Usaha kwenye Jino

(Usaha kwenye Jino)

Imepitiwa/Imerekebishwa Mar 2024

Usaha kwenye jino ni nini?

Usaha ni mkusanyiko wa udusi. Udusi ni mchanganyiko wa seli nyeupe za damu, tishu zilizokufa na bakteria. Hujikusanya wakati ambao mwili wako unapigana na maambukizi.

Usaha kwenye jino ni usaha ambao unajikusanya kando ya mzizi wa jino lako. Usaha mkali unaweza kuenea kwenye ufizi, mashavu au mfupa wako wa taya.

Je, ni nini husababisha usaha kwenye jino?

Usaha kwenye jino unasababishwa na bakteria ambayo huingia kwenye fofota ya jino lako au kwenye ufizi unaozunguka jino. Fofota inaweza kupata maambukizi wakati una pengo lililoingia ndani sana au jino lililovunjika.

Mwili wako huvamia maambukizi kwa idadi kubwa za seli nyeupe za damu. Seli nyeupe za damu zilizokufa huwa udusi ambao huunda usaha.

Jino

Je, dalili za usaha kwenye jino ni zipi?

Usaha kwenye jino husababisha:

  • Maumivu ya jino yasiyoisha ambayo huwa mabaya zaidi unapotafuna chakula

  • Kuhisi chakula moto au baridi

  • Uvimbe kwenye ufizi wako

  • Wakati mwingine, homa

  • Wakati mwingine, kuvimba kwa taya yako, sehemu ya chini ya mdomo au mashavu yako

  • Wakati mwingine, ugumu katika kufungua mdomo wako au kumeza

Hatimaye jipu linaweza kupasuka, hivyo kuacha usaha utoke

Madaktari wa meno hutibu usaha kwenye jino vipi?

Madaktari wa meno hukupea dawa ya maumivu na dawa za kuua bakteria na kutibu usaha kwa:

  • Kutoa usaha kwa njia ya upasuaji au tiba ya fofota

Tiba ya fofota ni utaratibu wa meno ili kuondoa sehemu nyororo kutoka kwenye jino lako. Kisha daktari hujaza na kufunika mfereji wa jino.