Kipindi cha Baada ya Kujifungua ni muda baada ya kupata mtoto. Kawaida inachukuliwa kuwa wiki 6 za kwanza.
Uterasi yako ni tumbo lako la uzazi. Ni kiungo ambacho kijusi hukua kabla ya kuzaliwa.
Je, maambukizi ya baada ya kujifungua ya uterasi ni nini?
Uterasi yako inaweza kuambukizwa baada ya mtoto kuzaliwa. Hii ni nadra lakini mbaya.
Maambukizi kwenye uterasi yako yanaweza kuanza punde tu baada ya kujifungua
Utakuwa na maumivu katika tumbo lako la chini, homa, na kutokwa na majimaji yenye harufu mbaya
Dawa za kuua bakteria za kawaida huponya maambukizi
Ni nini husababisha maambukizi ya uterasi baada ya kujifungua?
Bakteria wanaoishi ndani na karibu na uke wako wanaweza kuambukiza uterasi yako baada ya kujifungua.
Una hatari kubwa ya kupata maambukizi ya uterasi baada ya kujifungua ikiwa una:
Vipimo vingi vya uke wakati wa uchungu wa uzazi
Kipindi kirefu cha uchungu wa uzazi
Kujifungua kwa njia ya upasuaji badala ya kujifungua kwa njia ya uke
Wakati mwingine, madaktari wanakupa dawa za kuua bakteria kabla ya Kujifungua kwa njia ya upasuaji ili kusaidia kuzuia maambukizi.
Je, dalili za maambukizi ya uterasi ni zipi?
Dalili kawaida huanza siku 1 hadi 3 baada ya kujifungua na ni pamoja na:
Maumivu katika tumbo lako la chini
Homa na mzizimo
Kwa ujumla kujisikia mgonjwa
Kutokwa umajimaji wenye harufu kwenye uke wako
Madaktari wanawezaje kujua kama nina maambukizi ya uterasi baada ya kujifungua?
Madaktari wanaweza kujua kwa kukuchunguza. Wanaweza kufanya vipimo kwa sababu nyingine za maumivu na homa, kama vile maambukizi ya njia ya mkojo (UTI).
Madaktari hutibu vipi maambukizi ya uterasi baada ya kujifungua?
Madaktari hukulaza hospitalini na kukupa dawa za kuua bakteria kwa mshipa (IV).