Matatizo ya hofu (Fobia)

Imepitiwa/Imerekebishwa Dec 2022

Je, tatizo la hofu kupita kiasi ni nini?

Fobia ni neno la kimatibabu la hofu. Ni kawaida kuogopa vitu hatari. Watu wengi wanaogopa vitu kama vile kusimama kwenye ukingo wa mwamba au kumkaribia mbwa anayebweka.

Hata hivyo, tatizo la hofu kupita kiasi ni wakati hofu (hofu kupita kiasi) inakuwa:

  • Isiyo halisi

  • Kubwa kuliko hatari halisi

  • Kubwa sana kiasi cha kukuzuia kufanya shughuli za kawaida

Kwa mfano, unaweza kuwa na tatizo la hofu kupita kiasi ikiwa unaogopa urefu sana hata huwezi kufanya kazi katika jengo refu, au hivyo unaogopa wanyama sana hata huwezi kuwapeleka watoto wako kwenye bustani la wanyama.

  • Kuwa karibu na kitu unachohofia kunaweza kusababisha shambulio la hofu

  • Matibabu hufanyika kwa kutumia tiba ya kufichua, ambapo hatua kwa hatua unazoea kitu ambacho unahofia

Kuna hofu nyingi, lakini baadhi ya hofu kawaida ni pamoja na:

  • Wanyama (hofu ya wanyama)

  • Urefu (hofu ya urefu)

  • Maeneo yaliyofungwa (hofu ya kufungiwa)

  • Mvua ya radi (hofu ya mwale wa radi au muungurumo wa radi)

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina tatizo la hofu kupita kiasi?

Hakuna tofauti kubwa kati ya hofu ya kawaida na tahadhari na tatizo la hofu kupita kiasi. Hata hivyo, madaktari watashuku kuwa una tatizo la hofu kupita kiasi ikiwa una hofu ambayo:

  • Hukufanya ubadilishe tabia yako ili kuepuka hali au kitu hicho

  • Ni kubwa zaidi kuliko inavyopaswa ikilinganishwa na kiwango halisi cha hatari

  • Husababisha hofu kubwa sana au hufanya iwe vigumu kwako kufanya kazi

Je, madaktari hutibu vipi matatizo ya hofu kupita kaisi?

Inawezekana hauhitaji matibabu ikiwa mara chache unakutana na kitu unachokiogopa. Kwa mfano, ikiwa unaogopa nyoka lakini unaishi mjini, labda hutawahi kukutana na nyoka, kwa hivyo hofu yako si tatizo. Lakini ikiwa hofu yako ni kuhusu kitu ambacho ni vigumu kuepuka, kama vile kuendesha gari juu ya daraja, matibabu yanaweza kurahisisha maisha yako zaidi. Matibabu yanajumuisha:

  • Tiba ya kuzoesha kitu unachokiogopa (hii husaidia watu 9 kati ya 10)

  • Wakati mwingine, dawa za kupunguza wasiwasi hutumiwa kwa muda mfupi kutibu dalili

Katika tiba ya kumzoesha mtu kitu anachokiogopa, mtaalamu wa tiba hukusaidia hatua kwa hatua kuzoea kitu unachokihofia. Kwa mfano, ikiwa unaogopa mbwa:

  • Unaweza kuanza tu na kutazama picha za mbwa

  • Mtaalamu wa tiba hukusaidia kuwa mtulivu na kufanya kupumua kwako kuwa polepole hadi ujihisi vizuri kutazama picha

  • Kisha unaweza kutazama mbwa halisi aliye katika chumba kingine

  • Kisha hatua kwa hatua hadi kuwa katika chumba kimoja na mbwa

  • Kisha unaongozwa kumgusa mbwa huyo

Kawaida, unahitaji vikao vichache tu vya tiba ya kukuzoesha ili ifanikiwe.

Dawa hazimalizi hofu kabisa. Lakini dawa ya kupunguza wasiwasi zinaweza kusaidia pale ambapo huwezi kuepuka kufanya jambo ambalo unalihofia. Kwa mfano, daktari anaweza kukupa dawa ya kunywa kabla ya kupanda ndege.