Kingamimba ya Dharura

Imepitiwa/Imerekebishwa May 2023

Kingamimba ya dharura ni nini?

Kingamimba ya dharura ni mbinu ya kupanga uzazi (kitu kinachotumiwa kuzuia ujauzito) unayotumia baada ya kushiriki katika tendo la ngono. Unaweza kuitumia iwapo umeshiriki tendo la ngono bila mbinu ya kupanga uzazi au iwapo mbinu yako ya kupanga uzazi haijafaulu, kwa mfano kondomu ikipasuka.

Kuna aina 2 kuu za kingamimba za dharura:

Mbinu hizi huitwa "za dharura" kwa sababu unapaswa kuwa unatumia mbinu zingine za kukuzuia usiwe mjamzito. Hupaswi kutegemea kufanya kitu baada ya kushiriki tendo la ngono.

  • Tumia kingamimba ya dharura haraka uwezavyo baada ya kushiriki tendo la ngono ili usiwe mjamzito—kadiri unavyoitumia haraka ndivyo unavyopunguza uwezekano wa kupata ujauzito

  • Unaweza kupata aina kadhaa tofauti za dawa zinazofanya kazi kama tembe za kingamimba ya dharura

  • Kuweka IUD ya shaba ndiyo mbinu yenye ufanisi zaidi ya kingamimba ya dharura na itaendelea kuzuia ujauzito kwa hadi miaka 10 (au hadi itakapotolewa)

Ni zipi aina za kingamimba ya dharura?

Tembe hutumiwa sana kama mbinu ya dharura za kuzuia ujauzito, lakini IUD ya shaba hufanya kazi vizuri zaidi na huendelea kutoa kinga dhidi ya kupata mimba.

Dawa za kingamwili ya dharura (tembe za dharura)

Hizi ni tembe unazomeza punde baada ya kushiriki tendo la ngono ili kuzuia usiwe mjamzito.

Kuna aina kadhaa tofauti za tembe za dharura:

  • Levonorgestrel ni lazima imezwe ndani ya siku 3 baada ya tendo la ngono—nchini Marekani inapatikana kwenye kaunta (bila agizo la daktari) katika maduka ya dawa

  • Ulipristal ni lazima imezwe ndani ya siku 5 baada ya tendo la ngono—unahitaji agizo la daktari ili uipate

  • Tembe za kupanga uzazi za mseto (dawa za kuzuia mimba), zinazotolewa kwa agizo la daktari zinaweza kutumiwa lakini wakati mwingine zinaweza kusababisha kichefuchefu na kutapika

Levonorgestrel hufanya kazi vizuri zaidi ukiimeza haraka iwezekanavyo baada ya tendo la ngono. Haifanyi kazi vizuri sana kwa wanawake wenye uzani kupita kiasi

IUD za Shaba

IUD ya shaba ni kifaa kidogo cha plastiki chenye umbo la T kilichofungwa kwa waya wa shaba kinachowekwa kwenye uterasi (mfuko wa uzazi) ili kuzuia mimba.

  • Ni lazima IUD ya shaba iwekwe na daktari wako

  • Ni lazima uhakikishe imewekwa ndani ya siku 5 baada ya kushiriki tendo la ngono

  • IUD hiyo inaweza kuachwa ndani itumike kama mbinu ya kupanga uzazi kwa hadi miaka 10