Je, mifupa ni nini?

Mifupa ni miundo migumu, imara inayoundwa kwa protini na madini kama vile kalisi.

Mifupa yako:

  • Hutoa muundo na umbile kwa mwili wako

  • Hulinda viungo vyako, kwa mfano, fuvu lako hulinda ubongo wako

  • Huhifadhi uboho wa mifupa yako, ambao huunda seli za damu

Mifupa ina tabaka la nje ambalo ni gumu na zito ambalo huifanya iwe na nguvu. Sehemu ya ndani ya mifupa ina vinyweleo (imejaa matundu madogo) vinavyoruhusu damu kutitirika ndani yake. Ndani ya mifupa kuna uboho wa mifupa. Nje ya mifupa kumefunikwa kwa shiti nyembamba ya tishu inayoitwa periosteamu, ambayo hurutubisha mfupa.

Je, mifupa hufanyaje kazi?

Mifupa huupatia mwili wako muundo na umbo na kuhurusu kutembea.

Je, viungo ni nini?

Viungo ni sehemu ambapo mifupa 2 hukutana.

Viungo vinashikiliwa pamoja na kano.

  • Kano ni tishu ya lastiki ngumu, yenye kupinda ambayo hukua kwa kukatisha fundo kuanzia mfupa mmoja hadi mfupa mwingine.

Viungo vina kano kadhaa mbalimbali ambazo huvishikilia pamoja. Kano na jinsi pande za mwisho za mifupa yako zilivyo husaidia viungo kusogea katika ulekeo fulani tu. Kwa mfano kiungo cha goti lako kinaweza kupinda na kunyooka lakini hakiwezi kusogea upande upande.

Baadhi ya viungo, kama vile bega lako, vinaweza kusogea kwa kiasi kikubwa. Viungo vingine, kama vile vinavyopatikana katikati ya mbavu na mgongo, husogea kidogo tu.

Kama ilivyo kwa kano, misuli huunganisha mifupa 2 kwenye kiungo. Pale misuli inapokaza, hufungua au kufunga kiungo.

Je, mifupa huwa inameaje?

Unapoona kiunzi cha mifupa unaweza kufikiri kuwa mifupa haiishi, kama ilivyo kwa mabomba au fimbo za mbao. Hata hivyo:

  • Mifupa ni tishu zinazoishi

  • Kama ilivyo kwa tishu zote zinazoishi, mifupa inahitaji kuletewa damu wakati wote ili kupata oksijeni na virutubishi

Mifupa ya watoto hukua kwa kuongezeka urefu kwenye pande za mwisho. Kuna sehemu laini kwenye sehemu za mwisho za mifupa ya watoto inayoitwa kisahani za ukuaji. Visahani vya ukuaji huunda mifupa mipya ambayo hurefusha mifupa. Wakati wa balehe, visahani vya ukuaji vya watoto hugeuka na kuwa mifupa migumu na hivyo mifupa yao huacha kurefuka.

Lakini hata mifupa ya watu wazima huvunjika na kuundwa upya katika mchakato unaojulikana kama kurekebishwa.

  • Katika kurekebishwa, tishu za mifupa ya zamani hubadilishwa taratibu kwa tishu za mifupa mipya

  • Kila mfupa katika mwili wako hurekebishwa kabisa kila baada ya miaka 10

Ili mifupa ikue na kurekebishwa, inahitaji ugavi wa kutosha wa kalsiamu, madini mengine, vitamini D na baadhi ya homoni.

Je, uboho wa mfupa hufanya kazi gani?

Mifupa mingi ina sehemu ya kati yenye vinyweleo (inamaanisha zimejaa vitundu vidogo) ambavyo vina uboho. Uboho umetengenezwa kwa seli (ikijumuisha seli shina) ambazo huzalisha seli za damu.

Je, mifupa inaweza kupata matatizo gani?

Matatizo ya mifupa ni pamoja na:

Uvimbe wa mifupa ambao unaweza kuwa wenye saratani au usio na saratani (usio wa hatari) Baadhi ya uvimbe wenye saratani huenea kwenye mifupa yako kutoka kwa viungo vingine.

Aina kadhaa za saratani, ikijumuisha myeloma nyingi, lukemia, na limfoma, zinaweza kukua kwenye uboho wa mifupa.