Tatizo la Kula Kupita Kiasi

Imepitiwa/Imerekebishwa Jan 2024

Je, tatizo kula kupita kiasi ni nini?

Tatizo la kula kupita kiasi ni pale unapokula chakula kingi kwa haraka sana (kula kupita kiasi). Unapokula, unahisi kuwa hauwezi kuacha. Baada ya kula kupita kiasi, unajihisi vibaya sana kwa sababu haungeweza kujizuia. Kwa kawaida unakula sana hadi unakuwa na uzani uliopitiliza

Je, tatizo la kula kupita kiasi ni sawa na bulimia au anoreksia nervosa?

Hapana. Tatizo la kula kupita kiasi si sawa na matatizo mengine ya ulaji, yanayoitwa bulimia na anoreksia.

  • Bulimia navosa—unakula kupita kiasi lakini unajitapisha baadaye ili uwe na uzani wa kawaida

  • Anoreksia nervosa—huli chakula cha kutosha na wakati mwingine unajitapisha baada ya kula ili uwe mwembamba sana

  • Tatizo la kula kupita kiasi—unakula kupita kiasi lakini hujilazimishi kutapika na kwa kawaida una uzani mkubwa kupita kiasi

Je, nani anaweza kuwa na tatizo la kula kupita kiasi?

Wanaume na wanawake wanaweza kuwa na tatizo la kula kupita kiasi. Tatizo la kula kupita kiasi hutokea zaidi kuliko matatizo mengine ya kula kwa wanaume.

Watu wenye tatizo la kula kupita kiasi mara nyingi ni wazee kuliko watu wenye matatizo mengine ya kula.

Je, dalili za tatizo la kula kupita kiasi ni zipi?

  • Kula kupita kiasi na kuhisi kuwa huwezi kujidhibiti

  • Kula hadi kushiba kupita kiasi

  • Kula kiasi kikubwa cha chakula bila kuwa na njaa

  • Kula peke yake kwa sababu ya aibu

  • Kuhisi kuchukizwa, unyogovu, au hatia baada ya kula kupita kiasi

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina tatizo la kula kupita kiasi?

Madaktari wanaweza kujua kuwa una tatizo la kula kupita kiasi ikiwa una dalili na tabia za kawaida na:

  • Unakula kupita kiasi mara moja kwa wiki kwa angalau miezi 3

  • Unahisi kuwa hauwezi kudhibiti ulaji wako

Je, madaktari vipi tatizo la kula kupita kiasi?

Madaktari wanaweza kupendekeza:

  • Tiba ya kusaidia kuacha kula kupita kiasi

  • Mipango ya kupunguza uzani au dawa za kupunguza uzani ili kusaidia kudhibiti uzani

  • Aina ya dawa ya kupunguza unyogovu ili kusaidia kuacha kula sana na kudhibiti uzani