumu.

Je, nini huleta ugonjwa wa baridi yabisi uliosababishwa na maambukizi katika sehemu nyingine ya mwili?

Aina mbili za maambukizi husababisha matukio mengi ya ugonjwa wa baridi yabisi uliosababishwa na maambukizi katika sehemu nyingine ya mwili:

  • Maambukizi ya zinaa (STI), aghalabu kwa wanaume walio na umri wa miaka 20 hadi 40

  • Maambukizi ya matumbo kutokana na bakteria fulani

Lakini watu wengi walio na maambukizi haya hawapati ugonjwa wa baridi yabisi kutokana na maambukizi hayo. Jeni fulani inayopatikana kwenye familia inaweza kufanya baadhi ya watu waugue ugonjwa tendaji wa baridi yabisi.

Ni zipi dalili za ugonjwa wa baridi yabisi uliosababishwa na maambukizi katika sehemu nyingine ya mwili?

Dalili za kawaida ni:

  • Maumivu, kufura, wekundu na joto kwenye kiungo kimoja au zaidi, kwa kawaida miguuni

  • Maumivu na kufura kwa kano na tendoni karibu na kiungo

  • Maumivu ya mgongo, ikiwa ugonjwa ni mkali

Pamoja na maumivu ya viungo, huenda ukajihisi mgonjwa na kuonyesha dalili kama vile:

  • Homa kiasi

  • Kuhisi uchovu mwingi

  • Kukosa hamu ya kula na kupoteza uzani

Unaweza pia kupata matatizo yasiyohusiana na viungo vyako. Kwa mfano, huenda:

  • Macho kuwa mekundu, kuwasha na wakati mwingine kutoona vizuri (kuvimba kwa uvea)

  • Vidonda kwenye mdomo wako

  • Upele mgumu mnene kwenye ngozi yako, hususan kwenye viganja na nyayo zako na karibu na kucha zako

Wakati mwingine maambukizi yaliyosababisha ugonjwa wa baridi yabisi huwa hayajakwisha. Huenda bado ukawa na:

  • Maumivu ukikojoa au kutokwa na majimaji kwenye uke au uume ikiwa una maambukizi ya STI

  • Kuendesha, ikiwa una maambukizi kwenye matumbo yako

Madaktari wanawezaje kujua iwapo nina ugonjwa wa baridi yabisi uliosababishwa na maambukizi katika sehemu nyingine ya mwili?

Madaktari wanaweza kujua iwapo una ugonjwa wa baridi yabisi uliosababishwa na maambukizi katika sehemu nyingine ya mwili kulingana na dalili zako na kwa kufanya uchunguzi. Huenda daktari pia:

  • Eksirei ili kuona jinsi viungo vyako vimeharibika

  • Vipimo vya damu vya kuhakikisha kuwa huna magonjwa mengine yanayoweza kusababisha ugonjwa wa baridi yabisi

  • Wakati mwingine, vipimo vya kuangalia majimaji kutoka kwenye kiungo kilichovimba

Ikiwa una dalili za maambukizi ya utumbo au STI, madaktari watatibu maambukizi hayo.

Madaktari hutibu vipi ugonjwa wa baridi yabisi uliosababishwa na maambukizi katika sehemu nyingine ya mwili?

Madaktari hutibu maambukizi yaliyosababisha ugonjwa wa baridi yabisi ikiwa hayajakwisha.

Madaktari wanaweza kupendekeza dawa za kusaidia kupunguza maumivu ya viungo na dalili zingine, ikiwa ni pamoja na:

  • Dawa za kupunguza uvimbe zisizo na steroidi (NSAID) ili kupunguza maumivu na kuvimba kwa viungo

  • Sindano za kotikosteroidi kwenye viungo vilivyofura

  • Wakati mwingine, dawa zinazodhibiti mfumo wako wa kingamwili ili kupunguza uvimbe.

Tiba ya mazoezi ya mwili inaweza kusaidia kulegeza viungo.

Matatizo ya macho na ngozi yanayotokana na ugonjwa wa baridi yabisi uliosababishwa na maambukizi katika sehemu nyingine ya mwili hayahitaji kutibiwa.