Saratani ya Zoloto

Imepitiwa/Imerekebishwa Apr 2024

Zoloto yako (sanduku la sauti) hushikilia nyuzi za sauti zinazokusaidia kutoa sauti. Zoloto hufanya uvimbe unaoweza kuona na kuhisi katikati ya shingo yako.

Saratani ya zoloto ni nini?

Saratani ya zoloto ni saratani ambayo iko kwenye zoloto yako.

  • Dalili ni pamoja na kukoroma kwa sauti yako ambayo haitoki, uvimbe kwenye shingo yako, na baadaye matatizo ya kupumua na kumeza.

  • Ni mojawapo ya saratani za kichwa na shingo zinazotokea mara kwa mara zaidi

  • Saratani ya zoloto ni ya kawaida zaidi kwa wanaume kuliko kwa wanawake, haswa wanaume zaidi ya miaka 60

  • Uvutaji sigara na unywaji pombe zaidi huongeza hatari ya kupata saratani ya zoloto

Muone daktari ikiwa umekuwa na kukwaruza kwa sauti ambako kmedumu kwa zaidi ya wiki 2 hadi 3.

Kuipata Zoloto

Nini husababisha saratani ya zoloto?

Madaktari hawajui kila mara kinachosababisha saratani ya zoloto, lakini sababu kubwa ni:

  • Kuvuta Sigara

Karibu kila mtu anayepata saratani ya zoloto ni, au alikuwa, mvutaji sigara.

Uwezekano wa kupata saratani ya zoloto pia ni mkubwa ikiwa wewe:

  • Ni mwanaume, haswa ikiwa una zaidi ya miaka 60

  • Ulikunywa pombe kupita kiasi kwa muda mrefu

Je, dalili za saratani ya zoloto ni zipi?

Dalili za saratani ya zoloto ni:

  • Sauti iliyopwelea (au mabadiliko katika sauti yako) ambayo haitoweki baada ya wiki chache

  • Maumivu ya koo au sikio

  • Uvimbe shingoni

  • Shida ya kupumua na kumeza

Je, madaktari wanaweza kujuaje kama nina saratani ya zoloto?

Madaktari wanaweza kufahamu ikiwa una saratani ya zoloto kwa kuchunguza zoloto yako. Wataweka mrija mwembamba wenye uwezo wa kutazama kinywani mwako.

Madaktari wanaweza pia kuchukua kipande cha tishu kwa ajli ya uchunguzi (kuondoa sampuli ya tishu yako kwa ajili ya kuipima). Uondoaji wa kipande cha tishu kwa uchunguzi kawaida hufanywa kwenye chumba cha upasuaji wakati umelela kutokana na nusukaputi ya jumla.

Ikiwa una saratani ya zoloto, madaktari wataona ikiwa saratani yako imeenea katika sehemu nyingine za mwili wako kwa kufanya vipimo kama vile:

Madaktari wanatibu vipi saratani ya zoloto?

Matibabu yanategemea kiasi cha ukuaji na ueneaji wa saratani.

Madaktari hutibu saratani ya mapema kwa kutumia mojawapo ya yafuatayo:

  • Upasuaji wa laser (kwa kutumia mwanga wa juu ili kukata saratani)

  • Tiba ya mionzi, hasa ikiwa saratani iko kwenye nyuzi zako za sauti

Matibabu haya kwa kawaida hayaathiri sauti yako.

Madaktari hutibu saratani iliyoendelea zaidi kwa mchanganyiko wa matibabu, kama vile:

  • Upasuaji pamoja na tiba ya mionzi, ikiwa madaktari wanafikiri upasuaji unaweza kuondoa saratani yote

  • Mionzi pamoja na tibakemikali, ikiwa madaktari wanafikiri kuwa saratani ni kubwa sana kuweza kuondolewa kwa upasuaji—hii kwa kawaida haiponyi saratani lakini inaweza kupunguza saratani na kupunguza maumivu.

Madhara ya matibabu

Takriban matibabu yote ya saratani ya zoloto yana madhara.

Upasuaji unaofanywa kwa saratani ya hali ya juu wakati mwingine huondoa yote au sehemu kubwa ya zoloto yako. Ikiwa zoloto yako imeondolewa, kuna mbinu za kukusaidia kuzungumza bila nyuzi za sauti.

Mionzi kwenye shingo inaweza kusababisha:

  • Ngozi nyekundu yenye mwasho

  • Kupoteza ladha

  • Mdomo mkavu

  • Matatizo kumeza vyakula

  • Matatizo ya meno, meno yakifikiwa na mionzi

Ikiwa una shida kumeza baada ya matibabu, madaktari wanaweza kuhitaji kunyoosha umio lako. Umio ni bomba la chakula ambalo hubeba chakula kutoka kinywani mwako hadi tumboni mwako.