Utangulizi wa Biolojia ya Misuli na Mifupa

Imepitiwa/Imerekebishwa Apr 2024

Je, misuli na mifupa ni nini?

Misuli na mifupa huupatia mwili wako umbo na umbile na kukuwezesha kutembea. Ni sehemu ya mfumo wa kiunzi cha mifupa na misuli yako, ambacho hujumuisha:

  • Mifupa: Kiunzi chako cha mifupa

  • Misuli: Tishu ambayo hukaza ili kusogeza viungo vya mwili wako

  • Viungo: Eneo ambalo mifupa 2 hukutana

  • Gegedu: Tishu laini, zilizo sawa na mpira ambazo hufunika eneo la ndani ya viungo ili kupunguza msuguano

  • Tendoni: Kamba ngumu za tishu zinazounganisha misuli yako kwa mifupa yako

  • Kano: Lastiki ngumu za tishu zinazounganisha mfupa mmoja kwa mfupa mwingine na kushikilia viungo pamoja

Mwili wako una mamia ya misuli na mifupa mbalimbali. Baadhi ni mikubwa sana, kama vile misuli na mifupa mikubwa kwenye paja. Mingine ni midogo sana, kama vile misulil na mifupa ya vidole vyako.

Tendoni na kano huitwa tishu unganishi kwa sababu huunganisha sehemu za mwili wako pamoja.

Mfumo wa Kiunzi cha Mifupa na Misuli (1)

Mfumo wa Kiunzi cha Mifupa na Misuli (2)