Ugonjwa wa Neva

Imepitiwa/Imerekebishwa Jun 2023

Je, ugonjwa wa neva ni nini?

"Nyuro-" hurejelea ubongo, uti wa mgongo na neva. Ugonjwa wa neva ni maumivu ambayo yanatokana na uharibifu au matatizo kwenye neva, uti wa mgongo, au ubongo wako.

  • Kwa kawaida ugonjwa wa neva husababishwa na uharibifu utokanao na jeraha au tatizo la kiafya

  • Dalili zinaweza kujumuisha hisia za kuungua au kusisimka, kuwa na hisia kali kwa mguso au baridi, au maumivu ya mchonyoto kwa ndani

  • Si rahisi kutibu ugonjwa wa neva, lakini dawa za kuzuia mfadhaiko na dawa za kuzuia kifafa (dawa za mshtuko) mara nyingi husaidia

Je, nini husababisha ugonjwa wa neva?

Sababu za ugonjwa wa neva ni pamoja na:

Mara nyingi madaktari wanapaswa kukata neva wakati wa upasuaji, hasa uapsuaji mkubwa kama wa kuondoa titi au kiungo. Wakati mwingine, hili husababisha ugonjwa mkali wa neva. Kama umekatwa kiungo, unaweza kuhisi kama vile mkono/mguu uliokatwa bado upo na ukapata maumivu makali sana. Hali hii huitwa maumivu ya hisia bandia za kiungo.

Je, dalili za ugonjwa wa neva ni zipi?

Dalili za ugonjwa wa neva ni pamoja na:

  • Hisia ya kuungua au kusisimka

  • Maumivu ya ndani

  • Kuwa na hisia kali za joto, baridi au mguso kidogo

Mara nyingi ugonjwa wa neva unakuwepo pale ambapo hakuna kitu chenye maumivu kilichokupata.

Ugonjwa wa neva unaweza kufanya iwe vigumu kufanya kazi au shughuli nyingine za kawaida za kila siku, hivyo kukufanya uwe na wasiwasi au mfadhaiko. Wasiwasi na mfadhaiko pia vinaweza kuchangia ugonjwa wa neva kuwa mbaya zaidi. Kutokufanya shughuli za kawaida pia hufanya misuli yako ipoteze nguvu, hivyo unazidi kutojishulisha zaidi.

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa una ugonjwa wa neva?

Madaktari wanaweza kujua kuwa una ugonjwa wa neva kwa kukuuliza kuhusu dalili zako na kukufanyia vipimo vya kimwili. Wakati mwingine, ili kujua chanzo cha ugonjwa wa neva, hukufanyia vipimo kama vile:

Je, madaktari hutibu vipi ugonjwa wa neva?

Madaktari watatibu chanzo cha ugonjwa wa neva, iwapo wataweza kukibaini. Pia watatibu ugonjwa wa neva kwa:

  • Dawa ya maumivu

  • Dawa za kuzuia msongo wa mawazo

  • Matibabu ya kimwili

  • Tiba ya shughuli za kila siku

  • Upasuaji iwapo utahitajika ili kupunguza shinikizo kwenye neva

  • Kuchangamsha kwa umeme (TENS)

  • Kizuizi cha neva