Zoloto lako (pia huitwa kisanduku cha sauti) hujumuisha nyuzi za sauti. Lipo kwenye koo lako juu ya koo lako la sauti (trachea).
Kuvimba kwa zoloto ni nini?
Kuvimba kwa zoloto ni mwako (uvimbe) kwenye zoloto lako.
Kuvimba kwa zoloto mara nyingi husababishwa na virusi
Unaweza kupwelewa au kupoteza sauti yako
Kupumzisha sauti yako, kunywa viowevu kwa kiasi kikubwa na kuepuka vitu ambavyo vinakwaruza koo lako (kama vile kuvuta sigara) hukusaidia upate unafuu
Kuvimba kwa zoloto husababishwa na nini?
Kuvimba kwa zoloto kunakodumu chini ya wiki 3 kwa kawaida husababishwa na:
Mafua (kisababishi kikuu)
Maambukizi yoyote yanayokufanya ukohoe sana
Kutumia sauti yako kupita kiasi (kuzungumza au kuimba sana)
Mmenyuko wa mzio
Kuvuta hewa ya vitu vinavyokwaruza koo lako, kama vike moshi wa sigara
Kuvimba kwa zoloto kunakodumu zaidi ya wiki 3 huweza kusababishwa na mwako kutokana na:
Refluksi gastroesofajia, wakati chakula na asidi ya tumbo inarudi kwenye koo lako
Kikohozi kinachodumu muda mrefu
Bulimia, tatizo la kula ambapo watu wanajilazimisha kula kisha wanatapika chakula
Uvimbe kwenye kisanduku cha sauti
Dalili za kuvimba kwa zoloto ni zipi?
Dalili za kuvimba kwa zoloto ni:
Mabadiliko kwenye sauti yako
Kupoteza sauti yako
Koo linalowasha, linahisi kuwa bichi au linahitaji kusafishwa sana
Wakati mwingine, kulingana na kile kilichosababisha hali yako ya kuvimba kwa zoloto, unaweza pia kuhusi:
Homa
Matatizo kumeza vyakula
Koo kuuma
Madaktari wanawezaje kujua kama nina ugonjwa wa kuvimba kwa zoloto?
Madaktari wanasikiliza sauti yako unapozungumza. Wanaweza kujua ikiwa una ugonjwa wa kuvimba kwa zoloto kwa kusikiliza sauti yako.
Ikiwa una ugonjwa wa kuvimba kwa zoloto kwa wiki 3 au zaidi, huenda ukahitaji kufanyiwa vipimo vya kina zaidi. Daktari wako wanaweza kuangalia koo lako kwa kutumia kioo au kamera yenye umbo la nelo ili kukagua zoloto lako na kuwa na uhakika kuwa dalili zako si kwa sababu ya ukuaji usio wa kawaida.
Je, madaktari wanatibu vipi kuvimba kwa zoloto?
Daktari wako anaweza kukuomba:
Upumzishe sauti yako kwa kutozungumza sana au usizungumze kabisa
Tumia dawa ya kikohozi ya matone
Kunywa maji kwa wingi na viowevu vingine
Vuta hewa kwenye mvuke
Ikiwa unavuta sigara, acha.
Usijaribu kunong'ona, kupiga kelele au kutumia sana sauti yako kwa sababu hii inaweza kufanya hali yako ya kuvimba kwa zoloto kuwa mbaya zaidi.
Ikiwa hali yako ya kuvimba kwa zoloto imesababishwa na ugonjwa mwingine, kama vile refluksi gastroesofajia, bulimia au ukuaji kwenye zoloto lako, daktari wako atatibu ugonjwa huo.