Kusambazia Moyo Damu
Sawa na tishu nyingine yoyote mwilini, msuli wa moyo sharti upokee damu yenye oksijeni, na uchafu uchujwe kupitia damu. Ateri ya kulia na ya kushoto, ambayo hutoka kwenye aota nje ya moyo, huingiza damu yenye oksijeni kwenye moyo. Ateri ya kulia hugawanyika kuwa ateri ya kando na ateri ya nyuma upande wa chini, iliyopo kwenye sehemu ya nyuma ya moyo. Ateri ya kushoto (inayojulikana kwa kawaida ateri kuu ya moyo ya kushoto) hugawanyika kuwa ateri inayozunguka moyo na ateri ya kushoto inayoshuka upande wa mbele. Mishipa ya moyo hubeba damu iliyo na uchafu kutoka kwenye misuli ya moyo na kuielekeza kwenye mshipa mkubwa ulio sehemu ya nyuma ya moyo unaoitwa sanasi ya moyo, ambayo hurejesha damu kwenye ateri ya kulia.