Homa ya Uti wa Mgongo kwa Watoto

Imepitiwa/Imerekebishwa Oct 2023

Je, homa ya uti wa mgongo ni nini?

Homa ya uti wa mgongo ni maambukizi ya safu za tishu (zinazoitwa tando) zinazofunika ubongo na uti wa mgongo. Homa ya uti wa mgongo mara nyingi husababishwa na virusi, lakini aina hatari zaidi ya homa ya uti wa mgongo husababishwa na bakteria. Homa ya uti wa mgongo inayosababishwa na virusi na bakteria inaweza kusababisha matatizo ya ubongo.

  • Watoto wakubwa wenye homa ya uti wa mgongo huwa na shingo ngumu, homa na maumivu ya kichwa

  • Watoto wachanga wanaougua homa ya uti wa mgongo kwa kawaida huwa wakali (hata wanaposhikwa), hawali vizuri, au hutapika

  • Madaktari wanaweza kugundua kwamba mtoto wako ana homa ya uti wa mgongo kwa kinga majimaji ya uti wa mgongo na vipimo vya damu

  • Chanjo (dawa ambazo watoto wenye afya njema wanahitaji ili kusaidia kuwalinda kutokana na maambukizi fulani) zinaweza kusaidia kuzuia aina fulani za maambukizi ya bakteria ambayo husababisha ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo

  • Madaktari hutibu homa ya uti wa mgongo inayosababishwa na dawa za kuua bakteria

  • Watoto wengine hufa kutokana na ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo hata baada ya matibabu

Je, homa ya uti wa mgongo husababishwa na nini?

Homa ya uti wa mgongo husababishwa na maambukizi ya bakteria au virusi.

Homa ya uti wa mgongo kwa watoto waliozaliwa hivi karibuni kawaida hutokana na maambukizi ya bakteria kwenye damu. Maambukizi haya husababishwa na bakteria iliyo kwenye njia ya uzazi ya mama.

Watoto wachanga wakubwa na watoto kwa kawaida hupata homa ya uti wa mgongo kwa kutangamana na wengine ambao ni wagonjwa. Chanjo zimefanya baadhi ya vyanzo vya homa ya uti wa mgongo ya bakteria kuwa nadra sana.

Je, nani ana uwezekano mkubwa wa kupata homa ya uti wa mgongo?

Watoto wote wachanga na watoto wanaweza kupata homa ya uti wa mgongo, lakini baadhi ya watoto wako katika hatari kubwa zaidi. Sababu za hatari ni pamoja na:

  • Mfumo dhaifu wa kingamwili

  • Kutangamana na mtu aliyeugua homa ya uti wa mgongo ndani ya siku chache zilizopita

  • Kuwa na ugonjwa wa selimundu

  • Kutolewa kwa fizi (kiungo kilichoko juu kushoto ya tumbo) kwa sababu ya saratani au jeraha

  • Kasoro za kuzaliwa usoni au kichwani

Je, dalili za ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo ni zipi?

Dalili za ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo hutofautiana kulingana na umri. Katika watu wa umri wote, dalili za homa ya uti wa mgongo inayosababishwa na bakteria zinaweza kuwa mbaya zaidi haraka sana. "Ishara ya tahadhari" ni mtoto mgonjwa ambaye anapata usingizi usio wa kawaida au anayeanza kuwa kama aliyechanganyikiwa. Mtoto mgonjwa ambaye hajitambui kabisa ambaye hana tabia ya kawaida anahitaji kupelekwa hospitalini mara moja.

Kwa watoto walio na umri wa chini ya miezi 12, dalili za mapema ni pamoja na:

  • Kutooridhika na kuwa wakali hata wanaposhikwa

  • Kukataa kula, au kutokula vizuri

  • Kuwa na joto la juu au la chini

  • Kutapika

  • Upele

  • Kupata kifafa

  • Mahali laini palipovimba (fontaneli) kichwani mwa watoto wachanga walio chini ya miezi 3

Kwa watoto wakubwa na vijana, ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo mara nyingi huanza na mafua. Kisha wanapata dalili kama vile:

  • Homa

  • Maumivu ya kichwa

  • Shingo iliyokaza

  • Vifafa

Waangalie watoto walio na dalili hizi kwa karibu kwa sababu wanaweza kusinzia haraka au kuchanganyikiwa na watahitaji huduma ya dharura.

Je, madaktari wanawezaje kujua kama mtoto wangu ana ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo?

Madaktari watashuku ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo kutokana na dalili za mtoto wako. Ili kujua kwa hakika, madaktari wanaweza:

  • Kukinga majimaji ya uti wa mgongoo (kupenyeza sindano kwenye uti wa mgongo) ambapo daktari hutumia sindano kupata sampuli ya majimaji ya uti wa mgongo kutoka kwenye uti wa mgongo

  • Vipimo vya damu

Kabla ya kukinga majimaji ya uti wa mgongo kutoka kwa watoto, wakati mwingine madaktari hufanya uchunguzi wa upigaji picha zinazotimia mawimbi ya suti au uchanganuzi wa CT (tomografia ya kompyuta) ili kutafuta matatizo mengine.

Je, madaktari hutibu homa ya uti wa mgongo vipi?

Ikiwa mtoto ana homa ya uti wa mgongo inayosababishwa na bakteria, madaktari watampa:

  • Dawa za kuua bakteria kupitia kwenye mshipa wa damu (IV)

  • Wakati mwingine, kotikosteroidi kupitia kwa mshipa wa damu

Ikiwa mtoto wako ana aina fulani za homa ya uti wa mgongo unaosababishwa na virusi, madaktari wanaweza kumpa dawa za kuzuia virusi. Kwa kawaida, mtoto wako atapewa dawa za maumivu na homa tu, kama vile ibuprofen.

Hata baada ya matibabu, baadhi ya watoto na watoto wachanga hufa au kuwa na matatizo ya muda mrefu kutokana na ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo unaosababishwa na bakteria.

Je, ninawezaje kujikinga na ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo?

Chanjo zinaweza kuzuia visa vingi vya ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo unaosababishwa na bakteria.

Watoto ambao wametangamana na mtu ambaye ana ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo unaosababishwa na bakteria mara nyingi hupewa dawa za kuua bakteria ili kusaidia kuzuia maambukizi.