Upasuaji wa Kupunguza Uzani (Upasuaji wa Bariatriki)

Imepitiwa/Imerekebishwa Oct 2023 | Imebadilishwa Nov 2023

Je, upasuaji wa kupunguza uzani ni nini?

Upasuaji wa kupunguza uzani ni upasuaji wa tumbo au utumbo (au vyote viwili) ili kukusaidia kupunguza uzani. Pia inaitwa upasuaji wa bariatriki.

  • Wakati mwingine madaktari hupendekeza upasuaji wa kupunguza uzani kwa watu walio na unene wa kupindukia, hasa ikiwa wana matatizo ya kiafya yanayohusiana na uzani

  • Kuna taratibu nyingi tofauti za upasuaji

  • Baada ya upasuaji, bado utahitaji kufanya mabadiliko ya maisha yako nzima ya kile unachokula na kiasi chake

  • Upasuaji wa kupunguza uzani unaweza kupunguza matatizo ya kiafya yanayohusiana na uzani, kama vile kisukari

  • Upasuaji wa kupunguza uzani unaweza kuwa na ufanisi zaidi kuliko lishe lakini una athari za kando kubwa zaidi.

Ili kutimiza vigezo vya upasuaji wa kupunguza uzani, ni sharti:

  • Uwe umejaribu njia zingine za kupunguza uzani

  • Uwe na uwezo wa kimwili na kiakili wa kufanyiwa upasuaji

  • Uwe tayari kufuata maagizo ya daktari wako baada ya upasuaji kuhusu kile utakachokula, kiasi cha mazoezi utakayofanya, na wakati wa kufanyiwa vipimo vya ufuatiliaji

Je, madaktari hufanyaje upasuaji wa kupunguza uzani?

Tumbo lako ndipo mahali ambapo chakula huenda kwanza unapokimeza. Tumbo huanza kusaga chakula na kisha kukipeleka kwenye utumbo. Utumbo humaliza kusaga chakula na kufyonza virutubisho ndani ya mwili wako. Upasuaji wa kupunguza uzani hufanya kimoja au yote mawili kati ya haya yafuatayo:

  • Hufanya tumbo lako kuwa dogo ili kupunguza kiasi cha chakula unachoweza kula

  • Hufanya chakula kuruka sehemu ya matumbo yako ili chakula kidogo kiweze kufyonzwa

Upasuaji wa kawaida zaidi wa kupunguza uzani ni pamoja na:

Upasuaji wa kugawa tumbo katika vijisehemu ndiyo aina ya kawaida ya upasuaji. Baada ya upasuaji huu, tumbo lako linaweza kushikilia chakula kidogo tu. Chakula kinachotoka tumbo huruka sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo.

Daktari wako atapendekeza aina ya upasuaji wa kupunguza uzani unaokufaa.

Madaktari wanaweza kufanya baadhi ya upasuaji wa kupunguza uzani kwa kutumia laparoskopi. Badala ya kulikata tumbo lako, madaktari huweka bomba la kutazama (laparoskopi) na vifaa vya upasuaji kupitia mikato midogo kwa tumbo lako. Upasuaji unaotumia laparoskopi kwa ujumla ni salama na unapona haraka kuliko upasuaji wa (wazi) kawaida.

Kuruka Sehemu ya Njia ya Mmeng'enyo wa Chakula

Katika upasuaji wa kugawa tumbo katika vijisehemu, sehemu ya tumbo hutengwa kutoka kwa nyingine, na kuunda mfuko mdogo. Mfuko huo umeunganishwa na sehemu ya chini ya utumbo mdogo.

Kupunguza Chakula Kinachoingia Tumboni

Katika uwekaji wa mkanda unaoweza kurekebishwa tumboni ili kupunguza kiasi cha chakula unachokula, mkanda unaoweza kurekebishwa huwekwa karibu na sehemu ya juu ya tumbo. Huwawezesha madaktari kurekebisha ukubwa wa njia ya kupitisha chakula kupitia tumboni inapohitajika.

Je, ninapaswa kula nini baada ya upasuaji wa kupunguza uzani?

Huenda ukalazimika kusubiri kwa takriban wiki 4 ili kula chakula kigumu. Kwa muda wa wiki 2 za kwanza, utakunywa vinywaji vya protini. Kwa muda wa wiki 2 zinazofuata, unaweza kuanza kula vyakula laini, vilivyobondwa, au vilivyosagwa.

Unapoanza kula vyakula vigumu, daktari wako anaweza kupendekeza:

  • Kuuma chakula kidogo

  • Kutafuna chakula kwa uangalifu

  • Kutokula vyakula vyenye mafuta mengi na vyenye sukari nyingi, kama vile vyakula vyepesi, keki na kuki

  • Kula milo midogo pekee

  • Kutokunywa vinywaji unapokula vyakula vigumu

Ingawa kuwa na tumbo dogo husaidia kula kidogo, watu wengine bado hula sana. Watu wengine hunywa vinywaji vingi vinalivyochanganywa au vinywaji vingine vyenye kalori nyingi. Wengine huendelea kula hata wanapokuwa wameshiba na hivyo kulitandaza tumbo lao dogo hatua kwa hatua. Hata kama ulifanyiwa upasuaji, bado unapaswa kutilia maanani kile unachokula ili upunguze uzani na usiongezeke tena.

Pia, kwa sababu hufyonzi vyakula kama kawaida, unapaswa kuwa mwangalifu ili kupata vitamini vya kutosha, madini, protini na lishe nyingine muhimu.

Kubadilisha jinsi unavyokula inaweza kuwa ngumu. Kikundi cha ushauri nasaha au usaidizi kinaweza kusaidia.

Je, faida za upasuaji wa kupunguza uzani ni zipi?

Upasuaji wa kupunguza uzani unaweza kukusaidia kupunguza uzani ambao haungeweza kupunguza kwa kupunguza chakula unachokula. Pia, kikawaida unapoteza uzani mkubwa zaidi ukitumia upasuaji badala ya lishe.

Kupunguza uzani kunaweza kusaidia katika matatizo ya kiafya yanayohusiana na uzani, ikijumuisha:

Je, upasuaji wa kupunguza uzani ni salama kiasi gani?

Upasuaji wote una uwezekano wa kuwa na:

  • Maambukizi karibu na sehemu ya upasuaji

  • Kuganda kwa damu kwenye mapafu yako

  • Maambukizi ya mapafu (nimonia)

Upasuaji wa kupunguza uzani pia una uwezekano mdogo wa kusababisha:

  • Matumbo yaliyozibwa

  • Kuvuja kutoka kwa moja ya viunganisho vya upasuaji, jambo ambalo linaweza kusababisha maambukizi ya tumbo

  • Kuvuja damu kutoka kwa tumbo au utumbo, au katika sehemu ya tumbo

  • Matatizo ya mawe ya nyongo au kibofu cha nyongo

  • Mawe kwenye figo

  • Ugonjwa wa Jongo

  • Kutopata lishe ya kutosha kutoka kwa chakula chako

  • Kifo

Kutokana na hatari hizi, madaktari hufanya tu upasuaji wa kupunguza uzani kwa watu walio na unene wa kupindukia au ambao wana uzani mkubwa kupita kiasi na wana tatizo kubwa la kiafya linalohusiana na uzani. Wasiliana na madaktari wako kuhusu hatari za upasuaji.

Mpigie simu daktari wako mara moja ikiwa una dalili za maambukizi karibu na jeraha lako, kama vile:

  • Wekundu

  • Maumivu makali

  • Kuvimba

  • Harufu mbaya

  • Usaha

Mpigie simu daktari wako mara moja ikiwa una ishara hizi za tahadhari baada ya upasuaji:

  • Maumivu makali ya tumbo

  • Homa au mzizimo

  • Kutapika

  • Kuvuja Damu

  • Mapigo ya moyo ya haraka au ya inayoruka

  • Kuharisha

  • Kinyesi cheusi, kinachojivuta, chenye harufu mbaya

  • Kuishiwa na pumzi

  • Kutokwa jasho

  • Kupauka kwa ghafla

  • Maumivu ya kifua