Maambukizi ya Mfumo Mkuu wa Neva kwa Watoto Yanayosababishwa na Virusi

Imepitiwa/Imerekebishwa Dec 2023

Je, maambukizi ya mfumo mkuu wa neva yanayosababishwa na virusi (CNS) ni nini?

Mfumo wako mkuu wa neva (CNS) ni ubongo na uti wako wa mgongo. Maambukizi ya virusi yanaweza kuathiri kiungo kimoja au vyote viwili. Maambukizi yanaweza kusababisha:

Maambukizi ya CNS yanayosababishwa na virusi yanaweza kuwa mabaya sana.

  • Dalili ya kwanza kwa kawaida ni homa, ikifuatwa na hasira, kutotaka kula, kuumwa na kichwa, maumivu ya shingo, na wakati mwingine tukio la kifafa

  • Watoto wengi hupata nafuu, lakini wengine hupoteza fahamu na kufariki

  • Watoto wachache wana matatizo ya kudumu kama vile uziwi, matatizo ya akili, matukio ya kifafa, au udhaifu wa mkono au mguu

  • Madaktari hukinga majimaji ya uti wa mgongo ili kuona ikiwa mtoto wako ana homa ya uti wa mgongo au hali ya kuvimba kwa ubongo

  • Kwa kawaida hakuna matibabu maalum ya maambukizi ya virusi ya ubongo au uti wa mgongo

Je, maambukizi ya mfumo mkuu wa neva yanayosababishwa na virusi kwa watoto husababishwa na nini?

Maambukizi ya mfumo mkuu wa neva yanayosababishwa na virusi husababishwa na aina nyingi za virusi.

Watoto hupata virusi hivi kwa njia tofauti, kwa mfano:

  • Kutoka kwa mama yao wanapopita katika njia ya uzazi (virusi vya hepesi)

  • Kuumwa na wadudu walioambukizwa

  • Kupumua hewa karibu na mtu aliye na virusi

Je, dalili za maambukizi ya CNS yanayosababishwa na virusi kwa watoto ni zipi?

Dalili hutofautiana kulingana na umri.

Watoto wachanga huwa na:

  • Homa

  • Kutokua na furaha au kulia, hata wakati wameshikwa au kubembelewa—wakati mwingine kwa kilio kisicho cha kawaida, cha sauti ya juu

  • Kutapika

  • Kutokula vizuri

Kwa watoto wengine, ishara ya kwanza ni tukio la kifafa.

Watoto wanaweza kuwa na:

  • Maumivu ya kichwa

  • Shingo iliyokaza

  • Homa

  • Kwea hali mbaya ya kuvimba kwa ubongo, uvivu na kuchanganyikiwa vikifuatiwa na kupoteza fahamu na uwezekano wa kifo

Watoto wachanga na watoto walio na hali ya kuvimba kwa ubongo inayosababishwa na maambukizi ya virusi vya herpesi simpleksi, wanaweza kuwa na ishara za kuambukizwa katika sehemu zingine za mwili kama vile vipele vya madoadoa mekundu na vidonda vilivyojaa umajimaji kwenye ngozi, mdomoni, au karibu na macho.

Je, kuna matatizo yoyote yanayoletwa na maambukizi ya mfumo mkuu wa neva (CNS) yanayosababishwa na virusi?

Baadhi ya watoto wachanga na watoto hupata matatizo ya ubongo na neva baada ya kupata maambukizi. Wanaweza kuwa na:

  • Udhaifu katika mkono au mguu

  • Kupoteza uwezo wa kuona au kusikia

  • Mabadiliko katika namna wanavyofanya mambo

  • Matatizo ya kujifunza au ya tabia

  • Matukio ya kifafa yanayotokea na kisha kutoweka

Wakati mwingine matatizo haya huisha, lakini yanaweza kudumu.

Je, madaktari watajuaje ikiwa mtoto wangu ana maambukizi ya CNS yanayosababishwa na virusi?

Ili kujua ikiwa mtoto wako ana ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo au hali ya kuvimba kwa ubongo, madaktari hufanya:

  • Kinga majimaji ya uti wa mgongo

Katika kukinga majimaji ya uti wa mgongo, daktari huweka sindano kwenye sehemu ya chini ya mgongo ili kutoa majimaji karibu na uti wa mgongo. Wakati mwingine madaktari pia hufanya:

  • EEG (kipimo cha shughuli za umeme katika ubongo au electroencephalogram) ili kuona mawimbi ya ubongo ya mtoto wako

  • MRI (upigaji picha kwa mvumo wa sumaku) na uchanganuzi wa CT (tomografia ya kompyuta) wa ubongo wa mtoto wako

Je, madaktari hutibu vipi maambukizi ya CNS yanayosababishwa na virusi kwa watoto?

Huenda daktari:

  • Kuwatibu watoto hospitalini ili kuhakikisha wako mahali pasipo baridi kuwapa majimaji na dawa za homa au matukio ya kifafa

  • Kutibu maambukizi ya virusi vya herpes simplex kwa dawa ya kuzuia virusi kupitia mshipa wa damu wa mtoto wako (IV)

  • Wakati mwingine, kutibu uharibifu wa muda mrefu wa ubongo na neva kwa kumpa kotikosteroidi au dawa nyingine