Molaskam kontagiosam ni nini?
© Springer Science+Business Media
Molaskam kontagiosam ni maambukizi ya ngozi ambayo husababisha uvimbe mdogo wa waridi au mweupe wenye umbo la kuba yenye pengo katikati.
Molaskam kontagiosam husababishwa na virusi na huenea kwa urahisi kutoka kwa mtu hadi mtu
Unaweza kupata molaskam kontagiosam kwa kugusa ngozi ya mtu aliyeambukizwa, kugusa kitu baada ya mtu aliyeambukizwa kukigusa, au ndani ya maji, kama vile vidimbwi vya kuogelea
Molaskam kontagiosam inapatikana sana kwa watoto
Watu walio na mfumo wa kingamwili dhaifu (kama vile watu walio na VVU/UKIMWI) wanaweza kuwa na maambukizi makali zaidi
Uvimbe kwa kawaida huondoka wenyewe baada ya mwaka mmoja au miwili, lakini unaweza kudumu hadi miaka 3
Dalili za molaskam kontagiosam ni zipi?
Dalili kuu ni:
Uvimbe ya waridi au meupe yasiyo na maumivu yaliyo chini ya robo ya inchi (karibu sentimeta 0.2 hadi 0.5) ambayo yana umbo la kuba lenye dimple katikati.
Uvimbe unaweza kuwa mwekundu sana na kuwasha—wakati fulani hii hutokea unapokaribia kutoweka. Lakini ikiwa utajikuna, unaweza kuupata zaidi kwa kueneza virusi kwenye ngozi karibu na uvimbe.
Unaweza kupata uvimbe popote kwenye ngozi yako isipokuwa viganja vya mikono na sehemu za chini za miguu yako.
Watoto walio na molaskam kontagiosam mara nyingi huwa na uvimbe usoni, shingoni, kifuani na kwapani
Watu wazima mara nyingi huwa na uvimbe kwenye uume, uke, au kwenye mapaja na sehemu ya chini ya tumbo
Madaktari hutibu vipi molaskam kontagiosam?
Madaktari kwa kawaida hawatibu molaskam kontagiosam kwa sababu hutoweka yenyewe baada ya mwaka mmoja au miwili. Lakini inaweza kutibiwa ikiwa uvimbe unakusumbua. Ikiwa wewe ni mtu mzima uliye na uvimbe karibu na sehemu zako za siri, unapaswa kuutibu ili usiueneze kwa wenza unaoshiriki nao ngono.
Huenda daktari:
Uondoe kwa kuugandisha
Uchome kwa na leza au umeme
Ondoa msingi wa uvimbe kwa sindano na uukwangue
Hukupa dawa kama mafuta ya kupaka
Unaweza kuzuia vipi molaskam kontagiosam?
Funika uvimbe kwa watoto (kwa mfano kwa bendeji) ili uvimbe usienee kwa wengine. Mtoto wako bado anaweza kuenda shuleni au kwenye malezi ya watoto.
Ili kuzuia molaskam kontagiosam kuenea kwa watu wengine:
Nawa mikono mara kwa mara
Usiruhusu mtu yeyote kutumia taulo yako au vitu vingine vya binafsi
Endelea kufunika uvimbe kwa bendeji, haswa wakati uko karibu na watu wengine