Matundu kwenye meno

Imepitiwa/Imerekebishwa Mar 2024

Sehemu ngumu ya nje kwenye meno yako inaitwa enameli. Fofota imeingia ndani ya jino sana na inajumuisha mishipa ya damu na neva. Bakteria zinaweza kuharibu sehemu tofauti za jino.

Je, mapengo ni nini?

Mapengo ni sehemu dhoofu za jino lako.

  • Bakteria hukusanyika kwenye gamba la jino lako na hutengeneza asidi ambazo zinasababisha mashimo kwenye jino—mashimo hayo yanaitwa mapengo

  • Maumivu ya jino hufanyika vile mapengo yanakuwa makubwa na hupitia kwenye gamba la jino hadi kwenye sehemu ya ndani ya jino lako

  • Madaktari wa meno hupata mapengo kwa kuangalia jino lako na kuchukua eksirei

  • Matibabu yanajumuisha kutoa sehemu iliyooza na kujaza shimo

  • Kupiga mswaki meno yako mara kwa mara, kufanyiwa ukaguzi wa meno na kuepuka vyakula vyenye sukari kunaweza kusaidia kuzuia mapengo

Jino

Je, nini husababisha mapengo?

Bakteria hukusanyika kwenye meno yako na kutengeneza asidi ambayo husababisha kuoza.

Bakteria, mate (mate), vijipande vya chakula huunda tabaka nyembamba inayoitwa utando ambayo hujishikilia kwenye meno yako. Utando huwa ngumu baada ya muda na hugeuka kuwa ukoga. Kwa kawaida ukoga huwa wa rangi ya manjano. Wakati mwingine unaiona kwenye sehemu ya chini ya meno. Bakteria zinazoishi kwenye utando na ukoga ni ngumu kuzimaliza.

Bakteria huishi kwa kula sukari. Ndiyo kwa sababu vyakula na vinywaji vyenye sukari vinaweza kusababisha mapengo. Kiwango cha sukari ambayo unakula si muhimu sana kuliko mara ambayo unakula sukari. Cha muhimu ni kiasi cha muda ambao sukari inagusana na meno yako. Kunywa kinywaji kisicho na pombe polepole kwa zaidi ya saa kunaharibu sana kuliko kula baa ya pipi kwa dakika 5, hata kama baa ya pipi inaweza kuwa na sukari zaidi. Watoto ambao huenda kulala wakiwa na chupa, hata kama iko na mazima au fomula pekee, pia wako kwenye hatari ya kupata mapengo. Chupa za wakati wa kulala zinapaswa kuwa na maji pekee.

Una uwezekano mkubwa wa kupata mapengo ikiwa:

  • Una utando au ukoga mwingi kwenye mdomo wako

  • Unakula na kunywa vyakula vyenye sukari au asidi, kama vile soda ya kola au juisi

  • Una floraidi kidogo sana (madini ambayo hufanya gamba lako la meno liwe ngumu) kwenye meno yako

  • Hauna mate mingi (mate) kwenye mdomo wako (hali inayoitwa mdomo mkavu)

  • Una ufizi ambao umefifia chini kwenye sehemu ya chini ya meno yako (ufizi ambao unashuka)

Je, dalili za mapengo ni zipi?

Pengo la juu juu kwenye gamba la meno yako halina maumivu. Mapengo ambayo yameenda ndani kidogo yanaweza kusababisha maumivu unapokula vyakula na kunywa vinywaji moto, baridi au vyenye sukari.

Pengo ambalo limeingia ndani vya kutosha kufikia fofota linasababisha palpitisi. Palpitisi husababisha maumivu ya meno hata wakati haukuli au kunywa. Fofota ikiambukizwa, unaweza kupata mfuko wa usaha unaoitwa usaha kwenye jino.

Madaktari wa meno wanawezaje kujua kuwa nina mapengo?

Madaktari wa meno hutambua mapengo kwa:

  • Kuangalia meno yako na kuyachunguza kwa kutumia zana za meno

  • Kuchukua eksirei za meno yako

Madaktari wa meno hutibu mapengo vipi?

Ikiwa pengo lako ni ndogo sana na liko kwenye gamba la meno yako pekee, jino linaweza kujirekebisha lenyewe ikiwa una floraidi ya kutosha.

Madaktari wa meno hutibu mapengo ambayo yameingia ndani sana kuliko gamba la meno kwa kutoa sehemu ya jino iliyooza na kuweka kijazio. Kijazio kinaweza kuwa cha:

  • Mchanganyiko wa fedha (mchanganyiko wa fedha, zebaki, shaba nyekundu, bati na wakati mwingine metali zingine), mara nyingi zinatumiwa kwenye meno ya nyuma ambapo haitaonekana

  • Mchanganyiko wa resini, ambao unalingana na rangi ya meno yako

  • Ionoma ya kioo, ambayo ina rangi ya meno na huachilia floraidi, nzuri kwa watu walio na kuoza kwingi kwa meno

  • Dhahabu

Matibabu ya tiba ya fofota au kutolewa kwa meno

Kuoza kwa jino kukienda ndani vya kutosha kufikia fofota na inakuwa na mwasho mkubwa, madaktari wa meno watakupatia dawa ya maumivu na aidha:

  • Fanya tiba ya fofota ili kuondoa tishu mbovu kwenye jino lako kisha uzibe mwanya kwenye jino

  • Ng'oa jino ikiwa limeharibika kabisa

Ikiwa una maambukizi, utapewa dawa za kuua bakteria.

Je, ninawezaje kuzuia mapengo?

Unaweza kuzuia mapengo kwa:

  • Kupiga mswaki meno yako kwa dawa ya meno ambayo iko na floraidi (asubuhi na jioni na baada ya kula vyakula vyenye sukari)

  • Kutumia uzi kutoa uchafu kwenye meno yako kila siku

  • Kupata huduma ya meno ya mara kwa mara

  • Kula vyakula vyenye afya na kupunguza vyakula na vinywaji ambavyo vina sukari na asidi nyingi

Ni muhimu kupata floraidi ya kutosha. Floraidi ni madini ambayo hulinda meno yako yasipate mapengo. Floraidi inaongezwa kwenye usambazaji wa maji ya umma katika baadhi ya maeneo. Ikiwa haiko kwenye maji yako, daktari wa meno anaweza kukuandikia bidhaa za ziada za floraidi kwa watotowa hadi umri wa miaka 8, au kutumia matibabu ya floraidi kwenye meno yako.

Ikiwa bado unapata mapengo mengi, madaktari wa meno wanaweza:

  • Weka vifunikaji kwenye meno yako (vifunikaji ni kitu kigumu cha plastiki cha kufunika ambacho huzuia mapengo kwenye meno kwa mianya mikubwa)

  • Kukwambia utumie kisukutua cha mdomo chenye dawa ya kuua bakteria ambacho husaidia kuua bakteria inayosababisha pengo