Je, masikio ni nini?

Masikio ni kati ya ogani za hisia na yana kazi 2 muhimu:

  • Kusikia

  • Usawa

Je, sehemu kuu za masikio ni zipi?

Masikio yako yana sehemu 3 muhimu:

  • Sikio la nje

  • Sikio la kati

  • Sikio la ndani

Sikio la nje ni kile unachokiona kwenye sehemu ya nje ya kichwa chako. Ni kipande kikubwa cha gegedu ambalo limefunikwa kwa ngozi Njia inayoelekea kwenye sikio la kati inaitwa mfereji wa sikio.

Sikio la kati limeundwa kwa kiwambo cha sikio na nafasi ndogo iliyojazwa hewa. Nafasi hii ina mifupa midogo 3, ambayo imepewa majina kulingana na maumbo yake. Mifupa hii inaitwa nyundo, kifuawesikio, na mfupa katika sikio. Mifupa hii midogo husafirisha sauti kutoka sikio la kati hadi sikio la ndani.

Sikio la kati limeunganishwa na sehemu ya nyuma ya pua yako kwa bomba la eustachian Bomba hili husaidia kutoa majimaji, ili yasikusanyike ndani ya sikio la kati. Unapopata mafua, bomba hili linaweza kuvimba (kuwa jekundu na kuvimba) na kuziba, hali ambayo inaweza kusababisha maambukizi ya sikio.

Sikio la ndani limeundwa kwa komboli na mfumo wa usawa. Maumbo haya yamejazwa majimaji na yana vitambuzi ambavyo hubadilisha sauti na mwendo kuwa ishara za neva.

Ndani ya Sikio

Je, masikio hufanyaje kazi?

Je, kusikia kunafanyaje kazi?

Masikio yako huingiza mawimbi ya sauti na kuyabadilisha kuwa ishara za neva ambazo husafiri hadi kwenye ubongo. Ubongo wako hutafsiri ishara hizi kama sauti, kama vile sauti au muziki.

  • Mawimbi ya sauti huingia kwenye masikio yako na kusafiri hadi chini ya mfereji wa sikio hadi kwenye kiwambo cha sikio

  • Mawimbi ya sauti hufanya kiwambo cha sikio lako kutikisika

  • Mitikisiko ya kiwambo cha sikio husafiri kwenye mifupa midogo 3 ya sikio lako la kati

  • Mfupa mdogo wa 3 hutikisa sehemu ya sikio lako la ndani inayoitwa fenestra ovalisi

  • Mitikisiko kwenye fenestra ovalisi huingia kwenye komboli, ambayo hubadilisha mitikisiko kuwa ishara za neva

  • Ishara za neva kutoka kwenye komboli hupita kwenye neva ya kusikia hadi kwenye ubongo wako

Komboli ni ogani yenye umbo mzunguko iliyojaa majimaji. Katika komboli kuna maelfu ya vinywele vidogo sana vinavyoitwa vijisinga ambavyo hutikisika kwa kutikia sauti. Vijisinga tofauti huitika kwa masafa tofauti ya sauti. Baadhi huitika kwa sauti za chini kama vile ngoma. Baadhi huitika kwa sauti za juu kama vile kengele Baadhi ziko katikati. Ubongo wako unaweza kutambua ni vijisinga gani vinavyotuma ishara, hivyo kutambua kiwango cha sauti kilichoingia kwenye masikio yako.

Je, usawa unafanyaje kazi?

Mfumo wa vifuko na mabomba madogo ndani ya masikio yako hukusaidia kukaa kwa usawa. Vimfuko na mabomba haya madogo huitwa mfumo wa usawa.

Mfumo wako wa usawa umejazwa majimaji na uko sambamba na nywele ndogo sana zinazoitwa vijisinga.

  • Unaposogeza kichwa chako, majimaji yaliyopo kwenye mfumo wa usawa husogea

  • Majimaji yanayosogea hufanya vijisinga vipinde upande mmoja au mwingine

  • Uelekeo ambao vijisinga hupinda husababisha ishara maalum za neva

  • Ishara za neva kutoka kwenye vijisinga hupita kwenye neva ya vestibula hadi kwenye ubongo

  • Ubongo wako hutumia ishara za neva kufahamu ni upande gani ambao kichwa chako kinaelekea

Je, masikio yanaweza kupata matatizo gani?

Matatizo ya masikio ni pamoja na:

Ikiwa una matatizo ya mfumo wako wa usawa, unaweza kuhisi kizunguzungu au kisulisuli na una hatari ya kuanguka.